Alikuwa kwenye coma tangu 2006 baada ya kupata kiharusi (stroke). Anachukuliwa kama jemedari katika medani za siasa na kivita kwao Israel, akiwa ameshiriki na kuongoza(kama kamanda) vita 4 za taifa hilo dhidi ya mataifa ya kiarabu. Kabla ya kuwa waziri mkuu kuanzia 2001, aliwahi kuwa waziri wa ulinzi kabla ya kuachia kutokana na kashfa ya mauaji ya maelfu ya wa palestina katika kambi za wakimbizi nchini lebanon. Kabla ya kushiriki siasa, alikuwa afisa wa jeshi la ulinzi la israel akifikia cheo cha meja jenerali.