Arumeru-siasa zetu na hatma ya tanzania. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Arumeru-siasa zetu na hatma ya tanzania.

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Ringo Edmund, Mar 31, 2012.

 1. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu watanzania,nimejaribu kutafakari sana siasa zetu miaka hii na hatma ya nchi yetu.
  Ukiuangalia uchaguzi wa igunga na ukija uchaguzi wa arumeru mashariki utagundua kuwa safari yetu kama taifa si salama.
  Wanaoitwa waheshimiwa si waheshimiwa tena,matusi kwenye kampeni imekuwa jadi,kutishia kuua kwa silaha au kwa ngumi si kosa tena,kumwagiwa tindikali si kosa tena ni siasa,kutumia magari ya serikali au kutumia cheo cha uwaziri sikosa.

  Lipo wapi daraja la mbutu aliloahidi waziri wa ujenzi pale igunga?
  Ipo wapi ile misaada ya mahindi pale igunga?
  Mbona kampeni zimeisha lema hajauwawa na wazee wa kishiri wakati hajaomba msamaha na kampeni alipiga?
  Upo wapi uheshimiwa wa mkapa?
  Upo wapi uheshimiwa wa lusinde?
  Ni lini mali ya serikali itaachwa kutumika vibaya?
  Yapo wapi magazeti na redio za serikali kwa ajili ya watanzania wote?
  Wapo wapi polisi wakutokeza hadharani na kutuambia kesi ya musa tesha kumwagiwa tindikali pale igunga inaendeleaje mahakamani?
  Ipo wapi takukuru ilyosema uchaguzi wa ndani wa chama kimoja ulitawaliwa na rushwa?

  Tutachekelea leo lakini kesho tutalia.
  Rais akishachaguliwa ni wa watanzania wote,waziri akishateuliwa anatumikia watz wote kwani wao ndio wanaomlipa mshahara.

  Rais mstaafu analipwa pensheni na kodi za watanzania wote.
  Mungu atupe uhai tushuhudie mwisho wa haya kwani kwa utabiri wangu mdogo wa kuweza kutabiri kuwa usiku kutakuwa na giza natabiri ya kuwa mwisho wa yote umefika.

  KAMA SERIKALI YOTE INAINGIA KWENYE UCHAGUZI MDOGO WAKATI MIAKA 10 ILIYOPITA HAKUKU NA KITU KAMA HICHO TUTARAJIE NINI BAADA YA MIAKA 10 MBELE?
  SI KWAMBA UCHAGUZI WA KIJIJI KAMPENI ZAKE ZITAZINDULIWA NA RAIS MSTAAFU NA MAWAZIRI KUSHIRIKI?
   
 2. Chali wa Moshi

  Chali wa Moshi JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 258
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  daraja siwamesema linaanza after two weeks from now, nawame join venture wakandarasi 12 wazawa.
   
Loading...