ANACHOJARIBU UNAI EMERY...
Jana nimesoma exclusive interview ya Guillem Balague kuhusu mtazamo wake kwa Unai, alisema kazi ya Emery ni ngumu kwa sababu anabadilisha utamaduni wa Arsenal. Ian Wright aliwahi kusema wakati wa Wenger wachezaji hasa wadogo walikuwa wakikwepa mazoezi wakisingizia wanaumwa.
Kila mchezaji aliyewahi kuwa chini ya Unai anatoa ushuhuda ni very demanding coach. Hampangi mtu anayezembea mazoezi. Labda tujiulize Ozil kakosa mechi ngapi bila majeruhi lkn akisingizia kuumwa? Siku moja Unai aliulizwa lini Ozil amepata maumivu ya mgongo akasema 'sijui'.
Unai aliamua kuanza na big fish. Aubameyang aliwahi kusema ukikosa goli kwenye mazoezi unapigishwa push up 300. Lacazette mara kibao amepigwa sub, Ramsey bench.
Wanaofuata maelekezo yake wanapiga kila game. Iwobi, Guendouzi, Kolasinac utawaona kila mechi. Jana kabla ya mechi ya Bate Martin Kewon alisema ameambiwa Ozil alitrain vzr sana wiki nzima. Na kweli Unai kathibitisha kwamba kwa wiki mbili amefanya vzr mazoezini.
Lkn pia mashabiki wa Arsenal wajue kila timu ina utamaduni wake. Sioni mchezaji akisababisha kocha kufukuzwa kazi. Alichofanya Pogba kwa Moulinho au wanachokaribia kumfanyia Sarri akina Hazard usitarajie kukiona Arsenal. Kocha wa Arsenal atashinda battle na mchezaji yoyote any time any day
Aroon Toreira
View attachment 1028921
Sent using
Jamii Forums mobile app