Arumeru Mashariki: JOSHUA NASSARI vs SIYOI SUMARI

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,975
9,566
Baada ya vyama hivi vikubwa kupitisha majina ya wagombea wao, macho na masikio ya wananchi yapo kati ya wagombea wawili kutoka CCM na CHADEMA.
Joshua Nassari na Siyoi Summari.

Pamoja na kuwa kulikuwa na pingamizi kwa jina la Siyoi Summari kutokutaka kupitishwa na CC ya CCM kutokana na tuhuma za Rushwa zilizokuwa zinamkabili, sasa imedhihirika kwamba kumbe Mkono wa aliyekuwa anatuhumiwa kutoa rushwa kwenye kura za maoni (EL) ndiye mmiliki na ana mkono mrefu unaoweza hata kufikia CC ya CCM.

Siasa ya Tanzania jama!
 
Hivi Sherehe ya kupitishwa kwa jina la Siyoi inafanyikia wapi?
 
Kwa hapo kura ni kuchagua kati ya Uadilifu na uongozi uliotukuka kwa upande mmoja au ushoga na urithi wa uongozi wa mambo ya kibunge ki-ukoo kwa upande mwingine. Vijana wenzetu sasa tuingieni msituni rasmi kazi ianze mpaka kieleweke!!!

BAWACHA tungependa kuona cheche zenu zaidi na zaidi kama ambavyo wafanyavyo BAVICHA kila mahali penye uchaguzi; sote tucheze kama timu moja ili kuwarahisishia kazi uongozi wa juu kuleta ufanisi Arumeru Mashariki.
 
Bado sina hakika kama wameru wanahongeka kirahisi, nikiamini pia kwamba CHADEMA walisaidia sana Siyoi kushinda kwenye kura ya maoni.
 
Baada ya vyama hivi vikubwa kupitisha majina ya wagombea wao, macho na masikio ya wananchi yapo kati ya wagombea wawili kutoka CCM na CHADEMA.
Joshua Nassari na Siyoi Summari.

Pamoja na kuwa kulikuwa na pingamizi kwa jina la Siyoi Summari kutokutaka kupitishwa na CC ya CCM kutokana na tuhuma za Rushwa zilizokuwa zinamkabili, sasa imedhihirika kwamba kumbe Mkono wa aliyekuwa anatuhumiwa kutoa rushwa kwenye kura za maoni (EL) ndiye mmiliki na ana mkono mrefu unaoweza hata kufikia CC ya CCM.

Siasa ya Tanzania jama!
naomba kujua wadau wamezidiana kwa kura ngapi....nassar amepata ngapi kati ya ngapi na sumarry amepata ngapi kati ya ngapi?
 
Kwenye kura za maoni za vyama vyao, Siyoi alimshinda mwenzake kwa asilimia 67 kati ya 100, na Nassari aliwashinda wenzake watano kwa 90.8% kati ya 100%

sasa tunasubiri uchaguzi wenyewe
 
Kama sheikh Yahaya angekuwa yupo angepiga ramli yake na kumbashiria ushindi bwana Nassari. Lakini si neno ngoja tumsaidie kazi. J.o.s.h.u.a = herufi 6 na S.i.y.o.i = herufi 5 kwa wingi wa herufi Joshua anashinda. Tuje kwenye majina ya mwisho. N.a.s.s.a.r.i = herufi 7 na S.u.m.m.a.r.i = herufi 7 hapa kwa wingi wa herufi maizani iko sawa sawa ni sare. Ili kupata mshindi kwa majina ya mwisho kwa herufi ziko sawa basi tuangalie herugi ipi ya kwanza imeanza kuliona jua kati majina haya ya mwisho?. Nassari ni N na kws Summari ni S. Unaona, N na S kutoka herufi N ya Nassari na herufi S ya Summari kuna herufi saba katikati. Hivo ni kuonesha kuwa Nassari anamzidi Summari kwa mizungu saba. Ushindi kwa Nassari.
Kama ukija kwa majina yao tuone, Joshua ameanza na herufi J na Sioi ameanza na herufi S. Kutoka J mpaka S kuna mizungu nane katikati.Joshua anamzidi Summari kwa hiyo mizungu nane, atashinda kwa jumla ya mizungu nane kwenye majina yao ya kwanza na atashinda kwa mizungu saba kwa majina ya mwisho.
Ili BWANA Siyoi aipiku mizungu hii nini kifanyike?. Ngojeni ntawaelez baadaye.
 
Pasco uko wapi kwa hili?....
Feedback, nipo nimejinyamazia kimya!. Ila pia nimegundua ni wanabodi wachache sana huwa wanaukubali ukweli halisi!, wengi zaidi huogopa ukweli halisi na badala yake kung'ang'ania ukweli wa kujifariji nafsi zao kwa kujipa matumaini ya uwongo na mwisho wa siku huishia kulia lia tuu!.

Baada ya kupitishwa Sioi, uchaguzi Arumeru ndio umemalizika!. Kinachoendelea sasa ni kwa NEC kukamilisha tuu taratibu kukidhi matakwa ya kidemokrasia kusubiria kumtangaza rasmi!.

Wenye akili wataisoma hii post na kujinyamazia kusubiria April 2!. Ving'ang'anizi wa maubishi mtaanza kubisha na kuendelea kujifariji kuwa mtu yule yule toka chama kile kile aliyeshindwa na mahututi kitandani, sasa anaweza kushindana na mwana mfalme wa mtu yule yule aliyewashinda mwanzo na akashinda!.

Wengi wanategemea zaidi kura za chuki za wana CCM dhidi ya siasa za uchifu, usultani na ufalme za CCM kwa mtoto kumrithi baba yake bila kutambua asili ya Wameru ni ufalme wa koo fulani fulani!. Jerry alikuwa ni mfalme wao na Sioi ndiye mwana mfalume!.
Kwa wapenzi wa demokrasia ya kweli mtanisamehe sana kwa kuwadondolea ukweli mchungu!. Ili kuupata ukombozi wa kweli, lazima tukubali kukimeza "the bitter pill"- Sioi ndiye Mbunge Mteule wa Arumeru akisubiri kuapishwa!.

Pasco (wa jf).
 
Umeshatia Nuksi Mkuu Pasco, naomba sana haya maneno yako yaishie humu Jf, yasiwafikie waungwana kule Meru
 
Back
Top Bottom