Arusha: Lema arudishwa mahabusu, kesi yaahirishwa tena

Arusha: Lema arudishwa mahabusu, kesi yaahirishwa tena

Francis12

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2016
Posts
7,533
Reaction score
22,289
Jana baada kusikilizwa kesi ya Mbunge Lema.
Arusha. Wakati askari polisi saba watatoa ushahidi mahakamani katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, Mahakama imetoa onyo kwa askari Polisi na Magereza wanaowasumbua waandishi wa habari na wananchi.

Onyo hilo lilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha, Augustino Rwezile baada ya askari Magereza wakiwa na silaha kuwafukuza waandishi wa habari waliotaka kuchukua kumbukumbu za Lema kufikishwa mahakamani.

Pia, aliwaonya Polisi ambao wamekuwa wakilalamikiwa kwa kuwazuia wananchi wanapokwenda kusikiliza kesi ya mbunge huyo.

Leo Alhamisi kuanzia majira ya saa mbili asubuhi Jeshi la Polisi wamezuia wananchi pamoja na waandishi wa habari kuingia ndani eneo la mahakama kufutilia kesi ya Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema.

Jeshi la Polisi Arusha wamedharau Amri ya Hakimu Rwezile ambayo ametoa jana.
Nje ya mahakama Arusha kesi ya Lema
tmp_8621-IMG-20161117-WA00081970742980.jpg

My take: Jeshi la Polisi wanatoa wapi mamlaka ya kudharau Amri ya Mahakama kupitia Hakimu Rwezile?

=====================

#Arusha_Update : Watu wameshaingia kwa nguvu mahakamani ukumbini tayari kusikiliza kesi inayomkabili Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema na ukumbi umejaa.

Wakili wa serikali anajaribu kuishawishi mahakama itupilie mbali maombi ya kurevew maamuzi ya awali bali ijikite kwenye rufaa.

Wakili Kibatala anatetea uamuzi wa kuleta revew anasema maamuzi ya mahakama hayakufata sheria. Anasema pia utetezi wa serikali hauna msingi.

Wakili Kibatala
Mamlaka ya mahakama kuu ni supervisory not revisiory power.

Kifungu cha 372 kinairuhusu mahakama kuu kupitia mienendo ya mahakama za chini.Kibatala anaendelea kufafanua.

Wakili Kibatala
Sio njia ngeni kwa mahakama kuu kupitia mienendo ya mahakama za chini.

Hapo anaelezea jinsi hakimu alivyotoa maamuzi kinyume cha sheria
Wakili Kibatala. Anasema Lema aliomba dhamana akapatiwa.Kabla ya mahakama haijaweka masharti ya dhamana,serikali ilibreak notes of appeal.Hakukuwa na tatizo katika dhamana.

Wakili Kibatala
Rufaa inaweza kukatwa kama umenyimwa dhamana na sio kupinga kupewa dhamana.

Wakili Kibatala
Procidures hazikatiwi rufaa.anasema mahakama ilijivua madaraka kwa kuwa haikuelekezwa vizuri.Hapa anamsema hakimu aliyemmyima Lema dhamana.

Wakili Kibatala
Hakimu alikosea kumruhusu wakili wa serikali kusimama wakati wa kutoa masharti ya dhamana ni kosa la kisheria kwa mahakama.

Bado Wakili Kibatala anafafanua hoja anamponda wakili wa serikali.
Mabishano makali ya Kisheria yanaendelea kati ya mawakili wa Lema na wakili wa Serikali.

Kesi ya jinai no 440, 441 inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema imearishwa hadi Tarehe 22-11-2016 siku ya Jumanne hivyo basi Mh Mbunge kurudishwa tena Magereza.
 
Jana baada kusikilizwa kesi ya Mbunge Lema.
Hakimu Mkazi Arusha, hakimu Rwezile aonya askari kutoingilia uhuru wa korti pia awaonya Jeshi la Polisi kuhusu kuzuia wananchi kusikiliza kesi mahakamani.
Leo Alhamisi kuanzia majira ya saa mbili asubuhi Jeshi la Polisi wamezuia wananchi pamoja na waandishi wa habari kuingia ndani eneo la mahakama kufutilia kesi ya Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema .
Jeshi la Polisi Arusha wamedharau Amri ya Hakimu Rwezile ambayo ametoa jana.
My take=Jeshi la Polisi wanatoa wapi mamlaka ya kudharau Amri ya Mahakama kupitia Hakimu Rwezile?

Hakimu ana mamlaka ya kutoa amri kwa jeshi la polisi katika utawala wa sheria?
 
Hakimu ana mamlaka ya kutoa amri kwa jeshi la polisi katika utawala wa sheria?
Duh kumbe hutambui hilo?
Pia, aliwaonya Polisi ambao wamekuwa wakilalamikiwa kwa kuwazuia wananchi wanapokwenda kusikiliza kesi ya mbunge huyo.
 
Duh kumbe hutambui hilo?
Pia, aliwaonya Polisi ambao wamekuwa wakilalamikiwa kwa kuwazuia wananchi wanapokwenda kusikiliza kesi ya mbunge huyo.

Yaani hakimu anafahamu kuwa wale wanaozuiwa nje ya mahakama wamekwenda kusikiliza kesi ya Lema na hivyo kutoa amri? Labda uwasilishaji ndio mgumu, Napata shida kufahamu hakimu anapata wapi mamlaka ya mambo yanayotokea nje ya korti yake. Kama kuna jambo linalotokea ndani ya korti yake hapo sawa. Nje ya korti? Sijui labda! Mwenye kufahamukwa hakika hakimu aliamuru nini tafadhali anijuze.
 
Jana baada kusikilizwa kesi ya Mbunge Lema.
Arusha. Wakati askari polisi saba watatoa ushahidi mahakamani katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, Mahakama imetoa onyo kwa askari Polisi na Magereza wanaowasumbua waandishi wa habari na wananchi.

Onyo hilo lilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha, Augustino Rwezile baada ya askari Magereza wakiwa na silaha kuwafukuza waandishi wa habari waliotaka kuchukua kumbukumbu za Lema kufikishwa mahakamani.

Pia, aliwaonya Polisi ambao wamekuwa wakilalamikiwa kwa kuwazuia wananchi wanapokwenda kusikiliza kesi ya mbunge huyo.

Leo Alhamisi kuanzia majira ya saa mbili asubuhi Jeshi la Polisi wamezuia wananchi pamoja na waandishi wa habari kuingia ndani eneo la mahakama kufutilia kesi ya Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema.

Jeshi la Polisi Arusha wamedharau Amri ya Hakimu Rwezile ambayo ametoa jana.

My take: Jeshi la Polisi wanatoa wapi mamlaka ya kudharau Amri ya Mahakama kupitia Hakimu Rwezile?
Mkuu kama kawaida yao itakua ni Maagizo kutoka Juu Au kati kwa Kijana M,g
 
Wanatekeleza maagizo ya kutoka ngazi ya juu,kama katiba ya nchi yenyewe inayowaweka watu madarakani na kuwalinda washishitakiwe inadharauliwa,itakuwa mahakama ambayo haina hata vyombo vya dola?.
 
Back
Top Bottom