nkongu ndasu
JF-Expert Member
- Jan 19, 2013
- 22,532
- 6,628
Mkuu tafadhali! hawa jamaa kumuunga mkono ama kumvhagua Lowassa wana maana ya kwamba kama CCM ingempitisha Lowassa basi wao wasingekuwa na pingamizi maana ndiye wanayetegemea kuleta mageuzi, sasa tujiulize ni mageuzi gani hayo? Na hawa CHAUMA wameonyesha wazi kwamba sio wamewaunga mkono UKAWA bali Lowassa na hivyo wangemuunga mkono hata kama angechaguliwa na CCM. Ndivyo kisiasa inavyotafsirika.
Kama UKAWA walikuwa na dawa dhidi ya Lowassa na walijiandaa vema dhidi ya Lowassa na mgombea wao ikiwa Lowassa atapitishwa na CCM, basi hizo ndizo sababu zingewafanya wasimchukue Lowassa kwani uchaguzi wa rais unatokana na sifa za mgombea sio Chama kwa ujumla. Mrema alifanya vizuri kwa sababu wananchi walimtazama yeye na sio NCCR na hata Dr. Slaa 2010 kama Chadema ingemsimamisha Mbowe bila shaka matokeo yangekuwa tofauti kabisa na ndio maana CDM wakampitisha Dr.Slaa.
Kwa hiyo unajaribu a Chadema kwa vipi kwani wananchi hawakuiona Chadema wakati wa Dr.Slaa ama Mbowe na kwa nini hawakuichagua ikiwa itikadi na sera zake ni zile zile!. Mkuu hatupo katika majaribisho, na wala hatuna wakati huo kwa sasa isipokuwa tumefungiwa kanya boya tukiamini kuna mbuzi katika gunia.
Hii Chadema itaongoza vipi? kwa hizo ahadi za Lowassa! mtu hatangazi hata sera za Chadema isipokuwa it's all about him, leo anatuhakikishia kwamba Mkataba wa Richmond ulikuwa safi kabisa na kusema ilikuwa kosa kufuatilia kesi hiyo ilitugharimu millioni mia moja na sijui ngapi, wakati leo inatugharimu zaidi ya hicho karibu kila mwezi na umeme bado hautoshelezi!
Huyu kweli ni mtu wa kumpa nafasi kubwa azungumze uongo kwa niaba yenu kwamba haoni kama kulikuwa na makosa yalipofanyika ilihali watu wote tunaamini yalikuwa makosa!. Huyu huyu leo anadai ati alitaka kuuvunja mkataba na kwa ushahidi gani? tumuamini tu leo hii. Richmond - shirika la kitapeli la uchapishaji Houston, owner wake mhindi tumekua naye Gerezani na address ya Rostam iwe mkataba safi kabisa ulosifika ha Obama na Mama Clinton sijui baada ya kuuziwa Symbion! Lini rais wa Marekani akaingilia biashara za mashirika hata kutamka maneno kama hayo!. Huu ni uongo ulopitikliza!
Sisi tunaoishi nchi hizi tunajua fika rais wa nchi hawezi kabisa kusema maneno hayo ktk mikataba ya mashirika isimhusu na kama unakumbuka Waziri mkuu wa Canada Harper alipokuja Dar aliombwa kutusaidia juu ya Mkataba wetu na Barricks! Na akasema yeye hana mamlaka hayo maadam tumeshafunga mkataba tukajadili na wawekezaji! Leo Lowassa anaudanganya Umma kwamba Obama alisifia mitambo ya Richmond na maneno haya anayasema kwa tiketi ya Chadema (UKAWA) mnakubali tu!..
Mnasikitisha sana ndugu zangu, sijui haya mageuzi yenu yanalenga kugeuzwa kwa chapati ili iive pande zote mbili..
