Arusha: Jaribio la kumteka Katibu wa Chadema Jiji la Arusha kwenye Ofisi za Halmashauri ya Jiji hilo zashindikana

Pole kamanda,pamoja na MUNGU kukuokoa pia alikuwezesha akili kuhisi mambo yasiyo yakawaida mapema ili uhisi kitu,eg.tokatoka yahuyo mwanamke,inshara.
laa! eti mwanangu kumbe dokapewa dili lote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema ifike pahala muache kutafuta huruma kwa wananchi. Hii tabia ndio inayowafanya mshindwe kwenda Ikulu miaka yote na ijayo mkiendelea na uzushi wenu. Wananchi wanachagua maendeleo sio hadithi zenu hizo za kitoto

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi ni viongozi wangapi wa chadema wameuwawa bila wahusika kachukuliwa hatua, ukiachana hao wako jela kwa kesi fake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ni Mkenya?
Mimi sio mtoto wa town km akina nappe &co, ambao wana connection kibao, lkn wana buruzwa na mtu mmoja kutoka ktk kijiji cha call me jay. Wailipaswa waonyeshe action moja ambayo hata Huyo malaika mkuu, aachame mdomo.
 
Chedema kwa uongo bana tena uongo wa kitotooo, jipangeni bana, ashindwe kutekwa mashinji atekwe katibu kata dah!

Hata wewe ukiwa mwanasiasa mpinzani utakuwa hatarini siyo mashinji pekee. Wametekwa wengi, wamepotea wengi lakini siyo mashinji. Makinika.
 
Ushauri wangu kila siku mnalalamika mnajua wanapokaa na jamii zao mnazijua acheni kulalama fanyeni vitendo na ninyi

Katika woote walio changia humu wewe ndie umetoa Ushauri mzuri sana ,Dawa ya Moto ni Moto wataogopa na kuacha kutufanyia Raia.
 
Katika woote walio changia humu wewe ndie umetoa Ushauri mzuri sana ,Dawa ya Moto ni Moto wataogopa na kuacha kutufanyia Raia.
Kwa hiyo unashauri tuchukuwe sheria mikononi mwetu kwa kutumia kanuni ya jino kwa jino? Hapana bado hatujafika huko tuzidi kusungumza na kupaza sauti TISS ni watu wema kwa nchi hii na iko siku watawabaini wote wasioitakia nchi yetu mema kwa kuwaumiza na kuwapoteza watanzania.
 
View attachment 1030747

Siku ya Ijumaa tarehe 22/02/2019 kuanzia saa 5:41 asubuhi - 6:10 mchana nilikuwa kwenye jaribio la kutaka kutekwa kwenye Ofisi ya Afisa Uchaguzi/EO wa Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Nilipigiwa simu na Afisa Uchaguzi akiniambia kuna jambo la dharura na la umuhimimu la kutaka kuonana na mimi (Katibu wa CHADEMA Wilaya Arusha Mjini) na mimi kwa fikra/mtazamo wa kwanza nilidhani ni wito kuhusu kikao kinachohusu maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. At first sikupata hofu wala chembe ya mashaka kwa sababu Afisa Uchaguzi huyu nimeanza kumjua tokea mwaka 2014 akiwa kwenye position hiyo hiyo mpaka leo 2019.

