Arumeru: Dr lwaitama ana haya ya kusema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Arumeru: Dr lwaitama ana haya ya kusema

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by ABRAHAM LINCOLN, Apr 4, 2012.

 1. A

  ABRAHAM LINCOLN Member

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 23, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu Mjengwa,

  Ushauri wako kwa CCM hii ya makuadi wa soko huria na wapenda kusifiwa hata wanapokuwa hawana walilolifanya linalostahili kusifiwa si sahihi kwa maoni yangu. CCM ya leo wala haistahili kupewa ushauri wako wa eti: "CCM ya sasa inapaswa kupanga mikakati ya kuendelea kuongoza dola huku ikishirikiana hata na wapinzani. Ingawa hata huo ni mtihani mgumu wenye kukihitaji chama hicho kuwa na watu makini zaidi badala ya waendekeza fitina na majungu.

  " Hii CCM ya leo ni CCM ya viongozi wanaofikiria kujilimbikizia mali kupita kiasi kwa kutumia mgongo wa kushika dola pekee au na wapinzania walio walafi kama wao na ambao watakubali kutawaliwa na CCM milele. Ushauri unatoa ni hatari kwani si ushauri wa kidemokrasia. Wananchi ndio wanapaswa kupanga nani awatawale si eti "CCM ya sasa inapaswa kupanga mikakati ya kuendelea kuongoza dola huku ikishirikiana hata na wapinzani."


  Yale yale yaliyopangwa gizani Zanzibar na watu wawili ya kugawana madaraka viongozi chama tawala na cha upinzani na kuzalisha vyeo lukuki vya umakamu wa Rais na gharama zake zinabebwa na watu masikini...Kwani cheo cha Waziri Kiongozi na Naibu Waziri Kiongozi vingekuwa na ubaya gani? Leo Tanzania ina Rais 2 na Makamu wa Rais wa 3 na ikianzishwa serikali ya Tanganyika basi tunaweza tukajikuta tunao labda wa Rais 3 na Makamu wa Rais 5 eti? Natumaini huo sio mmoja wa "mikakati ya kuendelea kuongoza dola huku ikishirikiana hata na wapinzani"!!!!


  Hapana!!! CCM kinaitaji kuondolewa madarakani haraka iwezekanavyo kama walivyoonyesha njia watu wa Arumeru. Kikae upinzani nachenyewe na pale wakifurunda Chadema basi Watanzania wawapunzishe na wao na wawarudishe CCM. Huo ndi mfumo wa vyama vingi, Ndugu Mjengwa!. Wanasiasa wanakuwa wanyenyekevu kwa wapinga kura kwa vile wanajua watapunzishwa mara moja wakizembea katika uongozi. CCM iliyoongozwa na kauli za Mheshimiwa Mkapa na Mbunge Lusinde kule Arumeru ilistahili kubwagwa na kuangukia pua na wapiga kura makini maana ilijaa majigambo ya kijinga na kauli za kipuuzi za watu waliolewa madaraka kutokana na chama chao kutawala kwa nusu karne.Tusaidiane


  Mjengwa. Mimi siku hiyo CCM itakapoondolewa madarakani na kuwa chama cha upinzani nitafufua uanachama wangu wa chama hiki kilichokuwa chenye mwelekeo wa kijamaa na kizalendo enzi za Mwalimu Nyerere pamoja na mapungufu yake ya enzi hizo katika nyanja za haki za binadamu na uhuru wa vyombo vya habari. Tanzania inaitaji vyama vikuu viwili makini na vya kizalendo, kimoja chenye kuegemea ujamaa ( CCM) na kingine kuegemea ubepari ( Chadema), lakini vyote vya vikiogozwa na watu wanyenyekevu walio tayari kuwa kwenye upinzani kura za wananchi zikiitaji hivyo.

  Source: Mwl. Lwaitama

   
 2. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  doct.naheshu mawazo yako
   
 3. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Haya maneno mazito na ya msomi kwelikweli , si dr bana
   
 4. Omonto wa-hene

  Omonto wa-hene Senior Member

  #4
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 179
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Daktari Lwaitama nayaheshimu mawazo yako na kuyakubali kiwango kikubwa! Ikiwa kweli aliyekuhoji alikuwa serious na aina ya propositions zake, yaelekea kama anataka kuwaombea CCM ubiya kwa CDM 2015. Ashindwe na alegee kama kweli ni huyu Mjengwa wa Iringa ninayemsoma mara kwa mara!
   
 5. k

  kyening'ombe Member

  #5
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  If you don't think and dicide, other will think and decide for you.
   
 6. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Lwaitama Karibu Chadema
   
 7. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,908
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  Namkubali sana dr Lwaitama kwa uwazi wake.Huyu mara nyingi napenda kumsikiliza.Anakosoa kweli.Mjengwa nilimdharau toka Januari 2006.Alipata kuandika kitu ambacho kilinifanya nitambue ni mchumia tumbo na ni mkereketwa na CCM na pia ni mkereketwa wa Jakaya.Nimeacha kusoma makala zake ambazo nilikuwa nafuatilia sana kwenye Rai.Anatumika vibaya sana na CCM japo yeye mara nyingi kasema hana chama.Ni mwongo ni CCM.
   
 8. m

  mvunjamiwa JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 455
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Dr, anastahili kuheshimiwa kwani amejipambanua kuwa mkweli na mchambuzi makini katika masuala yanayogusa jamii/walio wengi. Hataki kuonyesha unafiki katika masuala yanayojieleza. Muda mwingi nimekuwa nikimfuatilia na kugundua kuwa anachukia sana uonevu bila kujali unafanywa na nani. Nimependezwa na dhana ya kuwa na vyama viwili vikubwa vyenye nguvu ambavyo vinaweza kushindana na yeyote akashinda kwa nguvu za hoja badala ya kuwa na utitiri wa vyana kibao, ambavyo vingine vinaweza kutumika kama wasindikizaji katika siasa. Big up Dr. endelea kuwa hivyo
   
 9. Mlingwa

  Mlingwa JF-Expert Member

  #9
  Apr 7, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 382
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  I salute you Dr.Lwaitama
   
 10. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #10
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  This is what I am praying for, hopefully oneday we will get there.
   
 11. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #11
  Apr 10, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ni heri kuwa mkweli kuliko kusifia kwa unafiki.
   
 12. M

  Malova JF-Expert Member

  #12
  Apr 11, 2012
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Good for your being open and honesty
   
 13. v

  veitvetve New Member

  #13
  Apr 15, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  we need ways which can chunt mafisad down thats nice doctor
   
 14. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #14
  Apr 15, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kibelaaaa imekaa njema hii
   
 15. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #15
  Apr 15, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Namkubali panafricanist huyu, nina maana Dr. lwaitama. anaweza kuwasemea wasio na kauli (mabubu) amaweza kutumia macho yake kwa manufaa ya wasio na nuru ya macho pia, anaweza kuitumia miguu yake kwa manufaa ya wenye ulemavu wa miguu pia, ANAWEZA KUITUMIA AKILI (ubongo) YAKE KWA MANUFAA YA MAMBUMBUMBU.
   
Loading...