Wizara ya Ardhi
Govt Institution
- May 14, 2024
- 255
- 150
Msajili wa Hati Nchini, Bw. David Mshendwa, amemkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Chato, Bw. Louis Bura, Hati Miliki aliyopata kupitia Kliniki ya Ardhi inayoendelea katika Viwanja vya Maonesho ya Madini mkoani Geita.
Kupitia Kliniki hiyo, wananchi wanapata fursa ya kupata elimu na ushauri kuhusu matumizi ya Mfumo wa e-Ardhi katika kuanzisha na kufuatilia miamala mbalimbali ya masuala ya ardhi, kukadiriwa kodi ya pango la ardhi, pamoja na kupata huduma nyingine zinazotolewa na Sekta ya Ardhi.
Ikumbukwe kuwa, Kliniki ya Ardhi inaendelea katika mikoa yote ya Tanzania Bara na inatarajiwa kuhitimishwa tarehe 3 Oktoba 2026.
Karibu tukuhudumie hujachelewa
#ardhikidijiti
#ardhisalama
#ulipotupo