Arumeru kunazidi kupamba moto! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Arumeru kunazidi kupamba moto!

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by OSOKONI, Feb 16, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  MBIO za Uchaguzi Mdogo wa Arumeru Mashariki, zimeendelea kushika kasi baada ya makada zaidi wa CCM akiwamo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa Arusha, Elishilia Kaaya, kuchukua fomu kuomba kuteuliwa na chama hicho kuwania nafasi hiyo.

  Licha ya Kaaya ambaye ni mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), kada mwingine wa CCM waliochukua fomu hizo jana ni Rais wa Mtandao wa Maendeleo ya Vijana nchini (YDN), Elipokea Urio na Elirehema Kaaya, ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi Wilaya ya Nyamagana, mkoani Mwanza.

  Wagombea hao walikabidhiwa fomu na Katibu wa CCM Wilaya ya Arumeru, Edson Lihweuli.
  Wakati CCM wakijitokeza kuchukua fomu hizo, pia wanachama wa Chadema amabo ni Joshua Nassari, Samwel Shami, Francis Tembo na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Arumeru (Bawacha), Anna Mwagirwa, wanafanya idadi ya watu saba kujitokeza kuwania kiti hicho.

  Akitangaza uamuzi huo jana, Urio alisema anataraji kuchukua fomu Jumamosi wiki hii kwa lengo la kuomba ridhaa ya chama chake kuipeperusha bendera katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika siku chache zijazo.
  Wakati vyama CCM na Chadema vikiendelea kupiga mbizi, Chama cha NCCR- Mageuzi hakijafanya uamuzi iwapo kishiriki au la.

  Katibu mkuu wa chama hicho, Samwel Ruhuza, alisema wametuma ujumbe maalumu kwenda jimboni humo kufanya utafiti wa awali kujua kama kinaweza kumsimamisha mgombea.
  “Sisi tumetuma task force (kikosi kazi) Siku zote tungependa ushirikiano na wenzetu, lakini yote hayo katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki yanategemea ripoti itakayoletwa na timu ya wataalamu wetu walioko katika jimbo hilo kwa sasa,” alisema Ruhuza.

  Alisema kazi inayofanywa na tume hiyo maalamu ya NCCR-Mageuzi, ni kufanya utafiti kujua kiwango cha kukubalika kwa chama hicho na kuona mtandao wa vyama vingine kikiwamo CCM na nafasi ya ushindi kwa upinzani.
  “Tunaangalia vitu vingi katika hili,mtandao wa chama chetu, vyote vya siasa kiwango cha kukubalika kwa wagombea wao na wetu na nafasi ya ushindi kwa upinzani, hatua hiyo ndiyo itakayotufanya tuamue kusimamisha mgombea au kuunga mkono chama cha upinzani,”alisema Ruhuza.

  Kuhusu ushirikiano na Chadema, Ruhuza alifafanua kuwa utategemea ripoti hiyo inayotarajia kukamilika wakati wowote na kutolewa kwa umma.

  “Kwa sasa ni mapema mno kutangaza kuunga mkono chama chochote katika uchaguzi huo au kutangaza kusimamisha mgombea, tunaweza kufanya hivyo kumbe mgombea kupitia chama chetu anakubalika zaidi ama tunaweza kusimamisha kumbe wa wenzetu ni mzuri,”alisema Ruhuza.

   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  CDM nadhani watachukua jimbo kirahisi
   
 3. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  asante kwa taarifa ningewashauri Chadema hasa wale wanao gombea wawe tayari kutoa ushirikiano kwa mwenzao ataye teuliwa na chama kuwania nafasi hiyo

  aidha ni bora pia vyama vya upinzani vingine viache ushindani kwa CDM na CCM ili kuepuka kugawanya kura

  asante!!
   
 4. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Urio na wewe upo ccm?,nimekushusha kaka
   
 5. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Dah, wengine hata sikutegemea, kumbe nao magamba
   
 6. t

  tisa desemba JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  i like it
   
 7. M

  Makupa JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hivi ina maana mbunge anapata malipo mazuri kuliko mkurugenzi wa shirika la umma tena la kimataifa
   
 8. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,706
  Likes Received: 17,756
  Trophy Points: 280
  CDM wawaachie NCCR nao wajimwaye-mwaye safari hii
   
 9. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Chadema jimbo wanachukua, Joshua Nassary yuko juu ya wote.
   
 10. l

  laleo Member

  #10
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baada ya kufanya utafiti wa kina na kuangalia wagombea wanajitokeza kugombea kuteuliwa na vyama vyao kupeperusha bendera ktk katika jimbo la Arumeru Mashariki,naungana kabisa na wapiga kura wengi kuwa hakuna anayeweza kumshinda Sioi endapo atapitishwa na CCM na yeye mwenyewe kujipanga vizuri.
  Huu ndio ukweli na CCM inatakiwa iangalie hilo kama wanataka kuwepo ktk jimbo hili.Wengine kwa sababu zao wanasema hana uzoefu ila wengi watakubaliana nasi kuwa uzoefu wa kuongea kwenye majukwa na kutia ahadi hew sii muhimu zaidi ya moyo wa ujasiri wa kukabiliana na changamoto za watu wa Meru.Kule Meru huwa tunaamini Maji yaliko pita mwanzo lazima tu yapite tena.
  Nawashauri akina Kaaya's,Urio na Shami kujitoa mara moja na Kuumunga mkono Jemedari Sio Sumari awe mgombea pekee.
  Sioi ni mtu wa kawaida sana,anaweza kuongea lugha ya kawaida kabisa hata na mtu ambaye si sawa na yeye.Na huyu ndie mtu anayetakiwa.Yeye si kama wengine wanatumia mifano ya kuwakejeli wananchi wa Arumeru Mashariki.Wananchi hawataki dharau,wanataka maendeleo.
   
 11. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #11
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,462
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
  Nani alimpa hilo jina la kutooa?

  Hivi mbunge anapatikana kirahisi hivyo?
   
 12. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #12
  Feb 16, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo? Ishauri serikali isipoteze fedha kufanya uchaguzi ilhali mbunge tayari mmeshamchagua!
   
 13. K

  Kiboko Yenu JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 312
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  sioi arts article
   
 14. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Peleka maoni yako ofisi ya CCM mimi nikisikia au kuona neno CCM inabidi nimuone dakatari kwa kuugua kichefuchefu
   
 15. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Umetumwa kumharibia? Ni mapema sana.
   
 16. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #16
  Feb 16, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Umetumwa na Ndugu Manywele?...Mnataka utawala wa Kisultani?...Wewe utapewa hisa ngapi katika dola hiyo?
  Unalipwa shiing' ngapi ukijiunga hapa kwaajili ya kumpigia debe mtu?
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Waachie CCM Arumeru wachague wanayeona anafaa. Kumchagua mgombea nje ya vikao vya chama ni kumharibia. Hizi ni kampeni kabla ya muda.
   
 18. m

  mtengwa JF-Expert Member

  #18
  Feb 16, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,745
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Kwa hyo?
   
 19. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #19
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  A. M 2012 CDM- Reloaded, Stay tuned uone new era politics inavyochezwa na majembe.........
   
 20. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #20
  Feb 16, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  aNA SIFA GANI ZA ZIADA KUWAZIDI HAO UNAOWASHAURI WAJIONDOE?
   
Loading...