Apple vs FBI; Maxence Melo vs DCI

Apple vs FBI; Maxence Melo vs DCI

Katika yote uliyosema mwisho tumekuja kuona serikali imeshinda na wamepata walichotaka nje ya mahakama na kwa njia wanazojua wenyewe na sijawai kusikia mtu au taasisi yeyote dunian ikashindana na serikali na ikashinda cha msing ni kuwa makini na kile ukisemacho na kukiandikacho
Ameshindwa kuhitimisha kwa kusema ukweli kuwa FBI waliweza kuifungua ile simu bila msaada wa Apple ndio maana wakaachana na kesi.

Hii ina maana hata sisi watumiaji wa simu tuwe makini na matumizi yake. Akina Melo wanaweza wasitoe taarifa, lakini bado Serikali ikapata namna nyingine ya kutufikia kama FBI walivyofanya.
 
Wewe ni (...) kabisa, kesi iko mahakamani.
Kwa maslahi mapana ya JamiiForums.com na kesi iliyopo mbele yetu naomba ufute na kuondoa neno liliachwa kwenye mabano. Pia dhamiria kutotumia lugha ya namna hiyo tena. Naomba...
 
kutoa mawasiliano ya mtu ni sawa na kumfungia mtu kamera bafuni bila mwenyewe kujua.....
 
kutoa mawasiliano ya mtu ni sawa na kumfungia mtu kamera bafuni bila mwenyewe kujua.....
Na wakati mwingne Camera zinaitajika kufungwa pia kwa ajili ya usalama wa huyo mtu .
 
Sidhani kama @Maxecence Melo au Jamii Media wamegoma kutoa ushirikiano. Ushirikiano daima una mipaka na hasa kwenye Taasisi. Ushirikiano unapokwenda mbali zaidi na kutakiwa ushiriki kwenda kinyume na Sheria, Kanuni na Miongozo ambayo mmejiwekea kuendesha shughuli zenu kulingana na Sheria Mama ya Nchi (Katiba), utakuwa tayari kutoa ushirikiano? Suala la consumer protection lipo katika kila huduma. Daktari hawezi kutoa faragha zako eti kisa ushirikiano! the same for ISPs, Telecomms etc. Pia kuna extreme moja tunapaswa kuiangalia. Je, taarifa zilizotolewa na hao ambao faragha zao zinatakiwa zilizkuwa zinahatarisha usalama wa nchi? Katika mashtaka yote matatu aliyosomewa Maxence hilo halimo!.
wewe sidhani kama una akili nzuri,hayo makampuni ya simu sheria inawataka kutoa taarifa za wateja wao endapo serikali itakua inazihitaji kwa sababu za kiusalama,same concept applies kwa madaktari,madaktari nao inapobidi kutoa taarifa kuwahusu wagonjwa wao kwa serikali wanatoa kwan hujawah kusikia madaktari wanatoa ushahidi mahakamani?
 
Nisaidie kujua, Serikali ilifanikiwa/shinda kwa Apple kutekeleza ilichotaka au ilitafuta njia mbadala? Hilo tu!

Tatizo hasomi bali mhemko.
Anajua iliwalazimu kutumia kiasi gani cha Dola kufanikiwa?
Na bado issue inaendelea .


Lawsuit against the FBI

On September 16, the Associated Press, Vice Media, and Gannett filed a joint lawsuit against the FBI, seeking information on how the agency was able to unlock Farook's iPhone. They also sought for information on the amount of money the federal government paid for the unlocking to commence, and claimed that "there is no lawful basis" for the agency to keep their records on the matter sealed.[112]
 
wewe sidhani kama una akili nzuri,hayo makampuni ya simu sheria inawataka kutoa taarifa za wateja wao endapo serikali itakua inazihitaji kwa sababu za kiusalama,same concept applies kwa madaktari,madaktari nao inapobidi kutoa taarifa kuwahusu wagonjwa wao kwa serikali wanatoa kwan hujawah kusikia madaktari wanatoa ushahidi mahakamani?

Uliposoma, hii sehemu umeisoma vema na kuielewa?
"Pia kuna extreme moja tunapaswa kuiangalia. Je, taarifa zilizotolewa na hao ambao faragha zao zinatakiwa zilizkuwa zinahatarisha usalama wa nchi? Katika mashtaka yote matatu aliyosomewa Maxence hilo halimo!"
 
