Apple vs FBI; Maxence Melo vs DCI

mshumbullah

Member
Jan 29, 2015
34
95
Kuna watu bado hawajapata usahihi wa anachokisimamia Maxence Melo hasa kile ambacho leo kimebainika kuwa ndicho kiini cha shtaka lake la kwanza na la pili. Ili kuwasaidia kupata mwanga, nimejaribu kutafsiri kesi ya mapambano ya kisheria kati ya Kampuni namba moja kwa teknolojia ya mawasiliano duniani, Apple dhidi ya Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI).

Nisimalize uondo, jisomee na kisha jipe jibu kama kweli Maxence ndiye mwenye jukumu la kuthibitisha uhalifu na kama kweli jeshi la polisi lina haki ya kudai na kupewa faragha za wateja wa @JamiiForums.com

Endelea Hapa Chini.....

2fd30af1-c2bd-4417-9110-e0d792319a2f.jpg


Mapambano ya Kisheria kati ya Taasisi ya Uchunguzi nchini Marekani(FBI) na Kampuni ya uzalishaji wa vifaa vya kieletroniki zikiwemo simu za mkononi Apple yamefikia mwisho.

FBI ilitaka kupatiwa taarifa za siri zilizokuwa kwenye simu ya muuaji, Syed Farook aliyewaua kwa risasi watu 14 katika eneo la San Bernardino Desemba mwaka jana.

Katika sakata hilo Jaji aliitaka Kampuni ya Apple kuipatia FBI na mamlaka zote ushirikiano wa kutosha, ambapo Apple walitakiwa kufumua mfumo unaoifunga simu baada ya kufanya majaribio 10 ya kuingiza nywila(password) bila mafanikio.

Apple waligomea agizo hilo la Mahakama na ndipo mabishano ya kisheria yalipoanzia.

Mkurugenzi Mtendaji wa Apple, Tim Cook alisema agizo hilo halikubaliki na kama wakiwapatia uwezo wa kuiingilia simu hiyo ya Syed Farook hakuna jinsi FBI watashindwa kuziingilia simu nyingine zote za wateja wao. FBI waliendelea kushikilia msimamo wao wa kutopatiwa taarifa hizo.


KWA NINI SUALA HILI LILILETA MABISHANO MAKALI

Kesi hii iliibua mjadala mkubwa kuhusu usiri/usalama wa taarifa za watu wanaotumia mitandao au vifaa vya kieletroniki dhidi ya Serikali pale zinapohitajika.

Taasisi zinazosimamia sheria zinasema kwamba njia wanazotumia makampuni ya teknolojia kulinda taarifa za wateja wao(encrpytion) zinapelekea kazi zao kuwa ngumu hasa kwenye mapambano dhidi ya ugaidi.

Lakini makampuni ya teknolojia yanashikila msimamo wao kuwa, njia wanazotumia kulinda taarifa(encryption) ni kwa ajili ya kupambana na wadukuzi(Hackers) na kulinda taarifa za wateja wao.

Mjadala kuhusu ulinzi wa taarifa za watumiaji wa mitandao na vifaa vya kieletroniki ulichochewa baada ya Mwanausalama Edward Snowden kuibuka na kuonyesha jinsi serikali inavyodukua na kufuatilia mawasiliano ya watu mitandaoni kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi.

NINI KILITOKEA

Baada ya mapambano hayo ya Apple na FBI, hatimaye serikali ya Marekani iliamua kutumia mtu wa tatu(Third Party) ili aweze kuingilia simu ya muuaji Syed Farouk na kupata taarifa. Taarifa ambazo sio rasmi zinasema kuwa kampuni ya Israel Cellebrite ndio imepewa kazi hiyo ya kuiingilia simu ya Syed Farouk.

Serikali ya Marekani imeshaitaka mahakama kuitupilia mbali kesi hiyo dhidi ya Apple na FBI imekataa kusema lolote kuhusu jinsi gani wameiingilia simu hiyo.

Apple imesema kuwa itaendelea kushirikiana na FBI pamoja taasisi zote zinazosimamia sheria katika uchunguzi na wataendelea kuongeza ulinzi katika bidhaa zao ili kulinda wateja wake dhidi ya matishio yote.
=====================================

The legal tussle between Apple and the U.S. Federal Bureau of Investigation (FBI) over access to the iPhone used by a shooter in last year's San Bernardino attacks is now over after authorities announced they had accessed the device.

