Arumeru Mashariki: JOSHUA NASSARI vs SIYOI SUMARI

kuingia uwanjani ukiwa umejiamini ni dalili ya ushindi na hata watu hufikia kusema umekwishashinda nusu ya vita yako japo ukweli unabaki ni jinsi gani utakavyoweza kuyakabili mabonde, milima, visiki, miiba na mbigili za uwanjani ndo ushindi wako ukamilike.

Kazi ndo kwanza inaanza tuake kuutafuta ushindi tuache maongezi pasina vitendo
 
Siasa siku zote ni mchezo msafi sana tu isipokua baadhi ya wachezaji wake ndio hutokea kuwa ni wachafu. Tafakari hilo.

Lowassa anaongoza kwa kucheza rafu nyingi uwanjani, na zinamsaidia sana safu zake
 
​OK he passed CCM - CC how about TAKUHURU?

Iwe umekosea au ulidhamiria - Ingekuwa TAKU-HURU kama ulivyoandika tungeona mambo ila hii mkuu ni TAKUKURU na inashabikia IKULU. Kama ikulu itasema ni mla rushwa basi atawekewa zengwe kama tulivyoona kwenye uchaguzi wa 2010, lakini ikulu ikisema ni safi, basi ni safi na Takukuru hawana cha kusema zaidi ya kumsafisha kama walivyomsafisha Chenge na pesa za rada.
 
Mkuu Pasco,

Kwenye kundi la wapayukaji wewe huwa haumo siku zote. Imekua vipi leo mwenzetu uone giza tupu hivi kuhusiana na uchaguzi kule AruMeru Mashariki au ndio kugangamala kule ndio kusema?

Feedback, nipo nimejinyamazia kimya!. Ila pia nimegundua ni wanabodi wachache sana huwa wanaukubali ukweli halisi!, wengi zaidi huogopa ukweli halisi na badala yake kung'ang'ania ukweli wa kujifariji nafsi zao kwa kujipa matumaini ya uwongo na mwisho wa siku huishia kulia lia tuu!.

Baada ya kupitishwa Sioi, uchaguzi Arumeru ndio umemalizika!. Kinachoendelea sasa ni kwa NEC kukamilisha tuu taratibu kukidhi matakwa ya kidemokrasia kusubiria kumtangaza rasmi!.

Wenye akili wataisoma hii post na kujinyamazia kusubiria April 2!. Ving'ang'anizi wa maubishi mtaanza kubisha na kuendelea kujifariji kuwa mtu yule yule toka chama kile kile aliyeshindwa na mahututi kitandani, sasa anaweza kushindana na mwana mfalme wa mtu yule yule aliyewashinda mwanzo na akashinda!.

Wengi wanategemea zaidi kura za chuki za wana CCM dhidi ya siasa za uchifu, usultani na ufalme za CCM kwa mtoto kumrithi baba yake bila kutambua asili ya Wameru ni ufalme wa koo fulani fulani!. Jerry alikuwa ni mfalme wao na Sioi ndiye mwana mfalume!.
Kwa wapenzi wa demokrasia ya kweli mtanisamehe sana kwa kuwadondolea ukweli mchungu!. Ili kuupata ukombozi wa kweli, lazima tukubali kukimeza "the bitter pill"- Sioi ndiye Mbunge Mteule wa Arumeru akisubiri kuapishwa!.

Pasco (wa jf).
 
Kwa wapenzi wa demokrasia ya kweli mtanisamehe sana kwa kuwadondolea ukweli mchungu!. Ili kuupata ukombozi wa kweli, lazima tukubali kukimeza "the bitter pill"- Sioi ndiye Mbunge Mteule wa Arumeru akisubiri kuapishwa!. Pasco (wa jf).

Wewe Pasco bado upo nao hadi sasa? wanakupa nini hao? hamna cha kukubali hapo, labda wewe ndo umeshakubali ila Nassari ndo mbunge mteule wa Arumeru Mashariki!!!..
 
Angepita Sarakikya,kazi ingekuwa ngumu sana kwa CHADEMA maana jamaa kule anajulikana sana,na miaka yote amekuwa anakubalika sema nguvu ya pesa ndio imekuwa ikimsambaratisha......huyu Siyoi watu hawamjui kabisa na wala haijui Arumeru ,CDM Arumeru itakuwa kama kumsukuta mlevi kiwete kwenye ngazi......90% ushindi..
 
Wewe Pasco bado upo nao hadi sasa? wanakupa nini hao? hamna cha kukubali hapo, labda wewe ndo umeshakubali ila Nassari ndo mbunge mteule wa Arumeru Mashariki!!!..
Dada na Rafiki BJ, kumbe na wewe umo?!. Samahani kwa ukweli huo mchungu, ila iweke hii kwenye kumbukumbu ili tukumbushane tena ifikapo tarehe 2 Aprili wakati tukifanya mrejesho!.
 
