Arumeru: Kama unawajua hawa tuambie

Silinde aende Kingori, ule ni ukanda wa wameru wapole, Lema acheze kuanzia Tengeru kuelekea mlimani,ambureni hadi ulong'a,asogee na maeneo ya sing'isi (huu ni upande wa wameru wenye msimamo mkali) na Mnyika asonge maeneo ya Usariver na viunga vyake kuelekea mlimani pia na akave mpaka maji ya chai,.. kikatiti na viunga vyake sio mbaya mdee akapiga kambi akisaidiana na kina mama wengine....zito, Dr. Weapon na mbowe wakiwa na mgombea wafanye kuzunguka pote kuwapa sapoti makamanda. Msigwa asikosekane hadi makanisani jamaa wa pande hizo wako sensitive sana na watumishi wa bwana/kanisa

ila kwa ujumla Lema ni rais wa pande hizi...anakonga nyoyo za wengi mno huku huwezi amini,...unganisha doti utakapojikumbusha tamko la washili, ilikuwa ni hofu tosha kwa jinsi jamaa alivyo na ushawishi
 
Nyerere akae pande za wazee na vibibi vilivyoaminishwa kuwa CCM ni chama cha Nyerere

Hao huku hawapo mkuu,wengi ni single pande hizi, hawana unazi kiasi hicho, hakujawahi kuwa na njaa pande hizi mjomba so ilikuwa ngumu kwa watu wa kundi hilo kurubuniwa na mavazi ya kijani
 
Back
Top Bottom