Wewe Mkandara uko upande upi sasa?Mkuu Mabaradhuli ni hawa mnaowapokea mkidhani wanaume kumbe mashoga tu..Mtandao ni zaidi ya fikra zenu na mnachoshangilia mimi sikioni kabisa kwa sababu Lowassa hawezi kuwa Chadema ikiwa Chadema ndio wamemfuata! hakuna mtu alowahi kujiunga na CDM kwa kuombwa yeye ajiunge na kuahidiwa nafasi kama ile.. CDM needed Edo sio kinyume. Lowassa ni Mbwa mwitu alovaa ngozi ya kondoo akiwa ndani ya zizi la kondoo ama niseme hivi Lowassa ni sawa na Chatu, mbwa humfuata wenyewe na wakabanwa mbavu na kumezwa, wewe na mimi hatutaijua sababu!.
Miaka 20+ sio swala la CCM kimaadili, hakuna mahala popote yameandikwa hayo waloyafanya kwa miaka hiyo isipokuwa wamegawanyika katika uchumia tumbo kutokana na mvutano wa kama katika kapu nla mvuvi. Kwa miaka zaidi ya 30 walikuwa wote hawa maskini kama sisi wakizeeka na umaskini wao. Toka Mwinyi hadi JK agenda ni swala la watu hao kutokana na Umaskini, kila mmoja wao kachuma kwa wakati wake na hata walipotoka tamaa za utajiri zaidi zikawashika wakaanza kuumizana wenyewe. Hii ni vita baina ya Fisi na Simba, wewe nyumbu unafurahia nini na kusema bora ya Fisi kuliko Simba?
Katika hali tulofikia mimi sina Upande in fact sitapiga kura na hata kama ningekuwa na kadi ya kupiga kura ingenipa shida kuchagua mbora kati ya Simba na Fisi maana Wadanganyika ni kama Nyumbu malishoni. Kwa hiyo sitazami kilicho bora kwangu mimi bali kwa wananchi wenyewe na ndio somo langu kuu. It's not about me but fellow Tanzanians!Wewe Mkandara uko upande upi sasa?
Kuunga mkono mabadiliko au tuendelee kuipa CCM miaka kumi mingine?
Nakusoma sana, lakini hautoi alternative zaidi ya kuwapinga tu UKAWA na mkakati wao huu waliokuja nao!
Please tell us. Unajua nyie ni wachambuzi wetu wazuri wa mambo ya kisiasa za Tanzania na binafsi huwa nafuatilia sana mijadala yenu na akina Nguruvi3, Mchambuzi, Mag3, Waberoya and others kule jukwaa la Great Thinkers na hujifunza mengi sana.
Lakini huku mbona kama una piga soga tu badala ya kukosoa na kutoa altenative as a way forward
Pls sometimes muhamishie mijadala ya kina ya hoja ya kule GT huku JS ili vijana wajifunze kitu.
Mimi sidhani kama Zitto ataweza kuwa rais wa Tanzania mwaka 2020 maana itachukua miaka mingi kwa ACT kujenga imani mpya za watu kutoka kuishi kwa mazoea na naweza sema kwamba pengine January Makamba is our next President! Na Usishangae kabisa kwani kanishangaza sana katika matokeo ya mwaka huu ndani ya CC. Nje ya CCM bado kabisa ushindi kupatikana hilo nakuhakikishia...
Mkuu tafadhali! hawa jamaa kumuunga mkono ama kumvhagua Lowassa wana maana ya kwamba kama CCM ingempitisha Lowassa basi wao wasingekuwa na pingamizi maana ndiye wanayetegemea kuleta mageuzi, sasa tujiulize ni mageuzi gani hayo? Na hawa CHAUMA wameonyesha wazi kwamba sio wamewaunga mkono UKAWA bali Lowassa na hivyo wangemuunga mkono hata kama angechaguliwa na CCM. Ndivyo kisiasa inavyotafsirika.
Kama UKAWA walikuwa na dawa dhidi ya Lowassa na walijiandaa vema dhidi ya Lowassa na mgombea wao ikiwa Lowassa atapitishwa na CCM, basi hizo ndizo sababu zingewafanya wasimchukue Lowassa kwani uchaguzi wa rais unatokana na sifa za mgombea sio Chama kwa ujumla. Mrema alifanya vizuri kwa sababu wananchi walimtazama yeye na sio NCCR na hata Dr. Slaa 2010 kama Chadema ingemsimamisha Mbowe bila shaka matokeo yangekuwa tofauti kabisa na ndio maana CDM wakampitisha Dr.Slaa.
