April '09 Bomb Blasts in Dar (Mbagala) and responses

Hapana, nimeelezwa milipuko hiyo inayosababisha moshi mkubwa hewani ipo maeneo ya Mbagala ilipo ghala ya silaha za Jeshi.

Wewe uko sawa katika kutufahamisha lakini kuna watu wanakuwa wanapotosha... Keep it up kaka tunasoma tufahamu ni nini maana wengine maofisi yako mwelekeo huo sasa unaweza toka nje ghafla ukumbane na mabalaa...
 
Kwa taarifa nilizozipata za hapa na pale ,ni kambi ya jeshi ,ghala la kuhifadhia silaha limewaka moto,na mabomu yanalipuka as a result,na watu wameumia nimesikia
 
najaribu kuwapigia baadhi ya wahariri naona wote wako busy is going to be big story kesho
 
Watu wameambiwa wasiende kwenye eneo la tukio

lakini mijitu mingine itakimbilia kwenda kuangalia ni sawa na wale wanaokimbilia kwenye magari ya mafuta kuchota wanaishia kuungua..
kule hakuna kitu labda vyuma chakavu

mtadhurika hakuna cha kuchukua kule
 
kupotea mawasiliano kwa wale wanaotumia network ya TIGO kunahusiana na hili wajameni? maanake siwezi piga simu ...
 
Watu wameambiwa wasiende kwenye eneo la tukio

lakini mijitu mingine itakimbilia kwenda kuangalia ni sawa na wale wanaokimbilia kwenye magari ya mafuta kuchota wanaishia kuungua..
kule hakuna kitu labda vyuma chakavu

mtadhurika hakuna cha kuchukua kule

Mkuu usinichekeshe.....huu ujasiri wa kipuuuzi namna hii ndiyo maaana hata tunaangamia kwa ukimwi
 
hapa ndio tutaona ufanisi wa kitengo cha maafa ofisi ya waziri mkuu
 
--------------------------------------------------------------------------------

kwani hii ya leo inatofauti na ile ya jana?

maana jana i was so uncomfortable..unajua tena you never know hawa CHADEMA hawaaminiki

u can easily know the hopeless thoughts
 
...Dah, nawahurumia wale watoto wadogo katika shule za mbagala incl St Mary's na wazazi wao saa hii...wapo katika hali gani na mtafaruku huu?
 
salam

kuna mtu amenipigia simu sasa hivi kuwa ghala la kutunzia silaha la jeshi la wananchi nyumbani Tanzania limelipuka.
 
kwani hii ya leo inatofauti na ile ya jana?

maana jana i was so uncomfortable..unajua tena you never know hawa CHADEMA hawaaminiki
Pale Dodoma kuna hospitali nzuri sana (inaitwa Mirembe) GT kama unahitaji tiba waweza kwenda pale utasaidiwa.
 
hata simu za mezani zilikuwa haziendi kabisa
Nimeambiwa hivyo pia tena inasemekana mpaka sasa kuna tatizo la mawasiliano via landline, ati hata mobile communications zilikata! Hii inatokana na hii issue au ni michemsho ya TCRA?
 
Waandishi wa habari waandamizi na wapiga picha tayari wapo Mbagala, huku wahariri wakiendelea kuwasiliana na viongozi wa juu wa Jeshi. Definitely this is going to make headlines.
 
Back
Top Bottom