Sasa unategemea nini kama vijana wanaona wanaume/wababa wengi wa kuwaiga ni wale walegevu legevu wanao-lack strong characters, morality and values. Inasikitisha lakini lazima nao waishie kuwa kama hao wengi.
1. kwa sasa wanaume wengi wanachumia matumbo yao na wapenzi wao......
2. uongozi wa familia tu imekuwa ishu, sembuse wa taifa? leo nilikuwa namuwashia moto rafiki yangu, kaolewa na akakabidhiwa binti mkubwa tu ambaye naweza kusema ni ndugu wa mbali wa mume, wamsaidie. wamekaa na binti miaka 10, binti ana tabia mbaya usiseme, lakini wanaendelea kukaa naye tu sababu eti mume anaogopa akimrudisha binti kwa wazazi wake ndugu watamsema........can you imagine this? mume unashindwa kuchukua maamuzi (tena hata siwezi kuyaita magumu) katika hili je tukikukabidhi ujumbe wa nyumba kumi utaweza? let alone uongozi wa juu.
Kwa Kina mama na wake ndo wakulaumiwa sana. Wanalea tabia mbaya za watoto wao nyumbani na wakikua wanakuwa hawana msaada. Wengine kwa tamaa za wanaume na mali wamewasahau watoto wao hata kujali kukua kwao. Wengine wamewashirikisha watoto wao kwenye uovu hata wakashindwa kuwakemea tena. Wanawalea watoto wao kama mayai wakikua wanashindwa kuhimili mapambano ya dunia kwa kushindwa kuwa wabunifu wa harakati za maisha. Wameshindwa kuwafundisha watoto maisha halisi ya kwao na kuendekeza ukisasa unaoharibu kujiamini kwa watoto wao.
Kutwa wake wanajifunza namna ya kuwa bora kwa waume zao na kuendelea kushindana na hawara za waume zao wakisahau kuwa watoto wao ndo wana safari ndefu kuliko hao wanaume. Wameshindwa kutumia nafasi yao ya kuwa "wake" kuwashawishi waume wao wajali vizazi vyao hadi watoto wanakosa huduma muhimu. Wanabembeleza wanaume magoigoi kwa kisingizio cha mapenzi na heshima kwa mme hadi nyumba zinakosa dira. Wanalia kwa watoto wao kuhusu madhaifu ya baba zao watoto wanakosa heshima kwa baba na jamii. Wanaacha kujitathimini na kushinda makanisani kutafuta suluhu za matatizo ya ndoa wakati wao wana mchango mkubwa katika matatizo hayo.
Familia zao huishi tamaa zao kuwaridhisha.
Katika nyumba hizi hatoki mwanaume au mwanamke jasiri, mwaminifu anajijali na kujali wengine.
Nikisemaga Miafrika ndivyo tulivyo mnaniona mwehu.
Ukweli ni kwamba haijalishi ni jinsia gani imeshika nafasi nyingi za uongozi.
Uongozi bora hauna cha mwanamke wala mwanamme.
mimi sitaki kujiaminisha hivyo....Kwa hiyo natakiwa kuamini hawapo tena? Je watuachie nafasi sie tujaribu? Wako tayari?
Mie sasa hivi naanza kuchanganyikiwa na hii dhana ya mwanamme kuwa kiongozi kwa kweli
Tukianza kuhoji kama sie tulotoka 'bupandagila' tunaanza kuambiwa 'unajidai umesoma unaelewa sana'
Sijui kuna mahali najichanganya.
mimi sitaki kujiaminisha hivyo....
najua wapo wengi tu, ila sisi hatuoni tumpe nani, kwa maana hiyo kosa ni letu.
kati ya vitu sitaki hasa kwa ngazi ya nyumba yangu ni mimi kiwa kichwa cha nyumba, sitaki kabisa
@Kongosho my dear,
Ubinafsiii umezidi mama yaani we acha tu
Nimeamua kuleta mada hii kutokana na ‘upepo' wa kisiasa/kitaifa unaolikumba taifa letu. Mie naona kila kitu vululuvululu. Hivi ‘wanamme' wetu wameenda wapi? Wako wapi wale wanamme tulioaminishwa ni ‘vichwa' vya familia na taifa?
Those strong, fearless, courageous, invulnerable, greatthinker and intellectually bright men? Where are our men waliokoe taifa? If our men are lost we are more lost.
Najua hata wanawake wana nafasi katika hilo lakini hadikufikia sasa asilimia kubwa ya uongozi uko chini ya wanamme, hadi 2005 wanawakewalikuwa 31%(including special seats) ukiondoa viti maalumu ni kama 9%
Do we need deconstruction and construction?
Hivi tunahitaji deconstruction ya "the myth of a strong man' and ‘Man asprotector and provider' Kwa sababu they have been challenged kwenye hili kuanzia ngazi za familia hadi kitaifa, hivi wanawake tunahitaji ku-adjust akili zetu tuondokane na hii delusion? Nielezeni.
May be a new construction of idea zinahitajika, kama ‘women and men partnership' ambapo kila component inapewa fursa sawa pamoja na ‘collective intelligence and collective leadership'room for debate, participation, recognition kwa wake na waume katika maendeleo.
Nikiongea kwa mtazamo wa niliyofundishwa na jamii iliyonikuza, kweli nahangaika sana kuwatafuta wanamme wetu kitaifa. Sitaki kuangalia chama wala nini, nataka kuangalia wanamme wetu tu, wako wapi, ni nini kinawapata? Mnapitia nini?
usisahau pia kuna kulipa fadhila rafiki....Nakumbuka, nilienda kufacilitate training moja kwenye kijiji kimoja baada ya kupata request ya mafunzo hayo kwa muda mrefu sana. So kwenye mkutano na serikali ya kijiji, niliweka karata mezani; nini twaweza fanya na nini hatutafanya.
Mafunzo hayo yalikuwa ya juma zima na ni mafunzo kwa vitendo, hakukuwa na payment kwa mafunzo ila tunge nunua vitu vile ambavyo wangetengeneza mwisho wa siku na kugaia wana kijiji.
Mwenyekiti yule akajitolea chakula cha ile team itakayopokea mafunzo cha siku 4 (watu kama 20 hivi); l was so impressed and moved kiasi kwamba nikatoa 100,000 ya kwangu (sio shirika) ili kuongezea kwenye chakula. Huyu ni tofauti na wenyeviti wengi ambao ukienda fanya nao mkutano, na kuwaambia kuhusu training; kwanza atatafuta ndugu zake ndio wawe kwenye kamati (anawazia posho) halafu mwisho wa siku hakuna kinachofanyika. Hao ndio tunao wengi sana hadi ngazi ya kitaifa; ni JANGA kwa kweli.
usisahau pia kuna kulipa fadhila rafiki....
hata kama siyo ndugu basi kuna wale waliotufanyia kitu kwa hiyo angalau tuwape ukuu wa wilaya tu, hata kama hawa-deserve, lol!