But the larger debate between technology firms and law enforcement authorities over data privacy and access remains. CNBC explains the case and why it was such a big deal.

What was the battle over?

Last month, a federal judge asked Apple to help the FBI unlock an iPhone belonging to Syed Farook, who was responsible for the shootings in San Bernardino in December which left 14 people dead.

The judge asked Apple to provide "reasonable technical assistance" to the U.S. authorities, which would require the technology giant to overhaul the system that disables the phone after 10 unsuccessful password attempts. Once this feature kicks in, all the data on the phone is inaccessible. Apple declined to help the FBI.

At the time, Apple chief executive Tim Cook called the order "chilling"and said that it would require writing new software that would be "a master key, capable of opening hundreds of millions of locks". Cook's argument was that if the FBI could access this iPhone, nothing would stop them from doing it to many others.

Law enforcement authorities insisted that it was a one-off request. As a result the case went to court.

Why was it controversial?

The case marked one of the highest-profile clashes in the debate over encryption and data privacy between the government and a technology company.

Law enforcement authorities say that encryption used by the likes of Apple makes it harder for them to solve cases and stop terrorist attacks

Technology firms have kicked back, saying that encryption is key to protecting user data from hackers.

Data privacy has been a sensitive topic particularly after revelations by former National Security Agency contractor Edward Snowden about the extent of the government's surveillance activities.

What was the outcome?

A hearing set for last week was postponed after the government said that it had found a third-party that was able to unlock the iPhone. Reports suggested that it was Israeli firm Cellebrite. This was never confirmed by the company.

On Monday, the Department of Justice said it had managed to access the data on the iPhone in question and asked the judge to drop the case. The FBI said in a statement that it could not comment on the "technical aspects" of how the iPhone was unlocked nor the third-party that was involved.

Apple said that it "will continue to help law enforcement with their investigations, as we have done all along, and we will continue to increase the security of our products as the threats and attacks on our data".


Who won?

It appears to be the best of a bad situation.

Apple stuck to its guns on defending civil liberties.

"From the beginning, we objected to the FBI's demand that Apple build a backdoor into the iPhone because we believed it was wrong and would set a dangerous precedent. As a result of the government's dismissal, neither of these occurred," Apple said in a statement following the dropping of the case.

The FBI got their desire result – getting access to Farook's iPhone.

Still, there are questions about the effectiveness of Apple's security.


Is this the end of it all?

Probably not. Rumblings between technology companies and the government are likely to continue.

Last month, several news outlets revealed that there have been numerous requests from law enforcement agencies across the country for Apple to help unlock other iPhones.

Apple will want to know how the FBI got into the iPhone in order for it to patch up any vulnerabilities in its software. The iPhone maker is likely to continue bolstering security in its software and devices.


Source: Apple vs FBI: All you need to know
 

izzo

JF-Expert Member
May 31, 2015
2,815
2,000
Katika yote uliyosema mwisho tumekuja kuona serikali imeshinda na wamepata walichotaka nje ya mahakama na kwa njia wanazojua wenyewe na sijawai kusikia mtu au taasisi yeyote dunian ikashindana na serikali na ikashinda cha msing ni kuwa makini na kile unachokisema ,kusikia au kukiandika
 

Ericus Kimasha

Verified Member
Oct 27, 2006
487
250
Katika yote uliyosema mwisho tumekuja kuona serikali imeshinda na wamepata walichotaka nje ya mahakama na kwa njia wanazojua wenyewe na sijawai kusikia mtu au taasisi yeyote dunian ikashindana na serikali na ikashinda cha msing ni kuwa makini na kile ukisemacho na kukiandikacho
Nisaidie kujua, Serikali ilifanikiwa/shinda kwa Apple kutekeleza ilichotaka au ilitafuta njia mbadala? Hilo tu!
 

Freeland

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
14,492
2,000
walipaswa wawe na wataalamu wa kuweza kupenya na sio kusumbua mmiliki
 

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
10,037
2,000
Katika yote uliyosema mwisho tumekuja kuona serikali imeshinda na wamepata walichotaka nje ya mahakama na kwa njia wanazojua wenyewe na sijawai kusikia mtu au taasisi yeyote dunian ikashindana na serikali na ikashinda cha msing ni kuwa makini na kile ukisemacho na kukiandikacho
Bila shaka umekurupuka pitia maelezo upya tena wao kesi yao ni ugaidi.....