Mkuu Pasco,

Kwenye kundi la wapayukaji wewe huwa haumo siku zote. Imekua vipi leo mwenzetu uone giza tupu hivi kuhusiana na uchaguzi kule AruMeru Mashariki au ndio kugangamala kule ndio kusema?
Mkuu uwezo tunao, hii ni sauti iliyo nyikani, ukiisikia kwa karibu utaiona ni kelele!. Uzuri wa sauti ya nyikani haishi au kupotea bali huendelea kuvuma mpaka litakapo timia lengo la sauti hiyo!. Leo uione ni upayukaji au kelele, tarehe 2 Aprili ndio utanielewa!.
 
Wameru wataonyesha mfano wa kudhihirishia umma kuwa wao wamechoka na CCM.

Tunachofanya ni kwenda kuwakumbusha wananchi kuwa muda wa mabadiliko ni sasa,kwa kuwa wameru ni waelewa na hawaongozwi kwa nguvu ya hela,na ni watu wanaotambulika kwa msimamo wao nadhani hili ndilo jambo la kujivunia kwa Chama changu cha CDM.

Tunakwenda kuzilinda kura kwa gharama yoyote.wananchi wameshudia jinsi CCM Walivyomstari wa mbele kutetea chama chao bungeni na kuwatupa wananchi.

Sasa ndio muda wa kuweka wazi hasira zetu na kupinga hujuma zote za CCM na kusimika matumaini ya ushindi ndani ya Arumeru pamoja na wana-arumeru kwa kuichagua CDM.

CCM IMEFIA ARUMERU,MAPAMBANO YANAENDELEA.
 
Mungu hapendi mtu kuonewa na kusingiziwa sana kiasi hiki, kwani atakuwa upande wake, na ndiyo maana Mungu anaendelea kumwangazia njia EL.

Linapokuja swala la huyu bwana nashindwa kujua watz wanamatatizo gani.

Tujiulize je EL ni mchungaji? Ni padri?
Mbona amekuwa yupo karibu sana na makanisa?

Usafi unaotafutwa makanisani si usafi wenye safi ndani yake.
 
Baada ya vyama hivi vikubwa kupitisha majina ya wagombea wao, macho na masikio ya wananchi yapo kati ya wagombea wawili kutoka CCM na CHADEMA.
Joshua Nassari na Siyoi Summari.

Pamoja na kuwa kulikuwa na pingamizi kwa jina la Siyoi Summari kutokutaka kupitishwa na CC ya CCM kutokana na tuhuma za Rushwa zilizokuwa zinamkabili, sasa imedhihirika kwamba kumbe Mkono wa aliyekuwa anatuhumiwa kutoa rushwa kwenye kura za maoni (EL) ndiye mmiliki na ana mkono mrefu unaoweza hata kufikia CC ya CCM.

Siasa ya Tanzania jama!

EL anaandamwa sana hii ni kampeni maalumu ambayo haina ushaidi akiwemo six etc kama anatuhuma hizo zote achukuliwe atua za kisheria
 
EL anaandamwa sana hii ni kampeni maalumu ambayo haina ushaidi akiwemo six etc kama anatuhuma hizo zote achukuliwe atua za kisheria

Hebu tuwe serious kidogo. Unaposema kuwa EL anaandamwa sana na akina Six, unataka kutuambia hata ile sms aliyokuwa akitumiana EL na Katibu wa UVCCM Monduli kwenda kuchukua hela kwa Askofu ili kufanikisha kuwawezesha wajumbe kumchagua Siyoi ina mkono wa Six? Ukweli utabaki kuwa ushindi wa Siyoi ni ushindi wa kambi ya Lowassa dhidi ya CCM ya akina Jk na Nape
 
Mkuu najua kwenye huu uchaguzi wewe utakuwa Neutral,Manake kwako wewe EL Unampenda na CDM Unaipenda,very wonderful Mix

Mnyisanzu ni chadema mwenye mapenzi makubwa na Lowassa! Kifupi anatamani kama Lowassa angegombea urais kwa tileti ya chadema duh!
 
quote_icon.png
By Pasco

Kwa wapenzi wa demokrasia ya kweli mtanisamehe sana kwa kuwadondolea ukweli mchungu!. Ili kuupata ukombozi wa kweli, lazima tukubali kukimeza "the bitter pill"- Sioi ndiye Mbunge Mteule wa Arumeru akisubiri kuapishwa!. Pasco (wa jf).

hapo kwenye Red. Pasco naona umekurupuka. wapenzi wa demokrasia ni nani na Shabiki wa demokrasia utamwitaje?
from the best of my knowledge, nimegundua wewe ni shabiki wa demokrasia, na hiyo msg inakufaa!
 
Back
Top Bottom