ManiTek TV
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 410
- 159
Upungufu mkubwa unaozungumziwa kwa simu ya iPhone kwa sasa ni udogo wa skrini, safiri pamoja nasi katika makala hii kwani Apple wamepata hakimiliki yenye miujiza mingi mno ambayo huenda ikawa ndio suluhisho la udogo wa skrini ya iPhone bila ya simu kuwa kubwa. Kwa mujibu wa mtandao wa The Register hakimiliki hiyo ni nambari 20130076612 ambayo imesajiliwa jana kwenye ofisi za US Patent and Trademark huko Marekani.
Ajabu ya hakimiliki hiyo ni kwamba simu nzima itakuwa inazungukwa na skrini, yaani skrini itazunguka mbele na nyuma ya simu, hii maana yake iwapo iPhone itabaki kuwa na skrini ya inchi nne, jumla ya ukubwa wa skrini utakuwa inchi nane kwa vile skrini itakuwa mbele na nyuma. Teknolojia hiyo inahusiana na skrini mregezo zenye kupinda aina ya Amoled (Flexible screen), tukumbuke kwamba wakati Samsung bado wako kwenye utafiti juu ya namna ya kutumia skrini hizi, Apple wameshawapiga bao la kisigino.
Mchoro wa hakimiliki hiyo unaonyesha kuwa simu zitakuwa na umbile la skrini mbinuko mbele na nyuma. Katika haki miliki hii Apple wameingiza teknolojia ambayo kuna sensa zenye uwezo wa kutambua sura ya mtuamiaji. Jambo jengine ambalo sio la kawaida katika haki miliki hii hi kuwa simu inaonekana kuwa na skrini mbili zilizopandiana moja juu ya mwenziwe, ya juu ikiwa ni yenye kuonyesha (see through) kisha kwa pamoja zinaweza kutengeneza taswira ya 3D, hii maana yake ni kwamba teknolojia hii sio tu haitahitaji kuvaa miwani kupata taswira ya 3D bali pia haitalazimu kuangalia kutoka pembe (angle) fulani, tofauti na ile iliyotumika kwenye Nintendo 3DS ambapo mtumiaji anahitajika kuwa katika pembe (angle) fulani kuweza kuipata taswira sahihi ya 3D.
Mbali na skrini zilizopandiana kuweza kuonyesha 3D pia skrini hizo zinaweza kushirikiana kutoa taarifa au taswira tofauti, mathalani skrini moja inaweza ikawa inaonyesha video na nyingine inatoa maandishi yanayoendana na video ile. Pia katika haki miliki hiyo Apple wameonyesha gajeti zenye maumbile tofauti likiwemo umbile la kijipipa fulani hivi, haikuelezwa hiyo itakuwa ni gajeti ya aina gani, na upo uwezekano kuwa gajeti hizo zitakuwa ni za kukunja na kukunjua.
Teknolojia hii iko mbele mno kiwakati, bado hatudhani kwamba itatumika kwenye iPhone 6 kwa vile betri itakayohitajika kwenye skrini inayozunguka gajeti nzima inahitaji kuwa na nguvu kubwa mno. Hivyo hii huenda tukaiona kwenye iPhone 8 kwenda mbele, isipokuwa iwapo patatokea mapinduzi makubwa kwenye nguvu ya cells za betri. Hii si haki miliki ya kwanza ya kampuni ya Apple inayohusiana na skrini mregezo. Apple hivi karibuni pia walipata haki miliki yenye kutumia skrini za aina hii katika saa ambapo skrini hiyo huzunguka mkono mithili ya saa na mkanda wake, hii imepelekea wanateknolojia wengi kutabiri kutolewa kwa iWatch mwaka huu.
CHANZO: GAJETEK HABARI: Apple Yapata Haki Miliki ya Ajabu ya iPhone