KERO Arusha ina mpangilio wa ovyo katika usafiri wa umma

KERO Arusha ina mpangilio wa ovyo katika usafiri wa umma

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Joined
Jan 2, 2019
Posts
69
Reaction score
79
HAKUNA JIJI LENYE MPANGILIO WA HOVYO KATIKA USAFIRI KAMA ARUSHA..

Kiukweli inashangaza sana kuona jiji kama Arusha linazidiwa na Mikoa ambayo haina hadhi kama ilivyo Arusha kuwa na mpangilio unaoeleweka katika suala zima la Usafirishaji wa Raia.

Magari mengi yanaenda shakalabaghala (hayana ruti maalumu) Unakuta gari imeandikwa Ngaramtoni--Intel lakini inapiga Ruti za Kilombero-Tengeru au Stendi Ndogo-Njiro yani ilimradi tu magari yanatembea na Abiria wanafikishwa sehemu wnazoenda.

Hii inachanganya sana abiria hasa wageni wanaokuja Arusha, Maana wanakotoka kama gari imeandikwa Kisongo-Mapambazuko inaenda ruti ilivyo na sivyo kama ilivyo kwa hapa Arusha...Nilazima tubadilike hata kwa shuruti...

TUNAIOMBA MAMLKA YA USAFIRISHAJI HAPA ARUSHA PAMOJA NA WAMILIKI WAANGALIE JAMBO HILI...
 
Kwanza waachane na vifodi/vihaisi, wanunue coaster,rosa na magari mengine ya kistaarabu kama dar gari ni kubwa hata za kongowe, kiluvya, mbagala, gongo la mboto, tegeta gari ni kubwa sio kama arusha bado wanatumia vipanya kusafirisha abiria. Eti ukiwa unaenda Moshi ndio unapanda coaster/rosa
 
Hilo sio tatizo hata mwanza mbona ipo hivyo... Muhimu ni kuwa na ustaarabu kama ilivyo huko Daslamu
 
Vipi hiko pia kuna kugombania daladala kama huku mzizima
Hilo kuwepo ni ngumu kutokana na dala dala kutokuwa na ruti maalumu Unakuta jioni dala dala zinakimbilia upande mmoja yaani zinapokezana na bajaji😂😂😂shida tupu sehemu ya nauli 600 utafika kwa 1500
 
Back
Top Bottom