Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Naomba ujifunze jambo moja bwana Castr , jitahidi upunguze NEGATIVITY.. nakuona mara nyingi tu huwa unaleta mtazamo hasi jukwaani.

Kwa mfano kuna posts huwa unatuma kabla ya mechi, which are good insights kwa jinsi ulivyoona wewe.. ila ndani yke utaweka dhana ya kukosoa, yani sijui ni kujihami au kutokujiamini. Unajipa negative energy ww na watu wengine wanaosoma.
Sasa sikia nikwambie kitu, hakuna timu iliyo perfect! We mpka unaona kocha amekuanza na timu flani au kafanya mabadiliko flani ndani ya mechi ujue hajakurupuka, tena hiyo ni baada ya kushauriana na benchi lake kujua wanataka nini kwenye mechi.

Sio dhambi kocha nae ni binadamu anaweza kukosea. Wote sisi tunakosea.

Ila nakusihi jaribu kuenjoy football.. hatuwezi kuwa sawa kiuchezaji na PSG, Barcelona, City, Chelsea, etc.. sababu ya utofauti wa wachezaji, aina ya uchezaji, hali ya mchezo, etc, etc.. nadhani unaelewa nikisema hivyo maana ww ndo umetuzidi wote humu kwa kuangalia mechi nyingi yani unaangalia mpka timu ambazo hazikuhusu.

Hivyo usijilinganishe bro, hata kwenye maisha.. just enjoy football.
 
Kwa scenario ya jana still Eze alikua ahead of Dowman kwa hayo uliyosema.. hakukua na haja ya jamaa kucritisize maamuzi ya kocha.
 
Kwa scenario ya jana still Eze alikua ahead of Dowman kwa hayo uliyosema.. hakukua na haja ya jamaa kucritisize maamuzi ya kocha.

yhaa! eze ni mzoefu kuliko dowman ila kuhusu mpira mguuni.. dowman kamzidi kidg eze ,shida yake ni kutokucheza kikubwa.. ubinafsi mwingi na maamuzi yake mengi ni ya kitoto.

ila pamoja na yote hayo.. eze bado hatoshi kwenye LW ,usajili mpya ni muhimu.
 
Wewe jamaa bwana πŸ˜‚

Jitahidi uwe unaelewa. Unaandika sana ila unaandika jibu lisilohusiana
 
Tusihame kwenye maisha, huko nitakosa cha kuandika. Tustick na mpira, ndiyo kitu nakijua.

Wachezaji wana strengths na weaknesses, ikatokea inakukera nikisema mchezaji A ana weakness H ikiwa exploited tumekwisha hapo sina cha kukusaidia.
 
Baada ya mechi ya jana Kompany ameiita Arsenal top opponent.

Zile kauli za mara ya kwanza safari hii hajaziongea
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…