Arsenal (The Gunners) | Special Thread

We jamaa hauko serious kabisa. Yani mechi ya wakubwa unataka acheze mtoto.
Mara 10 uwe na unfit Eze kuliko acheze Dowman ukitegemea akachuane na Davis + Stanisic
Kama kweli umeanza kuangalia mechi za Arsenal zamani kama ulivyodai utakua unajua Fabregas ameanza kucheza akiwa na umri gani hapo Arsenal. Wilshere, Saka et al
 
Tunafanya high press but leo hapa tunahitaji pace kwenda mbele. Madueke anayo ila haitusaidii bado
 
Unawaambia hawa watu kuna kikosi kikianza timu inaenda mbele kwa urahisi mtu anakuja kuanzisha ubishi hauna maana
 
Tumefanya poa.

Wameokolewa na goal line technology.

Jamaa kakumbatia mpira na ikazimwa.

Near miss zilikuepo mbili.

Tumepambana ila jitihada hazishindi kudra
 
Nadhani ni muda ya Kai kuanzia benchi,kocha kamng'ang'ania sana mbele na hatoi kitu tofauti.
 
Kama kweli umeanza kuangalia mechi za Arsenal zamani kama ulivyodai utakua unajua Fabregas ameanza kucheza akiwa na umri gani hapo Arsenal. Wilshere, Saka et al
Mzee tumia akili, huwezi kuweka mfano wa hivyo kwa scenario ya sasa.

Kwa mfano Wilshere alianza game vs Barcelona sio kwa sababu tu alikua mdogo, ni kwamba alikua regular starter kwenye kikosi cha Wenger, yani alishacheza mechi nyingi tu huko nyuma.. ko haikua tu majaribio kisa ni wonderkid ndo acheze..

Pia kwa kipindi hicho Wilshere alikua 18 km sio 19, ni sawa na kusema hii mechi angeanza Myles LS tungekuelewa coz alishakua regular.
 
Unawaambia hawa watu kuna kikosi kikianza timu inaenda mbele kwa urahisi mtu anakuja kuanzisha ubishi hauna maana
Mzee wewe hauna hata leseni ya kufundisha sekondari unakuja na uchambuzi wako wa mitandaoni ukirekebishwa unatafuta sababu, sasa wewe na Arteta nani anawajua wachezaji vizuri..
 
Saka nje.

Now kwa aliyeingia tuone kama anaweza offer zaidi ya anachooffer Saka.

Personally, hii mechi Dowman inamhusu
Huyo mtoto Dowman bado sana bado kana maamuzi ya kijinga jinga tu kanatakaga kukaa na mpira muda mwingi mpk kanapoteza na kukaba pia hawezi, ni heri kubaki na Madueke ndani mwanzo mwisho
 
Nimemtaja Fabregas kaka mbona hujamuelezea huyo?

Wewe unavyohisi mtu hadi anafika 18 anakua regular haitokani na kwamba amegewa time kidogo kidogo kabla hajawa 18?

Leo unamjua Lamine Yamal ameanza kua integrated kwenye timu akiwa na umri gani? Messi anaingia sub na kunyanyasa CL alikua na umri gani?
 
Mzee wewe hauna hata leseni ya kufundisha sekondari unakuja na uchambuzi wako wa mitandaoni ukirekebishwa unatafuta sababu, sasa wewe na Arteta nani anawajua wachezaji vizuri..
Mimi leseni sina. Wewe kama unayo ni sawa tu.

Kwani mashabiki wanavyokua wanasema hawamtaki kocha hua wanawajua hao wachezaji kuliko kocha? Shabiki maarufu wa united, Mark Goldbridge, anawajua wachezaji kuliko Moyes? Ole? Rangnick? Carrick? Mbona hua wanafukuzwa kweli.

Kaa chini uwe unaangalia mechi. Kama unaweza angalia mechi za timu zote ili uache kuhisi kujua kutazama movements za timu ni mitandao.
 
Huyo mtoto Dowman bado sana bado kana maamuzi ya kijinga jinga tu kanatakaga kukaa na mpira muda mwingi mpk kanapoteza na kukaba pia hawezi, ni heri kubaki na Madueke ndani mwanzo mwisho
Maoni juu ya mchezaji hua hayafanani kuna watu walimuangalia Partey wakasema Partey ni kiazi. Kuna watu wanamuangalia Kai wanamuona ni mchezaji mzuri. Kuna watu tunamuangalia Saka tunaona ni mchezaji mzuri.

It's fine wewe kuona hivi.
 
Unaanza kunipa wasiwasi na uchanganuzi wako wa mambo.. nimemuelezea mmoja kwa kuwa sababu ni hiyo hiyo.

Listen, Wenger alikua na tabia ya kuwaamini wachezaji wenye kipaji kwenye umri mdgo na kuwapa nafasi, ila hakufanya tu abrupt kwa kushtukiza au kwa mihemko km unavyofkiri wewe.

Narudia kule kule, young Cesc alikua ni regular starter kwenye kikosi japo umri wke ulikua mdgo. Ni km Myles Lewis Skelly, hakuna mtu angelalamika km Myles angeanza kwa sababu amekua akicheza kwenye hiyo nafasi kwa muda mrefu na anaelewana vizuri na wenzie.

Mfano mwengine ni Denilson japo hakutoka academy ila alisajiliwa kwenye umri mdgo ilimchukua muda mpka kuwa regular na baada ya kuaminikiwa... same same story!

Halafu unafurahisha kweli, kwahiyo Messi alianza tu kuwanyanyasa watu kwenye UEFA au sio😂 kasome tena story ya Messi ila unatakiwa uelewe ilimchkua zaidi ya msimu mmoja mpaka miwili kuwa regular starter kwa Barcelona.. nenda kapitie pia story ya Lamine ujishughulishe kidgo labda utaelewa.
 
😂 kwa majibu haya naamini umeanza kuelewa ila bado unarudi tena kule kule na kichogo chako..

Kwahiyo shabiki akimfukuzisha kocha ndio anajua? Wangapi baada ya kocha kufukuzwa wanakuja kusema uongozi ulikosea na wangetamani kocha apewe muda?

Mashabiki wangapi wa Arsenal walitaka Mikel aondolewe baada ya kuanza vibaya?
 
Shabiki maarufu wa united, Mark Goldbridge, anawajua wachezaji kuliko Moyes? Ole? Rangnick? Carrick? Mbona hua wanafukuzwa kweli.
Haya tuambie wewe mtu wa mitandao, huyo shabiki maarufu akishamfukuzisha kazi kocha wewe unaamini moja kwa moja tatizo ni la kocha?
Kwamba huyo shabiki anawajua sana wachezaji, kwamba yupi anastahili kucheza dakika ngapi.. simple fact as that eeh?!
 
Kaa chini uwe unaangalia mechi. Kama unaweza angalia mechi za timu zote ili uache kuhisi kujua kutazama movements za timu ni mitandao.
Kwahiyo wewe kwa akili hiyo na unavyoelezea mambo ndio faida uliyoipata kwa kuangalia mechi zote au sio..
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…