Nimetoka kuangalia mechi dhidi ya Everton, morali ya Arsenal hainiridhishi kabisa, tunawaonea sana vibonde lakini tunapokutana na mitihani ya kweli tunashindwa kuonyesha uwezo wetu, sasa sijui hizi mechi mbili kati ya Chelsea na Man City kama tutachomoka. Napata wasiwasi sana isije ikawa ni nguvu ya soda. wenzangu mnaonaje?
Ni matokeo mazuri tu na kama tungeshinda leo tungekuwa na uhakika zaidi wa kuanza kujiandaa kama mabingwa watarajiwa.
Kama unafuatilia hasa timu yetu hii, msimu wa 2003/04 hadi kufikia mechi 15 kama leo tulikuwa na idadi ya points 35 na ni msimu ule tulikwenda kuwa mabingwa bila kupoteza hata mechi moja, yaani kushinda mechi 26 na kutoa sare mechi 12.
Ni katika msimu ule ndio tuliweza kuboresha mikataba ya Patrick Vieira na Robert Peres na pia tuliwanunua Antony Reyes na Kipa Jens Rehmnan.
Msimu wa 2007/08 tulikuwa na 37 points baada pia ya kucheza mechi 15, lakini tukavurugwa na uondokaji wa Thiery Henry, Fredie Ljumberg na Antony Reyes na msimu ule tukamaliza tukishika nafasi ya tatu.
Hizi mechi na Everton, Man City na Chelsea hata tukitoa sare haitakuwa mbaya ingawa ushindi unatuweka mahali pazuri zaidi.
Kosa moja kubwa la mzee Wenger leo lilikuwa ni upangaji wa kikosi chake. Ilitakiwa Theo Walcott aanze ili aweze kutafuta nafasi kwa Giroud au Ozil.
Yule beki wa kulia wa Everton Oviedo, alikuwa na raha sana mpaka Walcott alipoingia na kuandaa chumba kwa Ozila kufunga kwahio ilibidi Walcott aanze.
Pili, Flamini na Rosiky wangeanza badala ya Cazorla na Wilshere. Unajua mechi kubwa kama hizi tena ambazo timu kama Everton imetoka kukung'uta watu huko old Traford unatakiwa nawe ujiandae kisawasawa na kwahio Wenger angeanza na Walcott Flamini na Rosiky badala ya kuwaingiza kipindi cha pili.
Lakini tusiwe na wasiwasi ni baadhi tu ya pundits na wanaotabiri mabaya ndio wanaleta mambo ya Arsenal wana mitihani na Man City au mara wana mtihani na Chelsea, hiyo yote ni hofu kwamba Arsenal mwaka huu wamepania "to prove everyone wrong".
Watu wamesahu kuongelea jinsi Chelsea walivyofanyiwa mbaya na Stoke kule Liberty Stadium ambako Arsenal tuliwafunga haohao Stoke, au Man City ambao jana nao wakatoa sare na Southampton, hakuna mjadala huo.
Sembuse Arsenal kuwa 5 points clear leo hii.