Nilienda Halmashauri nikiwa na Diwani mmoja wa CHADEMA ambaye alinipa lift kwenye gari yake na yeye akiwa anaenda Halmashauri kwa shughuli zake na tulipofika Halmashauri tulimkuta Diwani mwingine maeneo ya reserved parking ya Mkurugenzi na Meya na tukasalimiana na Mimi nikamwambia "... Kaka nimeitwa na Afisa Uchaguzi hapo Ofisini kwake ngoja nimuone inawezekana ikawa ni mambo ya Uchaguzi ..." yule Diwani wetu wa CHADEMA akanijibu kuwa "... inawezekana maana mimi nilikuja kumuona Mkurugenzi ila nimeshindwa kumuona kwa sababu pale Ofisini kwake yupo kwenye Kikao na nimeona watu wa usalama wengi kama kuna kikao fulani hivi ..." basi Mimi nikaingia kwenye Ofisi ya Afisa Uchaguzi na nilipofika kama nikamsalimia akanikaribisha lakini alikuwa ananiuliza maswali mengi mengi mfululizo kuhusu maandalizi ya CHADEMA kwenye Uchaguzi na kunichangamkia sana (isivyo kawaida kumbuka nimewaambia huyu Mama nimeanza kushughulika naye kuanzia 2014 kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014, 2015 kwenye Zoezi la Uandikishaji wa Wapiga Kura, Uchaguzi Mkuu wa Udiwani, Ubunge na Urais 2015, Uchaguzi Mdogo wa Mbunge Arusha Mjini Dec 13,2015, Uchaguzi wa Marudio wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa katika Mitaa 8 ya Jiji la Arusha 2016, Uchaguzi Mdogo wa Marudio ya Udiwani 2017, Uchaguzi Mdogo wa Marudio ya Udiwani 2018 na Vikao vingine vingi vya Halmashauri nilivyohudhuria kama Katibu wa CHADEMA Wilaya Arusha) na last kabla hali haijachafuka aliniuliza "... Inno mwanangu huwezi kuacha Siasa, angalia wajukuu zangu (akimaanisha watoto wangu/yeye huwa ananiitaga Inno mwanagu) wasije wakashindwa kuishi, hizi Siasa hizi ...".

*Ghafla simu yake ikaita akaniambia "samahani ninaomba nipokee hii simu" akatoka nje kuongea na hiyo simu then akarudi ndani akaniambia ngoja nikuandalie Chai nikamshukuru kwa kumwambia Ahsante niko sawa, palikuwa na Karanga kwenye meza yake akaniambia kula basi hata hizi Karanga, nikaokota punje kadhaa za Karanga, akaniambia samahani nakuja (alitoka nje) baada ya muda mfupi sana alirudi ndani/Ofisini pale aliponiacha nikaona watu watatu wanakuja (nilipokuwa nimekaa nilikuwa natazamania na dirisha hivyo kila anayekuja nilikuwa ninamuona) kati ya wale watu watatu mmoja nilimtambua alikuwa ni DSO wa Wilaya Arusha (ninamfahamu kwa sabubu wakati Uchaguzi unaanza huwa kinafanyika kikao cha Briefing (Makatibu wa Vyama vya Siasa Wilaya, OCD, DSO, RO, RO1, RO2, RO3, ARO, EO na wengine).
DSO alikuwa ameambatana na watu wengine 2 lakini hao wawili kwa kwa first impression yangu, body language na body morphology zao ni MANYAMERA/TASK FORCE.

Afisa Uchaguzi akaanza kusalimiana na DSO kwa salamu zisizoisha (zenye kujirudia rudia) na baadaye akamwambia "... Mkuu karibu muendelee na kikao" huku akiwa anampisha kiti DSO akae. (DSO na yule mtu mmoja waliingia Ofisini kwa Afisa Uchaguzi then mtu mmoja kati ya wale waliokuja na DSO alikuwa amesimama mlangoni) kwa mazingira hayo unaona kabisa nilikuwa chini ya Ulinzi tayari lakini good enough wakati haya yote yanaendelea nilikuwa ninawaona Madiwani wetu wa CHADEMA wawili niliowaacha pale kwenye eneo la parking ya Mkurungenzi & Meya na hata lolote lingitokea ndani ningeweza kuwaita na wangekuja kuni rescue.

*DSO alijeuka akaangalia nje kupitia dirishani then akamwambia yule Mama Afisa Uchaguzi ngoja kwanza tukamuone Mkuu hapo juu (Kwa haraka nilielewa anataka kumuona Mkurugenzi maana Ofisi yake ndiyo ipo juu kule ambapo gesture ya mkono wa DSO ulielekeza).

