April '09 Bomb Blasts in Dar (Mbagala) and responses

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Kwa wale mlio Dar,

Kutakuwa na milipuko flani mnaisikia. Ni mabomu ambayo yanalipuka eneo la kambi ya Jeshi Zakhem - Mbagala.

Hii inaweza kupelekea mitikisiko isiyotarajiwa.

Nimefahamishwa ili nitoe tahadhari hii mapema. Nini kinaenedelea? Tutafahamishana
 
Nimewasiliana na wakuu wanaonekana kutojua kinachoendelea... Naelezwa bado mabomu yanalipuka tu
 
Kwa wale mlio Dar,

Kutakuwa na milipuko flani mnaisikia. Ni mabomu ambayo yanalipuka eneo la kambi ya Jeshi Zakhem - Mbagala.

Hii inaweza kupelekea mitikisiko isiyotarajiwa.

Nimefahamishwa ili nitoe tahadhari hii mapema. Nini kinaenedelea? Tutafahamishana

Hakukaliki wa mbagala wote wanakimbia ovyo hapakaliki ....
 
City center kumetokea kishindo kikubwa dakika 5 zilizopita. Tulitaka kutoka mbio maofisini!!! Baadhi ya majengo yamepate ufa
 
Kuna moshi/moto mkubwa unaonekena maeneo ya Mbagala.
 
Jamani wana dar esalaama nikweli kuna tetemeko huko....na kama lipo kuna maafa yoyote?
 
hehehe ndo mnataka vita yaaani trailer tu watu mnakimbia ovyo haya bana....kwa nini kama ni mazoezi wasingefanyia mbali hukoooooo Ruvu kwenye open space?
 
Takriban dakika mbili zilizopita, kumesikika milipuko mikubwa Jijini Dar za milio kama ya bomu au milipuko ya matangi makubwa ya mafuta ikitokea maeneo ya Nyerere rd.
Nikiwa kwenye moja ya maghorofa ya kisasa yaliyojengwa kuhimili milipuko, jengo lilitetemeka na alarm ya bomu ikalia, acha watu waanze kutafutana!.
Mwenye taarifa zaidi, naomba atujuze.
 
ofisi yangu ipo barabara ya mirambo karibu na Umoja House, nikajua Osama anataka kufanya vitu vyake, ukizingatia tupo karibu na ubalozi wa Uingereza. Nikatoka nje ya ofisi kwa spidi kali
 
Kuna mushkeli kwenye kambi moja ya jeshi huko Mbagala. Available information indicates that milipuko imetokea kwenye ghala la silaha-nia ajali (bahati mbaya), so uvamizi wala jambom la kukusudia ingawa kumekuwa na conspiracy theiories ziemshaanza kusambaa mjini.
 
Kwa kweli tumeshtuka sana na tumetoka maofisini. Watu wa Mbagala tujulisheni jamani maana tuna hofu na mashaka
 
Back
Top Bottom