- Thread starter
- #41
Ainisha jambo gani ? Ukiona halipo kwenye kitabu ujue kwamba kitabu kimekupa muongozo wa wapi pakupata hilo jambo. Ndiyo maana kitabu kikasema "Waulizeni wenye kufahamu mkiwa nyinyi hamfahamu". Hii ni katika adabu za kutafuta elimu na kutaka kuyajua mambo.hilo jambo halijatolewa majibu kwenye hicho kitabu?
Ngoja nikupe mfano katika Qur'aan na Hadithi, hukuti wapi kumeandikwa ya kuwa Bangi ni haramu au Sigara ni haramu,ila kuna msingi wa ujumla upo katika Qur'aan na Hadithi, unao sema usijidhuru nafsi yako na mfano wa hayo.
Sasa unaposema usilo lijua ukibainishiwa tafakari uone wapi unakosea.
Hii sasa ndiyo maana ya kitabu cha kuongoza watu, kitabu ambacho hakina shaka ndani yake. Qur'aan si kitabu cha Sayansi wala mfano wake, bali ni kitabu cha kuwaongoza watu na kuwaonyesha njia. Ndiyo maana kikatuongoza sisi ya kuwa kama hatujui basi tuwaulize wanao jua, maana yake kinajua ya kuwa wapo wanao jua na wasio jua kama wewe.kwa maana hiyo dini yako kupitia kitabu chake haina maarifa yeyote kuhusiana na umeme mpaka iwatake watu wanaotaka kuujua waende kwa wajuzi walioweza kuujua umeme bila msaada wa hicho kitabu?
Huko ndiyo kugusa kila kitu, tena kinakupa muongozo.hapana. hapo umenionesha kua sio kitabu kilicho gusa kila kitu na ndio maana mnaelekezwa kupata maarifa nje ya hicho kitabu
Shida yako huwa unavamia mambo yaliyo kuzidi uwezo. Nilikwambia hapo awali ya kuwa unaposema ni mapendekezo ya watu, unatakiwa uthibitishw ya kuwa kweli ni mapendekezo. Usilete habari za vilingeni kijana. Onyesha tu vitu viwili hivi :kitabu kuitwa muongozo wa watu sio kigezo cha kuonesha hakina shaka, ni mapendekezo ya watu tu kuitwa "muongozo" na kamwe muongozo huo hauwezi kuvuka mipaka nje ya jamii hiyo ya watu waliokipendekeza. Ni kama ilivyo katiba ya nchi ya tanzania kuwa muongozo wa nchi hii kutokuwa na authority ya kisheria katika nchi ya kenya
1. Umashaka katika hicho kitabu (ukiweza nitaomba hiii ID yangu ifungwe maisha)
2. Onyesha mapendekezo hayo kwa ushahidi.
Nikikuuliza ya kuwa upi ushahidk wa kuonyesha ya kuwa katiba ya nchi ni mapendekezo na makubaliano ya watu hili bila shaa utaweza kunipa ushahidi huo, sasa nataka unipe ushahidi unao onyesha ya kuwa Qur'aan kuitwa muongozo kwa watu, ni mapendekezo au ni zao la mapendekezo ya watu fulani.