Arusha: Kinana, Nape awageuza CCM "Toys"

Kazi mojawapo kwenye job descriptions alizopewa Kinana ambazo ni kupata viongozi kutoka CHADEMA, imeshamshinda.

Tena yeye mwenyewe Kwa kujua au kutojua, anakiri kushindwa hayo majukumu aliyopewa na maCCM wenzake.

Kwa watu wanaofuatilia ziara za Kinana mikoani akijaribu kuinasua CCM chumba cha ICU, watakuwa wamebaini aibu aliyoipata juzi huko Ngorongoro ambapo aliingizwa mkenge na wenzake.

Wakamwekea watu wawili. Akaambiwa kuwa eti ni viongozi wakubwa au vigogo huko CHADEMA. Loh! Naye kama ilivyo kawaida ya CCM akaingia kichwa kichwa na kuwapokea jukwaani eti anapokea viongozi wa CHADEMA.

Alas! Kumbe Mzee mzima na ujeshi wake amelambishwa galasa na viongozi wake.

Kumbe hao wote alioambiwa kwamba ni vigogo wa CHADEMA kumbe wako CCM kitambo hadi mmoja amegombea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na akabahatika kushinda nafasi Kwenye serikali za mitaa...

Leo pia kaharibikiwa huko Longido.

Si tu kwamba amelamba galasa tena Kwa mara nyingine, bali safari hii kampokea mtu aliyekuwa mlinzi wa ofisi akiambiwa ni kiongozi mkubwa wa CHADEMA, kigogo wa Wilaya ya Longido.

Tutoe wito kwa CCM; kwanza hiyo job description waliyompatia Kinana ya kuendelea kufanya siasa za ghiliba za kununua au kulaghai viongozi wa CHADEMA imeshamshinda.

Kama walimpatia target za ku-meet wajiandae kumwonesha njia aliyoelekezwa Mangula, Makamba na Mkama.

Katika hali ya umahututi wa kisiasa ambayo CCM imefikia, si Kikwete, Kinana wala kijana wao asiyejua hadhi ya mdomo wake, wanaweza kuinua chama hicho.

Tunashukuru ziara za Kinana zinashuhudia namna CHADEMA ilivyojikita akilini na mioyoni mwa watu. Hawakununuliwa wale. Hawajaghilibiwa. Ni Hoja za kisiasa zinazozungumzia maendeleo yao na mstakabali wa maisha yao na taifa hili.

Wakati Kinana katika kukimbizana na target alizopewa na aliyemtuma za kununua viongozi wa CHADEMA eti kama njia ya kushusha morali wa mapambano ya wanyonge dhidi ya mfumo na utawala mbovu, CHADEMA inaendelea kusimika mizizi si kwa wale wenye vyama tu, bali ikilenga constituent kubwa ya Watanzania ambao hawakuwahi kuwa CCM wala chama kingine cha siasa na sasa wanatambua kuwa SIASA si porojo (kama za CCM) bali ni maisha yao. Ndiyo maana waliweza kuthubutu kuamka usiku wa manane kwenda kujipanga kujiandikisha ili kupiga kura ya MABADILIKO uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Source: Makene.

Alafu habari za ndani kutoka ccm wanasema watu hao ambao niwababaishaji wanalipwa kati ya 50000 na 100000
 
Miccm mwaka huu itakuwa na movie nyingi sana za ajabu ajabu sasa hawa Mafisadi Mafisi ndio siku ile Kinana kazihirisha kuwa ni Mafisi baada ya kwenda mkutanoni na FISI,Nape nae mtoto wa haramu akisemacho hata hajui maskini lakini kwa sie tufahamuo MTOTO HARAMU ANAWEZA KUSEMA CHOCHOTE hana mafunzo hana kitu chochote zaidi ya kutoa mapovu
 
Ndio maana wanajeshi wetu waliuwawa kwa wingi sana vita ya kagera. tusingekuwa wengi IDD amini angejimegea mpaka mwanza.
 
Hilipendo

Jana nilimpigia simu Kamanda mmoja hapo Namanga na kutaka kujua kuhusu hilo la kigogo mmoja wa Chama amehamia ccm,kwanza alinishangaa sana kusikia kituko kama hicho,na akaniuliza nani kaniambia nikamjibu nimekuta Jf habari hii na ndipo akaniambia huyo alikuwaga mlinzi katika ofisi ya chama na akawa haudhurii kazini na akafukuzwa kitambo sana na leo eti anatangazwa kigogo???? Kha ha ha haaaaaaa,,,,,,,,,,ama kweli Juliana Shonza ataendelea kitumika kama dekio sana tu!

Hongera Tumaini Makene,hongera Hilipendo kwa kkusahihisha upotovu huu unaendezwa na huyu mtumwa mpumbavu Juliana Shonza
 
Last edited by a moderator:
Miccm mwaka huu itakuwa na movie nyingi sana za ajabu ajabu sasa hawa Mafisadi Mafisi ndio siku ile Kinana kazihirisha kuwa ni Mafisi baada ya kwenda mkutanoni na FISI,Nape nae mtoto wa haramu akisemacho hata hajui maskini lakini kwa sie tufahamuo MTOTO HARAMU ANAWEZA KUSEMA CHOCHOTE hana mafunzo hana kitu chochote zaidi ya kutoa mapovu

Kha ha haaaaaaaaaaa!!!! Mkubwa na kwambia safari hii yao ni ngumu daadekiiiiii!!!!!!!
 
