Arusha imebadilika kabisa

Arusha imebadilika kabisa

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
10,416
Reaction score
18,443
Wakuu Amani iwe nanyi., Peace and love 😍 wana jf.

Jambo ambalo nataka kusema ni kuwa Arusha imebadilika kwa kiasi kikubwa sana tangu hili gonjwa liingie yaani ni balaa.

Arusha ni mji uliojaa wazungu kila Kona utafikiri tupo South Africa 🌍 na tushazoea kufanya biashara au mazungumzo ya hapa na pale na hawa wadoshi wakiwa hapa jijini.

Na wazungu wengi wao wamewekeza sana hapa. Asilimia kubwa sana ya wana Arusha pato Lao kubwa achia mbali madini la pili ni utalii.

Lakini kwa sasa hali ni tofauti kabisa urafikiri tupo singida au wap sijui hatuoni wazungu kabisa kabisa hata Ile migahawa wazungu hukaa hamna mtu mweupe hata kidogo.

Hotel, migahawa, na kule vinyagago na sehemu zote wazungu wanapopendelea kutembea au kukaa hamna kabisa watu weupe.

Makampuni mengi, migahawa, maduka na hata masoko wengi tunategemea utalii, sahiv kila mtu analia.

Watu weusi tunalia Arusha kwa kweli sijui kwa mikoa mingine mimi ila hapa chuga tunalia 😭😭😭
 
Mi ni mzawa wa Arusha ila kwa sasa nko dsm amna penye afadhali hata hii dsm yenyew jam za kipumbavu amna... Watu wanakaa level seat na bado life linaenda.

Yakija magonjwa mengine kama haya ma3 nafkir dunia itakaa kwa kunyooka maana watu walishaona pesa ndo kila kitu sasa hapa tunapambana mwenye pesa na mwenye kinga ya mwili.

Via/ A-Town my home town
 
Mi ni mzawa wa Arusha ila kwa sasa nko dsm amna penye afadhali hata hii dsm yenyew jam za kipumbavu amna... Watu wanakaa level seat na bado life linaenda.

Yakija magonjwa mengine kama haya ma3 nafkir dunia itakaa kwa kunyooka maana watu walishaona pesa ndo kila kitu sasa hapa tunapambana mwenye pesa na mwenye kinga ya mwili.

Via/ A-Town my home town
Mkuu sahiv wana chuga wale wa kisoro Soro hamna tena, kila mtu ameweka adabu mfukoni.
 
Arusha inaathirika sana kwa ajili ya utalii kuporomoka
Hali ni mbaya duniani kote hakuna mwenye ahueni
Hili janga ni vita haswa na uchumi umeanguka kila mahali
Matajiri wamepigika sana na wa hali ya chini wanaumia pia kwani tunategemeana



Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Back
Top Bottom