Alafu hapa kesi za kuwasema wezi eti police isaidiwe ...

Upuuzi mtupu.....
 

izzo

JF-Expert Member
May 31, 2015
2,815
2,000
Nisaidie kujua, Serikali ilifanikiwa/shinda kwa Apple kutekeleza ilichotaka au ilitafuta njia mbadala? Hilo tu!
Kwanza unatakiwa kujua kukataa kutoa ushirikiano kwa vombo vya dora ni kosa tena sio Tanzania tu bali ni dunia nzima pili Apple walikubali kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dora na Taasisi zake na pia Apple alishindwa kesi na kukata rufaa na maamuzi ya mahakama yalikuwa Apple ampatie ushirikiano FBI juu ya kufungua simu ya yule Gaidi sasa linapokuja swala la usalama au Tishio la kiusalama wa nchi ni lazima hatua zichukuliwe haraka so wakat kesi ikiendelea mahakamani tayali serikali ilikuwa imeshatafuta njia nyingne ya kupata kile inachotaka na baada ya kupata serikali yenyewe ikaondoa shitaka mahakamani so jambo ili linatufundisha nini??? tunaomba sana ucku na mchana serikali yetu isije chukua maamuzi kama waliochukua serikali ya US juu ya kupata kile wnachokitaka maana wengi wetu wa jukwaa la siasa tutaishia kwenye majengo ya serikali
 

Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Nov 10, 2016
2,968
2,000
Katika yote uliyosema mwisho tumekuja kuona serikali imeshinda na wamepata walichotaka nje ya mahakama na kwa njia wanazojua wenyewe na sijawai kusikia mtu au taasisi yeyote dunian ikashindana na serikali na ikashinda cha msing ni kuwa makini na kile ukisemacho na kukiandikacho
Wewe toka sakata la Melo post zako ni kama unafurahia hivi.
 

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Mar 1, 2016
4,641
2,000
I think there is a point, security is number one priority, no serious state can dare not to have such kind of "imposed" privilege. It is important to have citizens understand the essence and the state must use such imposed privilege wisely and judiciously. So all state machinery for administration of justice should step up and clear the bad air to win back the trust of the citizens.
 

General Stalin

JF-Expert Member
Mar 6, 2014
627
500
Na lazima serikali ipewe taarifa za watumiaji wote wa mitandao ndivyo sivyo

Melo wape polisi wanachotaka maisha yaendelee vinginevyo forum itafungwa kabisa
 

izzo

JF-Expert Member
May 31, 2015
2,815
2,000
Wewe toka sakata la Melo post zako ni kama unafurahia hivi.
Nitakuwa ni mpuuzi na nisiye na fadhila kama nitafurahia jambo kama hili na kama itasibitika nafurahia basi Mungu anihukumu tatizo inawezekana tukawa tofauti kimawazo juu ya kukabiliana na Tatizo la Max kumbuka uchungu au simanzi ni moyo ndo unafeel si mikono, masikio au midomo
 

jimmyfoxxgongo

JF-Expert Member
Jan 23, 2013
5,363
2,000
Kwanza unatakiwa kujua kukataa kutoa ushirikiano kwa vombo vya dora ni kosa tena sio Tanzania tu bali ni dunia nzima pili Apple walikubali kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dora na Taasisi zake na pia Apple alishindwa kesi na kukata rufaa na maamuzi ya mahakama yalikuwa Apple ampatie ushirikiano FBI juu ya kufungua simu ya yule Gaidi sasa linapokuja swala la muda na swala la usalama au Tishio la kiusalama la nchi ni lazima hatua zichukuliwe haraka so wakat kesi ikiendelea mahakamani tayali serikali ilikuwa imeshatafuta njia nyingne ya kupata kile inachotaka na baada ya kupata serikali yenyewe ikaondoa shitaka mahakamani so jambo ili linatufundisha nini??? tunaomba sana ucku na mchana serikali yetu isije chukua maamuzi kama waliochukua serikali ya US juu ya kupata kile wnachokitaka maana wengi wetu wa jukwaa la siasa tutaishia kwenye majengo ya serikali
Lumumba
 