Kitendo cha wale mabwana kutoka tuu pale Ofisini nilimwambia Afisa Uchaguzi ngoja nikamuone Mh ... pale nje narudi sasa hivi. Sikusubiri ruhusa nilitoka kwa haraka nikamkuta Mh Diwani pale nje nikamwambia "... Mh ... tafadhali tuingie kwenye gari na tutoke eneo hili haraka sana kuna hali mbaya hapa" basi bila kusita Mh Diwani aliwasha gari tukaondoka pale Halmashauri kwa Haraka sana na kuelekea kwenye Super Market ya yule Diwani.

Tulipofika tuu Afisa Uchaguzi alimpigia simu yule Diwani akimwambia Mkurugenzi anataka kuongea na wewe "Mkurugenzi alipoanza kuongea akaanza kumfokea Mh Diwani nani amekuruhusu uondoke hapa ninakupa dk 5 tuu uwe umerudi hapa la sivyo nitakuweka ndani na hauta toka simu ikakatwa.

Kuna maelezo mengi baada ya hiyo simu lakini let's me end here.

Ninawaomba Viongozi wenzangu na Wanachama sasa tuchukue tahadhari kubwa ya Kiusalama.

*Mimi nilikuwa nitekwe na kama Chama kingejitokeza na kusema mara ya mwisho Katibu wetu wa CHADEMA Wilaya alionekana Halmashauri alipokuwa ameeitwa na Afisa Uchaguzi, wao wangekuja na hoja ya utetezi wangesema mtu hawezi kutekwa kwenye eneo la Halmashauri mchana kweupe na Halmasahuri kuna CCTV camera.

Lakini what if Watekaji wangeniweka chini ya ulinzi pale pale kwenye Ofisi then wakaninyang'anya simu zote then nikafungiwa chooni mpaka muda wa usiku then nikatolewa nje ya eneo la Halmashauri kwenda kuteswa au kuuwawa huko pasipojulikana.

*Kwenye hili jambo kwanza kuna MUNGU kwa sababu mimi mwenyewe ninaamini hivyo then kingine kilichosaidia ni wale Madiwani wawili waliokuwepo kwenye eneo la Reserved Parking ya Mkurungenzi na Meya kwa sababu ukiwa kwenye Ofisi ya Afisa Uchaguzi unachokiona kupitia Dirisha la Ofisi yake ni hiyo reserved parking ya Mkurugenzi na Meya.*

*Simu DSO aliyompigia Diwani (aliyenitoa na gari pale Halmashauri) jioni baada ya tukio hili kutokea inadhihirisha shahiri kuwa DSO ana guilt conscious kwenye hii issue, I have to declared this public kuwa sina urafiki wala undugu na DSO zaidi nimewahi kuonana naye kwenye vikao kadhaa Mimi nikihudhuria kama Katibu wa CHADEMA Wilaya Arusha

Glory be to the Almighty GOD
Zaburi 34:19 - 22

KISANYAGE INNOCENT J
KATIBU
CHADEMA WILAYA ARUSHA
Pole sana na hongera sana. Ukiona hivyo ujue dawa inawaingia kaza mwendo kamanda wetu wa nguvu.
 
Ushauri wangu kila siku mnalalamika mnajua wanapokaa na jamii zao mnazijua acheni kulalama fanyeni vitendo na ninyi
Hili jambo siyo la kukaa kimya kwa yeyote mwenye machungu na nchi hii maana wanaotekwa siyo wapinzani peke yao, wapo wafanyabiashara, waandishi wa habari na wanaharakati mbalimbali wametekwa na kuuawa na hawa usalama wa taifa, kukaa kimya mkuu kwa sababu siyo mpinzani si sawa, hapa tupige kelele sote na ikiwezekana tuwe tunawajibu kwa vitendo kama alivyowajibu yule Zakaria wa Tarime
 
... Mh ... tafadhali tuingie kwenye gari na tutoke eneo hili haraka sana kuna hali mbaya hapa" basi bila kusita Mh Diwani aliwasha gari tukaondoka pale Halmashauri kwa Haraka sana na kuelekea kwenye Super Market ya yule Diwani.

