Wakuu niaje?, naona Arsenal sasa imekamilika kila idara na kwa kweli tushindwe sisi tu.
Wachezaji wengi isipokuwa Theo Walcott ni salama tayari kumalizia mechi 16 za ligi kuu ya Uingereza pamoja na CHampions league na FA Cup.
Aaron Ramsey, Lucas Podolski, Nicklas Bendtner, Alex Oxlade Chamberlain wote sasa wapo fit.
Ni Yaya Sanogo na Abou Vasiriki Diabi ndio wanaobakia kuuguza majeraha.
Kuhusu usajili kama ilivokuwa ikitarajiwa kuwa Arsenal wangesajili wachezaji kadhaa, hali haijawa hivo na wachezai hao imekuwa ni vigumu kuwapata kwa msimu huu wa baridi.
Lakini jioni hii chanzo kimoja cha habari na ambae ndie aletoa dondoo kuhusu deal la Mesut Ozil, ametoa dondoo usiku huu kwamba deal la Julian Draxler limekubaliwa na Schalke na huenda mchezaji huyo akaingia London wiki ijayo kukamilisha taratibu za usajili.
Julian Draxler
Schalke walikuwa wanataka pesa yote ya milioni 37 zilipwe na inaonekana kumekuwa na "breakthrough".
Meneja Arsene Wenger anataka kumbadilisha Draxler awe mshambuliaji kama alivofanya kwa Robin Van Persie ambae Arsenal ilimsajili kutoka Feyenoord.
Van Persie alisajiliwa na Arsenal mwaka 2004 kuchukua nafasi ya Dennis Bergkamp na alikuwa akicheza kwenye nafasi ya kiungo pale Feyenoord.
Baadae Van Persie alikuja kuwa mmoja wa washambuliaji hatari kabisa kwenye ligi kuu ya Uingereza na barani Ulaya kwa ujumla.
Kama Draxler atakuja Arsenal basi atakuwa ni mmoja wa washambuliaji makini baada ya kufuata maagizo ya kitaalam ya meneja Arsene Wenger.