Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Wakuu tutamlaumu sana kocha ila timu yetu ina matatizo makubwa mawili ambayo nimeyaona;

Kwanza timu haitengenezi nafasi nyingi za kufunga, dakika zote 90 timu inatengeneza nafasi 3 tu hapo unategemea nini?.

Pili timu haina uwezo wa kuzuia, inaruhusu mashambulizi mengi ambayo huletea kufanyika kwa makosa mengi golini.

Hali ikiendelea hivi tutarajie maumivu zaidi.
 
Aaron arsenal anaugulia tu maumivu huko.....na leo kama chelsea wakishinda basi yule ollachunga atapiga kambi hapa
 
Haya yote ni uzembe wa kocha lakini...yeye ndo kashindwa kurekebesha makosa
 
Nliisema na narudia hii kauli
 
Sasa kama timu haishambulii na haiwezi kuzuia, wewe unataka tumulaumu nani kama sio kocha?
 
Alafu nijuavyo mimi hakuna mchezaji wakufikia kuonwa na timu kubwa kama Arsenal akawa hajui kucheza mpira. Hivyo kazi ya kocha ni kumfundisha mchezaji mbinu ya kutumia kipaji chake na nafasi yake hiyo. Na kumfanya mchezaji kuendeleza ubora wake na kuiwezasha XI kuwa bora inapokuwa na mpinzani na kutambuwa chakufanya kama timu wanapokutana na mpinzani.
 
Hahaha naona wenye jukwaa kina Aaron, dully na wengineo wamelikimbia jukwaa lao

Msisahau kunitag wakuu kwenye breaking news ya muhindi wenu kufukuzwa Naendelea kukumbushia tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…