Tulipofika tuu Afisa Uchaguzi alimpigia simu yule Diwani akimwambia Mkurugenzi anataka kuongea na wewe "Mkurugenzi alipoanza kuongea akaanza kumfokea Mh Diwani nani amekuruhusu uondoke hapa ninakupa dk 5 tuu uwe umerudi hapa la sivyo nitakuweka ndani na hauta toka simu ikakatwa.
......
....
*Simu DSO aliyompigia Diwani (aliyenitoa na gari pale Halmashauri) jioni baada ya tukio hili kutokea inadhihirisha shahiri kuwa DSO ana guilt conscious kwenye hii issue, I have to declared this public kuwa sina urafiki wala undugu na DSO zaidi nimewahi kuonana naye kwenye vikao kadhaa Mimi nikihudhuria kama Katibu wa CHADEMA Wilaya Arusha
Wewe jamaa liongo, hii habari imetungwa ili kujaribu kutafuta huruma. Cheki habpo bold, ulisema afisa wa uchaguzi alimpigia diwani simu, then DSO alimpigia simu huyo diwani, inamaana ktk kutunga uongo wako umekosa consistency. Ulitakiwa uandike hivi, ile simu ya afisa uchaguzi inadhihirisha blabla kwenye hapo SIMU ya DSO. Au basi ungedanganya kwa kuanza kusema DSO alimpigia simu Diwani blahblah.

Wapinzani mumekuwa waongo hamuaminiki kabisa, sijui lengo lenu ni nini, ila majibu mtayapata maana Allah yupo na Tanzania
 
Yaani umeanza tu na kusema UWONGO... !!!! Huna hata suhahidi wa unachokisema... Binafsi wewe na huyu aliyetaka kutekwa mnalo la kusema zaidi ya haya....

Kwa aliyenusurika kutekwa
1. Kuwepo na/atoe ushahidi wa wazi sisi ambao hatukuwa katika eneo la tukio tuondolewe doubt
2. Waliomuokoa waseme kuwa kilichosemwa na mnusurika ni kweli
3. Kama wana recorded voice note waiweke hadharini kujua simu zilizopigwa za kuitana kwenye ofisi na vitisho vya kuwekana ndani
4. Kama kuna CCTV basi clips ziwe hadharani... HILI NAJUA YA KWA LISU YATATAMALAKI KAMA KWELI ZIPO

Kwa wewe unayesema huyu mnusurika ni muongo
1. Weka ukweli wako na useme kwa muda anaosema amenusurika, USEME ALIKUWA WAPI
2. KAMA UNA VIDEO INAYOMUONYESHA KUWA MUDA HUO HALUWA KATIKA OFISI ZA HALMASHAURI BASI WEKA
3. Au kama wewe una ushahidi wa waliotajwa kutokuwepo eneo la halmashauri wakati hili likitenedeka , weka tuoone uwongo wa huyo mnusurika

KUSEMA TU JAMAA NI MUONGO, HUKU HUWEZKI CHOCHOTE KUSAPOTI UNACHOKISEMA, kwa wenye akili wataona tu wewe ndo muongo na unaendeshwa na ITIKADI na UCHAMA
.
 
Siku ya Ijumaa tarehe 22/02/2019 kuanzia saa 5:41 asubuhi - 6:10 mchana nilikuwa kwenye jaribio la kutaka kutekwa kwenye Ofisi ya Afisa Uchaguzi/EO wa Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Chadema uongo mwingine hauna mashiko
Yaani mtu atake kukuteka akiwa kwenye ofisi ya umma yenye pilika pilika siku nzima?
Kwanza utekwe una impact gani kwa siasa zaArusha?
Itafikia wakati mtasema mlitaka kutekwa mkiwa vyumbani na wake zenu
 
Back
Top Bottom