Miccm mwaka huu itakuwa na movie nyingi sana za ajabu ajabu sasa hawa Mafisadi Mafisi ndio siku ile Kinana kazihirisha kuwa ni Mafisi baada ya kwenda mkutanoni na FISI,Nape nae mtoto wa haramu akisemacho hata hajui maskini lakini kwa sie tufahamuo MTOTO HARAMU ANAWEZA KUSEMA CHOCHOTE hana mafunzo hana kitu chochote zaidi ya kutoa mapovu

Kwa heahima na taadhima naomba umtake radhi Mh.Nape kwa kumuita MTOTO WA HARAMU....naamini haitakugharimu kitu kumuomba radhi,najuwa umepitiwa tu kama binadamu.
 
Hawa Makamanda wako wapi jamani hapo Arusha?
Tunapitwa na mengi mazuri yanayondelezwa na majangili huko kanda ya kaskazini

Filipo
Mzee wa Rula
PakaJimmy
sweetlandy
Mungi

Hawa member ni muhimu sana katika jukwaa hili

Hilipendo tunashukuru kwa kutujuza hili.
 
Last edited by a moderator:
Wale fisi hawana soko mahala nje ya nchi??

Kinana kubeba matofali,kusaidia kuezeka nyumba,kufyatua matofali,kufanya mashindano ya fisi,kukagua shamba la raia la karanga na kushika jembe la plau haijaondoa ukweli kuwa sera,itikadi na falsafa za ccm kwenye Elimu,kilimo,soko la bidhaa,Afya,Umeme,na maji vimefeli.hadanganyiki mtu hapa
 
Ccm imefika sehemu ya kutafuta wanachama wananunua kwa garama kubwa aibu sana
 
Kazi mojawapo kwenye job descriptions alizopewa Kinana ambazo ni kupata viongozi kutoka CHADEMA, imeshamshinda.

Tena yeye mwenyewe Kwa kujua au kutojua, anakiri kushindwa hayo majukumu aliyopewa na maCCM wenzake.

Kwa watu wanaofuatilia ziara za Kinana mikoani akijaribu kuinasua CCM chumba cha ICU, watakuwa wamebaini aibu aliyoipata juzi huko Ngorongoro ambapo aliingizwa mkenge na wenzake.

Wakamwekea watu wawili. Akaambiwa kuwa eti ni viongozi wakubwa au vigogo huko CHADEMA. Loh! Naye kama ilivyo kawaida ya CCM akaingia kichwa kichwa na kuwapokea jukwaani eti anapokea viongozi wa CHADEMA.

Alas! Kumbe Mzee mzima na ujeshi wake amelambishwa galasa na viongozi wake.

Kumbe hao wote alioambiwa kwamba ni vigogo wa CHADEMA kumbe wako CCM kitambo hadi mmoja amegombea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na akabahatika kushinda nafasi Kwenye serikali za mitaa...

Leo pia kaharibikiwa huko Longido.

Si tu kwamba amelamba galasa tena Kwa mara nyingine, bali safari hii kampokea mtu aliyekuwa mlinzi wa ofisi akiambiwa ni kiongozi mkubwa wa CHADEMA, kigogo wa Wilaya ya Longido.

Tutoe wito kwa CCM; kwanza hiyo job description waliyompatia Kinana ya kuendelea kufanya siasa za ghiliba za kununua au kulaghai viongozi wa CHADEMA imeshamshinda.

Kama walimpatia target za ku-meet wajiandae kumwonesha njia aliyoelekezwa Mangula, Makamba na Mkama.

Katika hali ya umahututi wa kisiasa ambayo CCM imefikia, si Kikwete, Kinana wala kijana wao asiyejua hadhi ya mdomo wake, wanaweza kuinua chama hicho.

Tunashukuru ziara za Kinana zinashuhudia namna CHADEMA ilivyojikita akilini na mioyoni mwa watu. Hawakununuliwa wale. Hawajaghilibiwa. Ni Hoja za kisiasa zinazozungumzia maendeleo yao na mstakabali wa maisha yao na taifa hili.

Wakati Kinana katika kukimbizana na target alizopewa na aliyemtuma za kununua viongozi wa CHADEMA eti kama njia ya kushusha morali wa mapambano ya wanyonge dhidi ya mfumo na utawala mbovu, CHADEMA inaendelea kusimika mizizi si kwa wale wenye vyama tu, bali ikilenga constituent kubwa ya Watanzania ambao hawakuwahi kuwa CCM wala chama kingine cha siasa na sasa wanatambua kuwa SIASA si porojo (kama za CCM) bali ni maisha yao. Ndiyo maana waliweza kuthubutu kuamka usiku wa manane kwenda kujipanga kujiandikisha ili kupiga kura ya MABADILIKO uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Source: Makene.

Copy kwa FaizaFox & Julian Shoza...
 
hyena.jpg
A_green_hyena_110121-230915-035009.jpg
Green_Hyena_ID_by_Korrok.jpg

Teh..teh..teh..Acha uchokozi mkuu.
 
Back
Top Bottom