Huyu ndie aliyemuua yule sheikh mlemavu Yassin muasisi wa Hamas, huyu ndie muuaji wa Yasser Arafat. Ameionja joto ya mateso hapahapa duniani.
Mola ampokee panapomstahili, maana aliamuru mpaka misikiti mitakatifu kuingiliwa na askari wake wakiwa na viatu.
Nakumbuka jinsi alivyoibomoa ikulu ya Arafat na kutaka kumuua, walifaulu kumuua kwa sumu hauati Arafat huku chief negotiator wa Palestine Saeb Erakat akipaza kelele nyingi juu ya uonevu wanaopewa na Israel ya Sharon ambapo Marekani ya Bush jr na Collin Powel wakiitazama tu hali hiyo.
Kwa Israel, ni Yitzhak Rabbin pekee ndie alikuwa muungwana akifuatiwa kwa mbali na Shimon Peres rais wa sasa wa Israel.
Pumzika unapostahili ewe Ariel Sharon, coma ya miaka takriban nane si mchezo.