Arusha imelemewa na Wazungu Volunteers, Why Arusha Pekee?

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
2,712
6,507
Arusha inaelekea kulemewa na volunteers kutoka Ulaya huko na Marekani, sina shida na wao ku volunteer, ila ninachouliza kwanini ni Arusha pekeee?

Nchi hii ina amani kote kule, kwanini Volunteer iwe ni Arusha pekee yake na sio Kigoma wala Kagera wala Singida wala Shinyanga wala Tabora wala Katavi au Mbeya au Mtwara na Lindi huko.

Kuna sehemu nilifika nikakuta kuna Volunteers wako 60 eti wanadili na kusaidia mbwa wa mitaani. Hospitali za Arusha hasa hizi za Serikali zima Wazungu volunteers huku Watanzania waliohitimu wao wakiambiwa nafasi za kujitolea hazipo.

Uhamiaji kama hakuna dili wanafanya wanapaswa hawa volunteers kuambiwa kuvolunteer sio Arusha pekee yake bali ni nchi nzima.

Hawa Wazungu ni wajanja wajanja sana, na uhamiaji ni kama kuna mshiko wanapewa na hawa Wazungu.

Nchi ina mikoa 25+ haiwezekani mkoa mmoja tu ndio uwe wa volunteers wote. Pia serikali inapaswa kuingilia kati na kuhakikisha kama ni kujitolea iwe ni nchi nzima na sio mkoa mmoja tu tena wilaya moja au mbili tu.
 
Angalia how much wana contribute kwenye business visa ya $250/person ndo ujue kwamba hakuna namna, watakuja na watakaa wanapotaka. Unataka waende Tandahimba?
 
Wanavolunta hasa kwenye shule yao, alafu wanaajiliwa kwenye mashule ya international na wakijtolea Kuna kitu wanapewa kiasi tu.
 
Wenye mijengo ya maana wanafaidi kupitia Kampuni ya Airbnb home stay.
 
Arusha inaelekea kulemewa na volunteers kutoka Ulaya huko na Marekani, sina shida na wao ku volunteer, ila ninachouliza kwanini ni Arusha pekeee?

Nchi hii ina amani kote kule, kwanini Volunteer iwe ni Arusha pekee yake na sio Kigoma wala Kagera wala Singida wala Shinyanga wala Tabora wala Katavi au Mbeya au Mtwara na Lindi huko.

Kuna sehemu nilifika nikakuta kuna Volunteers wako 60 eti wanadili na kusaidia mbwa wa mitaani. Hospitali za Arusha hasa hizi za Serikali zima Wazungu volunteers huku Watanzania waliohitimu wao wakiambiwa nafasi za kujitolea hazipo.

Uhamiaji kama hakuna dili wanafanya wanapaswa hawa volunteers kuambiwa kuvolunteer sio Arusha pekee yake bali ni nchi nzima.

Hawa Wazungu ni wajanja wajanja sana, na uhamiaji ni kama kuna mshiko wanapewa na hawa Wazungu.

Nchi ina mikoa 25+ haiwezekani mkoa mmoja tu ndio uwe wa volunteers wote. Pia serikali inapaswa kuingilia kati na kuhakikisha kama ni kujitolea iwe ni nchi nzima na sio mkoa mmoja tu tena wilaya moja au mbili tu.
Hawana lolote,hao wamekuja kutalii, angalia Vituo vya Watoto Yatima vipo vingi ...Kilimanjaro,Meru,Arusha ...then vinafuata Barabara ya Singida ,ukifika Makayuni vinapinda kuelekea Mto wa Mbu hadi Karatu!
 
Inatakiwa uelewe wazungu hawatoi Rushwa hawakulelewa mazingira hayo.
Watu ufuata taratibu
 
Wakati Natoma Lushoto Kuna Kundi la mbu lilikuwa linapita kama limetumwa lkn wakawa wanapotea .tukawa tunajisemea kuwa wazungu wanatuzalishia mbu .
 
Hao volunteer wanakuja hapo hawalipwi, au wanalipwa na mashirika yao huko walikotoka,
Utaona kuwa hatuna cha kuwapangia sana, wao wanakuja kwa kazi tu, ila sasa serikali isolve issue kwa kutoa ajira nyingi mikoan
Kwa hio huko wanaelekezwa waende Arusha sio? Kwa nini sio Singida au Dodoma?
 
Back
Top Bottom