Uchaguzi 2020 Arusha kuwa kama Calfornia ni kichekesho na mzaha mkuu

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,493
8,729
Mheshimiwa Jimbo la California sio saizi yetu kabisa, huko ni maji marefu sana.

Mheshimiwa Magufuri anataka kuifanya Arusha kuwa kama Calfornia, Marekani.

Kwa ambao hatujui ni kwamba ukitaja Calfornia basi unaitaja Marekani moja kwa moja, hili ndo Jimbo tajiri Marekani nzima labda likifuatiwa na Texas.

Calfornia ina Uchumi mkubwa kuliko nchi ya Uingereza, mwaka jana California GDP yake ilikuwa Dola 3.2 Trillion.

California umeme wanaotumia kwa siku, yaani mahitaji ni zaidi ya megawatt 50,000.

Kwa Ulaya nchi Pekee ambayo inaizidi Calfornia ni Ujerumani, ila wote wakina France, Uingereza wote wanapitwa mbali na Calfornia.

California ingekuwa ni nchi ingekuwa ni nchi ya TANO kwa Uchumi mkubwa Duniani kwa takwimu za sasa.

Calfornia inapitwa na nchi kama China, Japan, Ujerumani, India ilikuwa na GDP sawa na Calfornia mwaka jana,

Kwa Africa Ukichukua nchi zote sijui 52 GDP yao bado inapitwa na California, yaani chukua GDP ya Africa Kusini jumlisha na nchi zote na Tanzania ikiwemo bado hatuifikii Clafornia Jimbo.

Calfornia ndo kuna silcon valley huko San Francisco, huko ndo nyumbani kwa Wababe wa Dunia kwenye Techinolojia, ni kwamba Dunia inatawaliwa kutokea California Sun Francisco.

Kule ni nyumbani kwa:
Google, Facebook, Twitter, Adobe Inc., Apple, The Walt Disney Company, Ebay, HP Computer, Intel, McAfee, Mozilla Corporation, Netflix, Oracle Corporation, PayPal, Qualcomm, Samsung Group America, SanDisk, SpaceX,Tesla, Inc, Youtube, Yahoo, Visa Inc, Toshiba na kadhalika.

Hayo makampuni ni ya Techilinoia pekee,

Pia ndo nyumbani kwa Hollywood, na usisahau na kilimo ndo jimbo linalo ongoza kwa kilimo Marekani nzima.

Wanalima jumla ya hekari 24.5 Million.
 
Labda hamkumuelewa. Huenda alikua anamaanisha ataagiza nguo kubwa na viatu vikubwa zaidi vya mitumba kwa ajili ya vijana wa Chuga kuvaa
Mitumba?Kwa sasa hivi wazungu wanavaa mitumba kutoka kwetu.
Screenshot_2020-09-28-19-00-29-1.jpg
 
Utopolo mtupu, lema amefanya nini hapo zaidi ya kulemaza mafanikio ya jiji la Arusha. Watanzania tumeona kufanya mabadiliko ni sasa, lema akae bench now.
 
Huyu mzee kwa uongo yupo level nyingine aise.

Barabara ya Namanga mpaka Tengeru imejengwa njia 4 na EAC (East African Community), ila huyu mzee bila aibu anasem eti Mrisho Gambo alikua anamkera kweli mpaka akaamua kuijenga.

Mungu anamuona.
Na zaidi ya hapo, kama ilivyo kwa miradi mingine mingi tu anayojifanya kajenga yeye, mradi wa hii barabara na wenyewe JPM kakuta kimefanyika almost kila kitu ikabaki tu utekelezaji tu!
 
Mheshimiwa Jimbo la California sio saizi yetu kabisa, huko ni maji marefu sana.

Mheshimiwa Magufuri anataka kuifanya Arusha kuwa kama Calfornia, Marekani..
Mika 1000 iliyopita California ilikuwepo? Tunaambiwa binadamu wa kwanza alitokea Olduvai Gorge au sio? sasa kuna tatizo gani kwa Arusha kuwa kama California? Mnakwama wapi nyie kizazi cha watumwa?
 
Back
Top Bottom