Artists of the decade 2010's

el nino

JF-Expert Member
Nov 5, 2013
4,708
2,000
Tukiwa tunaelekea kumaliza muongo mmoja, haya ndiyo maoni yangu kuhusu wasanii bora zaidi wa muziki katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.

1. Diamond Platnumz

There is no competition to the undisputed King of Afro-Pop, King of the East, muite unavyotaka lakini wengi tunakubaliana kuwa Diamond ni the biggest star kwa sasa, katika kipindi cha miaka 10 iliyopita na katika historia ya muziki wa Tanzania.

Numbers don't lie, he is the most streamed artist In Tanzania and East Africa, followers kibao kwenye social networks kumaanisha anafuatiliwa zaidi, kaweka rekodi ya kushindana na media houses na kuzishinda plus ndiye mwanamuziki anayecharge gharama kubwa zaidi kwenye shows zake hapa East Africa.

Kifupi hana mpinzani.

2. Ally Kiba

Huyu sote tunajua alikuwa amepotea kwenye reli akarudishwa kwa lazima kupitia mgongo wa Diamond.

Amejitahidi tangia amerudi maana ni mtu fulani passive sana, kinachomfanya asimame zaidi ni support kubwa ya fans wake tangia amerudi bila wao asingeshika hii nafasi.

Fans wake wamevumilia tabia yake ya kutoa ngoma moja au mbili kwa mwaka, wameonyesha kuzipokea kila zilipotoka bila kujali muda anaokaa kimya, kitu kinachofanya ngoma zake ziende.

3. Nandy

The last sucessful project chini ya mtalaam jasiri muongoza njia, huyu aliletwa kama mbadala wa Ruby ambaye alionekana kuwa mjeuri na asiyependa kutumika kinyonyaji. Nandy hakuchezea nafasi kabisa, out of no where ameweza kumu-outshine Ruby na wanamuziki wengine wengi sana.

She is the most streamed female artist, ana hit songs nyingi sana with a very bright potential.

4. Harmonize

Kutoka jikoni kwa mafundi wa WCB, they created one of the best selling artists in East Africa, projects zake nyingi zimeenda hasa alishoshirikiana na Diamond Platnumz bila kusahau wimbo wake wa Kwangwaru ambao ndio the most viewed YouTube Music Video in Africa 2018, upo mbioni kuwa the most viewed video on Youtube (E.A)

Nimemuweka nambari 4 ila wengine wanaweza kujenga hoja za yeye kuwa namba 3 na zikawa na mantiki kabisa.

5. Rayvanny

Kwa maoni yangu ni more talented than Harmonize, ila shida yake ni huwa hatoi hits back to back na hana consistency, mfano huu mwaka baada ya kutoa tetema alitakiwa aachie mawe ya kutosha, tukashangaa anatoa mediocre materials kama "Naogopa" mara "I Love You "..Bs.

Ukiacha yote, ni bonge moja la msanii. sifa yake kubwa ni uwezo wake mkubwa wa kuandika na kubadilika, akiamua kuwa serious kwa kutoa consistent hits atamchomoa kiba pale juu.

Itaendelea...

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom