Pole sana jirani.....Naona jahazi linazidi kuzama......Mshalambwa kimoko na Bosingwa na Drgoba wamelamba mwekundu.....Kuna kipindi marefa huwa wanaumiza sana aisee.....Penati na red card mbili inakuwa ni kuumizana jamani....
Arsenal ile back four ilikuwa inajipanga na huko mbele utaona ushirikiano mzuri baina ya Mertesacker na Vermaelen akirudi. Santos nae ni beki mzuri sana.
Kulikuwa na tatizo la mawasiliano na sasa Mertesacker anafanya mawasiliano mazuri na mabeki wenzake na wanaweza kujipanga uzuri.
Ila leo tena palikuwa na tatizo na huyu Laurent Koscielny ambae ndie atatupa matatizo sana na mipira ya adhabu ambayo ni yeye anasababisha. Lakini kuna mchango mkubwa anatoa wakti Vermaelen bado yupo nje.
Mimi naamini Arsenal itashinda mechi sita kuanzia ile ya Sunderland, Marseille, sasa Stoke na wanafuatia Bolton halafu Chelsea pale Stanford Bridge na Marseille tena pale Emirates.
Adui mwombee njaa,cha ajabu ni pale Van Persie atakaposaini long term na Arsenal,na hili naliandika na litatokea.Kwa ushauri wangu ni kuwa tusikimbiane hapo J'mosi mchana.