Katika kikao kwa kutumia Application ya Zoom iliyohusisha wachezaji wa Arsenal, kocha mkuu Mikel Arteta na kocha wa Vijana Per Mertesacker,
Prince William, shabiki wa Astonivilla,
Waliuliza kwa Utani kuhusu Aubameyang kuhamia Villa Park.
Kikao hicho cha Video ilikuwa kujadili maswala ya afya ya akili, na mchezo wa fainali ya Kombe la FA kubadilishwa jina na kuitwa
"Heads Up FA Cup final"
baada ya Emirates kuruhusu haki ya jina hilo kutumika kwenye Faunal.
Na Duke wa Cambridge alisema:
"Nilitaka kusema kuwa ni kweli ninatumaini Piere utakuwa Aston Villa msimu ujao."
Mertesacker, Aubameyang na Hector Bellerin basi walionekana kucheka,
lakini majibu ya Arteta yalikuwa tofauti kidogo.
Arteta alikuwa na tabasamu usoni mwake, lakini pia alionekana akiweka mkono wake hewani na kuushusha kutoka upande kwa upande kuiashiria 'hapana, hapana.
Je! Hiyo ni hatua kuzizuia klabu zingine zozote zinazomtaka Auba?
Mashabiki wa Arsenal wanatarajia hivo