Kwa hiyo unajaribu a Chadema kwa vipi kwani wananchi hawakuiona Chadema wakati wa Dr.Slaa ama Mbowe na kwa nini hawakuichagua ikiwa itikadi na sera zake ni zile zile!. Mkuu hatupo katika majaribisho, na wala hatuna wakati huo kwa sasa isipokuwa tumefungiwa kanya boya tukiamini kuna mbuzi katika gunia.
Hii Chadema itaongoza vipi? kwa hizo ahadi za Lowassa! mtu hatangazi hata sera za Chadema isipokuwa it's all about him, leo anatuhakikishia kwamba Mkataba wa Richmond ulikuwa safi kabisa na kusema ilikuwa kosa kufuatilia kesi hiyo ilitugharimu millioni mia moja na sijui ngapi, wakati leo inatugharimu zaidi ya hicho karibu kila mwezi na umeme bado hautoshelezi!
Huyu kweli ni mtu wa kumpa nafasi kubwa azungumze uongo kwa niaba yenu kwamba haoni kama kulikuwa na makosa yalipofanyika ilihali watu wote tunaamini yalikuwa makosa!. Huyu huyu leo anadai ati alitaka kuuvunja mkataba na kwa ushahidi gani? tumuamini tu leo hii. Richmond - shirika la kitapeli la uchapishaji Houston, owner wake mhindi tumekua naye Gerezani na address ya Rostam iwe mkataba safi kabisa ulosifika ha Obama na Mama Clinton sijui baada ya kuuziwa Symbion! Lini rais wa Marekani akaingilia biashara za mashirika hata kutamka maneno kama hayo!. Huu ni uongo ulopitikliza!
Sisi tunaoishi nchi hizi tunajua fika rais wa nchi hawezi kabisa kusema maneno hayo ktk mikataba ya mashirika isimhusu na kama unakumbuka Waziri mkuu wa Canada Harper alipokuja Dar aliombwa kutusaidia juu ya Mkataba wetu na Barricks! Na akasema yeye hana mamlaka hayo maadam tumeshafunga mkataba tukajadili na wawekezaji! Leo Lowassa anaudanganya Umma kwamba Obama alisifia mitambo ya Richmond na maneno haya anayasema kwa tiketi ya Chadema (UKAWA) mnakubali tu!..
Mnasikitisha sana ndugu zangu, sijui haya mageuzi yenu yanalenga kugeuzwa kwa chapati ili iive pande zote mbili..
Wanachama wa UKAWA ni wale wananchi wa mijini na vijijini waliopigika kwa sera za CCM zilizoshindwa kuwaboreshea maisha yao, hivyo wakajikusanya chini ya UKAWA ili kujaribu kutafuta ahueni kwa kuiondoa CCM madarakani sawa na walalahoi wa Marekani walivyomchagua Obama na democrat wakijaribu kutafuta nafuu ya maisha yao. Rungwe na wenzako mnaogombea urais kupitia vyama ambavyo havina hata diwani mmoja nchini mnajua kuwa hamtashinda, na sisi wananchi tunawaona nyie kama watu wenye nia ya kuisadia CCM ili iendelee kutubana wananchi kwa kuzigawana kura za upinzani wakati wa uchaguzi. Tunakufahamu kuwa wewe ni mkurugenzi wa bahari motors pale Mwananyamala, hivyo sio mlalahoi kama sisi. Lakini rasilimali ya watu wanyonge ni umoja wao, tutahamasishana wapenda UKAWA wote ili kuzisusia biashara zako zote na za wenzako sokoni ili muwe walalahoi kama sisi, lambda mtaelewa mateso yetu na juhudi halali tunazozichukua katika kujitafutia nafuu.