bne

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
1,574
2,000
Kwanza unatakiwa kujua kukataa kutoa ushirikiano kwa vombo vya dora ni kosa tena sio Tanzania tu bali ni dunia nzima pili Apple walikubali kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dora na Taasisi zake na pia Apple alishindwa kesi na kukata rufaa na maamuzi ya mahakama yalikuwa Apple ampatie ushirikiano FBI juu ya kufungua simu ya yule Gaidi sasa linapokuja swala la muda na swala la usalama au Tishio la kiusalama la nchi ni lazima hatua zichukuliwe haraka so wakat kesi ikiendelea mahakamani tayali serikali ilikuwa imeshatafuta njia nyingne ya kupata kile inachotaka na baada ya kupata serikali yenyewe ikaondoa shitaka mahakamani so jambo ili linatufundisha nini??? tunaomba sana ucku na mchana serikali yetu isije chukua maamuzi kama waliochukua serikali ya US juu ya kupata kile wnachokitaka maana wengi wetu wa jukwaa la siasa tutaishia kwenye majengo ya serikali
Hapana hapa ni kwamba apple alishinda kuwa jukumu LA kuingilia simu hiyo na kupata habari ni jukumu LA FBI ndio maana walitafuta mtu wa tatu na baada ya kujua kuwa hawatashinda wakaamua kuondoa kesi.
Kama wangekua na uhakika wa ushindi wangeendelea kutafuta hiyo haki kwani huo sio mwisho wa matukio
 

Ericus Kimasha

Verified Member
Oct 27, 2006
487
250
Kwanza unatakiwa kujua kukataa kutoa ushirikiano kwa vombo vya dora ni kosa tena sio Tanzania tu bali ni dunia nzima pili Apple walikubali kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dora na Taasisi zake ...
Sidhani kama @Maxecence Melo au Jamii Media wamegoma kutoa ushirikiano. Ushirikiano daima una mipaka na hasa kwenye Taasisi. Ushirikiano unapokwenda mbali zaidi na kutakiwa ushiriki kwenda kinyume na Sheria, Kanuni na Miongozo ambayo mmejiwekea kuendesha shughuli zenu kulingana na Sheria Mama ya Nchi (Katiba), utakuwa tayari kutoa ushirikiano? Suala la consumer protection lipo katika kila huduma. Daktari hawezi kutoa faragha zako eti kisa ushirikiano! the same for ISPs, Telecomms etc. Pia kuna extreme moja tunapaswa kuiangalia. Je, taarifa zilizotolewa na hao ambao faragha zao zinatakiwa zilizkuwa zinahatarisha usalama wa nchi? Katika mashtaka yote matatu aliyosomewa Maxence hilo halimo!.
 

izzo

JF-Expert Member
May 31, 2015
2,815
2,000
Sidhani kama @Maxecence Melo au Jamii Media wamegoma kutoa ushirikiano. Ushirikiano daima una mipaka na hasa kwenye Taasisi. Ushirikiano unapokwenda mbali zaidi na kutakiwa ushiriki kwenda kinyume na Sheria, Kanuni na Miongozo ambayo mmejiwekea kuendesha shughuli zenu kulingana na Sheria Mama ya Nchi (Katiba), utakuwa tayari kutoa ushirikiano? Suala la consumer protection lipo katika kila huduma. Daktari hawezi kutoa faragha zako eti kisa ushirikiano! the same for ISPs, Telecomms etc. Pia kuna extreme moja tunapaswa kuiangalia. Je, taarifa zilizotolewa na hao ambao faragha zao zinatakiwa zilizkuwa zinahatarisha usalama wa nchi? Katika mashtaka yote matatu aliyosomewa Maxence hilo halimo!.
kiongozi moja ya shitaka la kiongoz Max ni Maxence Melo, anatuhumiwa kuzuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi chini ya kifungu cha 22 cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao
pili unasema Dr, ISPs, Telecomms linapotokea tatizo au wanapotakiwa kutoa taarifa na vyombo vya dora au taasisi zinazohusika na jambo ilo wanatoa taariifa za wateja wao ni mala ngapi tumesikia watu taarifa za miamala yao ya bank ikijulikana na ikitajwa unazani taarifa hzo anatoa nani??? kulikuw na kashfa ya 'Tegeta escrow tulitajiwa mpaka ela zilzokuwa zinabebwa kwnye mifuko ya rambo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom