Chanzo ni NiNII?
Mimi nitasema chanzo ni Siasa za Chama Cha Majambazi.
Why?
Mambo mengi hapa nchini kwa sasa yanafanywa au yanaamuliwa kisiasa zaidi.
Suala la Dr. Ulimboka, madaktari walikuwa wanadai vitu vya msingi kabisa kwa faida ya nchi badala yake Dr. Ulimboka amekuja kudhurika na serikali mpaka leo haiwajui hawa watu waliomdhuru Dr. Ulimboka.
Same to Mwangosi, Kibanda wahusika hawajulikani.
Udini: kwenye hili suala la Arusha mimi sioni kama ni geni labda kwa sababu ni jipya ktk mkoa wa Arusha lkn tujiulize kabla ya hili la Arusha ni matukio mangapi yametokea yakiwamo ya mchungaji, padri kuuawa, makanisa kuchomwa, watu kugombea kuchinja lkn serikali iliyopo madarakani haijui na wala haitaki kujua nini chanzo, haikemei wala haitaki kukemea, haifanyi chochote kile.
CD, DvD, vipeperushi, mihadhara, makongamano, misikiti ya kujifunzia Ugaidi vyote hivi vinakashifu dini fulani lkn serikali inayotakiwa kusimamia haya yote inaona na ipo ila haijishughulishi na hawa wanaovunja sheria za nchi, ipo imekaa kimya.
Hapa kinachotokea ni watawala wamefika mwisho wa kuongoza na hawataki kuachia madaraka sasa wanatugawa kwa kutuchonganisha kidini ili sisi wananchi tuendelee kutandikana wao waendelee na maisha yao ya kutafuna nchi.
Lkn wanashindwa kuelewa kwamba wanachokipanga hakiwi kama wanavyotegemea.
Haya mauwaji, mateso, vimbwanga vyote hivi ni serikali inafanya kutugonganisha vichwa, haiwezekani uniambie padri auwawe tena bunduki asubuhi kweupe muhusika ashindwe kukamatwa eti mpaka FBI waje kuchora kikaragosi.
Kama hata kujilinda sisi kwa sisi hatuwezi basi tumpe nchi Mmarekani sisi tubakie kuwa manamba kwenye mashamba na viwanda vyao hapa Tz.