BUKAYO SAKA KINDA ALIYEWACHONGANISHA' UNAI EMERY NA LJUMBERG...
Anachukuliwa kama kinda mwenye kipaji cha hali ya juu sana ndani ya Arsenal.
Kipaji na uwezo wake uliwafanya Emery na Ljumberg watofautiane.
Unaweza kusena Bakayo Saka ndiye success story ya Fredrick Ljumberg tangu arejee Arsenal kama kocha.
Alimkuta akiwa na miaka 15 na akiwa anachezeshwa kama beki 3, akaamua kumbadilisha kuwa winga. Siku zote Ljumberg amesisitiza kwamba Saka ni gwiji wa soka mtarajiwa.
Msimu jana Ljumberg alimshauri Emery amtumie kwenye Europa. Alipoanza kumtumia Emery alitaka apandishwe kikosi cha kwanza, kitu ambacho Ljumberg hakukubaliana nacho akitaka Saka aachwe amalize msimu mwingine angalau mmoja U23.
Unaweza kusema pia Saka amechangia kiasi kikubwa Ljumberg kupandishwa kuwa kocha msaidizi kikosi cha kwanza. Kwa sababu kwanza jinsi alivyoweza kumtengeneza mpaka akafikia hapo. Pili Ljumberg alipandishwa ili awe daraja kati ya vijana wanaotoka academy kwenda kikosi cha kwanza.
Saka amesababisha maamuzi makubwa kwenye timu. Alichangia kiasi kikubwa kuuzwa kwa Iwobi.
Baada ya miaka mingi ya kumvumila Iwobi afikie matarajio ya timu kwake ilifika wakati wakaona kama anawabania Saka, Nelson na Martinelli hasa hasa Saka.
Ni vigumu kutabiri kwa uhakika future ya wachezaji wadogo.
Ndiyo maana academy yenye wachezaji 200 wanaofanikiwa kupenya kikosi cha kwanza ni mmoja wawili. Lakini matarajio kwa Saka kwenye viunga vya Emirates ni makubwa mno.
Katika Hale end acardemy Napendezwa na EDDIE NKETIAH , SAKA , BOLOGUN ,
Aaron