Kama vile simsomi
Mkuu hatuwezi wote kulia au kulalamika tu tunaitaji solution si emotion kwani siku zote solution ndio kitu kwenye kubeba masilai ya wengi si emotion na pia sku zote watu wenye akili uambiana ukweli juu ya hatari iliyombele yao si kuleta hisia au kufalijiana leo emotion azitatatua Tatizo la kiongozi Max bali solution ndo itatatua tatizo la Max na wengine wote watakao fata baada ya yeye na solution ni kupiga kelele na kupaza sauti juu ya sheria mbovu ya makosa ya mtandao na sheria ya habari kwani hz ndo chanzo cha matatizo na kuakikisha JF Rules zinafwatwa si mtu kuleta taarifa za uongo na uchochezi kumbuka hakuna Taifa au serikali yeyote duniani inaweza kucheza na usalama na utulivu wa nchi kumbuka information is power. Giving people the knowledge to understand na JF ndo imebaki ni soure pekee yenye kuaminiwa na watu wa kada na rika mbalimbali
 
Katika yote uliyosema mwisho tumekuja kuona serikali imeshinda na wamepata walichotaka nje ya mahakama na kwa njia wanazojua wenyewe na sijawai kusikia mtu au taasisi yeyote dunian ikashindana na serikali na ikashinda cha msing ni kuwa makini na kile unachokisema ,kusikia au kukiandika
Walifanikiwa kwa kutumia third party sio apple. Km police wanahitaji hizo taarifa na wao watumie third party km fbi.
 
Juzijuzi polisi UK walitaka data kwenye simu ya mtu,wapate ushahidi-walijua hawawezi kupata wanayoyataka sababu Apple hawatatoa ushirikiano-jamaa aliviziwa kwa siku 3-kuingiza pin tu akavamiwa,screen ikachezewa ili simu isi lock wakapakua kila walichotaka-ushahidi jamaa alifungwa miaka 6
 
Walifanikiwa kwa kutumia third party sio apple. Km police wanahitaji hizo taarifa na wao watumie third party km fbi.
Zipo sababu za wao kutumia third party na kumbuka kesi ilikuwa mahakamani na kesi zile zinazohusu maswala ya kikatiba uchukua muda mrefu na pia hata kama inatokea umeshindwa kuna option ya kukata rufaa na pia unatakiwa kujua swala la National security au Threat yeyote kwa Taifa siku zote hatua uchukuliwa mapema kama ni kulinda,kuzuia au kushambulia sisi sidhani kama kuna haja ya kufikia huko cha muhimu ni kuja na solution bora ya JF,members na stuff wa jf tuwe safe na tuendelee kutoa maoni na mitazamo yetu bila ya kuvunja sheria au kuleta sintofahamu yeyote kwa tutoa taarifa za uongo au uchochezi
 
Kwanza unatakiwa kujua kukataa kutoa ushirikiano kwa vombo vya dora ni kosa tena sio Tanzania tu bali ni dunia nzima pili Apple walikubali kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dora na Taasisi zake na pia Apple alishindwa kesi na kukata rufaa na maamuzi ya mahakama yalikuwa Apple ampatie ushirikiano FBI juu ya kufungua simu ya yule Gaidi sasa linapokuja swala la usalama au Tishio la kiusalama wa nchi ni lazima hatua zichukuliwe haraka so wakat kesi ikiendelea mahakamani tayali serikali ilikuwa imeshatafuta njia nyingne ya kupata kile inachotaka na baada ya kupata serikali yenyewe ikaondoa shitaka mahakamani so jambo ili linatufundisha nini??? tunaomba sana ucku na mchana serikali yetu isije chukua maamuzi kama waliochukua serikali ya US juu ya kupata kile wnachokitaka maana wengi wetu wa jukwaa la siasa tutaishia kwenye majengo ya serikali
Kuna posts humu JF zimetishia úsalama wa nchi yangu pendwa Tanzania?
 
Hapana hapa ni kwamba apple alishinda kuwa jukumu LA kuingilia simu hiyo na kupata habari ni jukumu LA FBI ndio maana walitafuta mtu wa tatu na baada ya kujua kuwa hawatashinda wakaamua kuondoa kesi.
Kama wangekua na uhakika wa ushindi wangeendelea kutafuta hiyo haki kwani huo sio mwisho wa matukio
huwezi kusema apple walishinda kesi wakati kesi haikufika mwisho.. kwanza mara ya kwanza walishinda FBI na federal judge aliwaamuru FBI kutoa technical assistance pale wanapohitajika.

waliona ni kupoteza muda na rasilimali kuendesha kesi ambayo tayari washapata suluhisho. {mfano, wewe unanidai pesa mimi na ukapeleka kesi mahakamani, atokee mtu kama rugemalira aseme anakulipa hela yote unayonidai pamoja na fidia, wewe utaendelea na kesi ya kunidai mimi mahakamani au utaachana nayo tu?? na kama ukiamua kuachana nayo tafsiri yake itakuwa kwamba uliona ungeshindwa??}

Na mpka sasa, FBI wanauwezo wa kuangalia kila kitu katika simu yako hiyo ya iphone.
 
Back
Top Bottom