Sisi ambao tumeanza kufuatilia mpira kabla ya ujio wa makocha wanaodictate kuanzia kujiposition mpaka idadi ya pasi tulikua tunamuangalia mchezaji na kufurahia anachofanya.
Hatukuwahi kua busy kuangalia statistics iwe pasi, chance creation au assists. Ndiyo sababu kizazi chetu kilimheshimu Drogba na kuamini ni bonge la striker.
Lakini hivi karibuni wameanza kumuita average kwakua amefunga magoli 104 misimu 9 aliyoishi EPL. Ni kama kusema kila msimu alikua na wastani wa magoli 11.4.
Kwa mpira wa siku hizi Okocha na Ronaldinho wangeonekana hawajui kwakua entertainment waliyonayo miguuni haikupi magoli constantly. Tulienjoy kuona akifanya step overs, akizipiga roulettes, akiwapiga watu kanzu. Magoli atafunga Etoo ila macho yetu kwa Dinho.
Na tutakumbuka goli la Dinho dhidi ya Chelsea alilofunga huku anakata viuno kuliko magoli mengi ya Etoo.
Newcastle walikua na mtu anaitwa Alan StMaximin, aina ya wachezaji kama Okocha. Bahati mbaya alikuja era ambayo ule mpira unahesabiwa unakwamisha mashambulizi akauzwa China.
Angalia ligi ya EPL wachezaji wangapi wanajiexpress kama Ronaldinho? Hakuna. Sana sana mchezaji atafanya step over au atafanya body faint ili a-cut in ashoot. Kwa miaka yetu ya karibuni waasisi wa aina hii ya wing alikua Ribery na Roben.
United walinunua winger ambaye ilidhaniwa atakuja na hizo expressions na kunyanyasa mabeki, Antony, hakumaliza misimu miwili.
Sasa tuje kwa Saka. Timu ya taifa ya UK alikuepo Southgate kama kocha alikua akiita timu ya taifa Saka anaanza, akipumzika anaingia Madueke au Palmer.
Amekuja Tuchel, huyu sasa hata kumuita Palmer timu ya taifa hajamuita na walikua wote chelsea hawa. Sasa swali ni imekuaje makocha wanne wote wanaona Saka anatakiwa awe kule alipo?
Jibu jepesi ni output. Na hii ilisemwa mwanzoni kabisa msimu wa 22/23 kwamba hana madoido anautegemea sana mguu wa kushoto lakini haina shida kwakua anautendea haki mguu wake wa kushoto.
Saka alikua mchezaji mwenye speed kuliko Martinelli. Alivyopata injury na kurudi amepunguza kukimbia na decision making imekua ya uoga tofauti na mwanzo lakini Arsenal bado haina RW wa kumsusia wing ile. Usifananishe Dowman na Yamal kwakua Yamal anacheza ligi ambayo Rodri anaishangaa inakuaje na wachezaji dhaifu wapo ligi kuu.
Pili angalia Saka akipata mpira anatakiwa kuwavuka wachezaji wangapi? Mara nyingi ni wawili au watatu na kilichosemwa msimu wa 22/23 kwamba hana madoido bado tunakiona hapa kwamba hawezi wachambua watu watatu bila kutoa pasi.
Tafuta wingers wa timu zingine hua wanazingirwa na wapinzani wangapi ili kuelewa kwanini huyu dogo kila kocha anaona ni mtu sahihi kua RW.