Apple iPhone X goes on sale today.

kumbe unalinganisha simu? hukusema toka mwanzo?

binafsi mimi simu bora kabisa duniani kwa sasa ni samsung galaxy s6 active. . tuanze na zako then nitamalizia zangu
nayalist
-battery
-perfomance
-display
-camera
-build

1. simu yenye quad HD inayokaa na chaji zaidi. (gsmarena)

compare na iphone x


hivyo mkuu ukiangalia kwenye ukaaji chaji haina mjadala kila idara active ipo juu kuanzia standby, call time, browsing hadi video playback.

2. build quality
bila kupepesa macho active ipo juu sababu ni rugged phone utapata vitu kama
-water proof
-shock proof
-best build quality na imara inayovumilia mianguko, simu kama hii hata cover haihitaji


3. display
zote ni quad HD na on paper ya iphone x ni nzuri ila haiwezi fanya haya hivyo anyday anytime nitachagua ya active.
-hakuna themes wala black mode kwenye ios, ukiwa na kioo cha oled rangi nyeusi ni nzuri sana, najua kuna invert mode, ila invert sio black mode. utasave charge na themes nyeusi kwenye amoled ya active. (serious 2017 ios haina blackmode? karibu zama za mawe)
-Hakuna VR- tunajua display inakula sana charge na lengo kubwa la kuwa na display yenye resolution kubwa ni kuangalia video za 3d au video za 360, ila ios na iphones kwa ujumla hazikubali haya mambo hivyo resolution kubwa ni useless kwao, nikiwa na s6 active yangu navuta tu headset ya VR au natengeneza mwenyewe (rahisi tu) kisha naangalia zangu 3d kiulaini.


4.perfomance
again on paper iphone x ni monster ina cpu kali, almost inai double nguvu s6 active, ila in reality ni joka la kibisa haling'ati, unaweza nipa matumizi makubwa ya ios yanayohitaji powerfull cpu? kwenye android s6 active unafanya haya
-ndio simu ya kwanza ku emulate dolphin na kucheza games za nintendo wii na gamecube, games kali sana huwezi fananisha quality yake na games za simu
-utafanya pia emulation nyengine kama vile kurun visoftware vidogo vidogo vya windows na linux distro.
-unaweza ukawa na user hata watatu kazini, personal, guest kwenye simu yako na zote ukazi process kwa pamoja
kuna mambo mengi sana unaeza ukatumia processor yako kwenye android ila kwenye ios huwezi.

5. camera
iphone x ina camera nzuri zaidi kuliko s6 active

hayo ni mambo yako na mimi naongezea yangu

6. bei
s6 active unaiokota ebay chini ya $200 sometime mpaka $120 kwa hela za kitanzania ni around 400,000 wakati iphone x ni dola 1000 kupanda aka 2,300,000 kupanda.

7. connectivity
nikiwa na s6 edge yangu nitachomeka waya wa HDMI na adapter ya usb, nikiamua nitatumia wifi kama miracast au widi nitaangalia kwenye tv kupitia simu etc, iphone x ina airplay tu hio hio ndio utumie kama huna utajijua mwenyewe na airplay ni weaker kuliko miracast. pia naweza chomeka vitu kama hard disk, mouse, game controller za usb, keyboard na vyenginevyo kwenye usb port.

8. 3.5mm jack
iphone x haina sehemu ya kuchomekea earphone zaidi ya ile port ya kuchajia, ukitaka kusikiliza kitu huku unachaji mpaka ununue adapter. huku kwenye active hakuna hayo.

etc etc etc yapo mengi sana.

so bwana island ungetoa milioni 2.3 kununua simu dhaifu au utoe 400,000 kununua simu bora zaidi?
 
Heheee kweli maisha ni nini unataka,usipojua utahangaika sana.kwa hii dolla 200 hupati hata iphone 5s wakati ni simu ya kipuuzi hailingani kwa chochote na six active.

Wacha android tuenjoy maisha.
 

Mkuu nenda tu kkoo chukua laptop i3 ya laki 3 ongeza na modem ya 4G elf thelathini hivo vitu ulivyotaja hapo juu utaweza kuvifanya mara mia zaidi ya hiyo simu . Utapata kioo kikubwa 15” badala ya tuvioo twa simu sijui 5.5” , utaweza kucheza movie zaidi ya kumi kwa wakati mmoja, utaweza kuweka programme mpaka za gb kumi, games ndo usiseme, utafanya kazi kwenye Ms office vizuri kabisa achana na simu ambayo hata proposal ya page kumi huwezi kuandika, utachomeka Hdd za terabyte kadhaa mbili au tatu kwa wakati mmoja, utapata internal storage 500gb na unaweza badili internal disk anytime Kama external hazitoshi, kwa modem yako utaweza kupiga cm , ku download movie zaidi ya 30 kwa wakati mmoja, utafungua browser zaidi ya tano kufanya mambo yako ya kimtandao, utaweza kuchora ramani za majengo kwa software kubwa achana na simu ambayo kazi hizi ni ndoto utaweza kuweka software Kama bluestacks na ku run android programme, utaweka Linux humo humo na vitu vingine vingi. Vyote kwa sh 330,000/= tu

Usikubali kuibiwa mkuu .

Mbali na ushauri hapo juu pia nimeweka snapshot toka gsmarena ambao leo hii umesema unawaamini, wao kwa upande wao wameongelea performance ya “Beast” iPhone X Kama ifuatavyo, labda tu uamue kuwakataa lakini machache ya kwao ndo hayo Hapa chini

Kifupi ni kwamba visimu vingine vimeachwa mbali.
 
nilijua tu utarudi kwenye benchmarks, tunafahamu A11 ina speed hakuna anaekataa ila ina utofauti gani na joka la kibisa? nimekwambia nitajie matumizi sina shida na benchmark ambayo ios inatake advantage ya hio nguvu ya soc?

nimekupa mifano mingi hapo juu ya namna android inavyotumia soc zake.

na last time naangalia s6 active ni simu sio laptop,
 

Haaaa haaaa yan Iphone X performance inakuwa kubwa mpaka unauliza hii yote ni ya kufanyia nini ? hilo ndo mnaloweza kusema baada ya kukutana na unrivaled A11 Bionic chip a.k.a "Mistral" and "Monsoon." Hizo flagship zenu zinazidishwa mara mbili kama siyo tatu.

Hizi ndo kazi za kupongeza na kujifunza, Tafuta kitabu cha bill gates kinaitwa Business@the speed of thought utajua kwa nini haya mambo ni muhimu na jamaa aliya predict toka miaka hiyo.
 
hujajibu swali, kuna task gani kwenye ios inayohitaji cpu kubwa? usikimbie swali na kuongea mambo ambayo hujaulizwa.
 
Mkuu mkwawa amekufafanulia vizuri sana hapo juu.ila sababu ya ubishi usio na msingi hutaki kuelewa.

Embu nieleze kwa speed hiyo ya iphone x kipi itafanya ambacho hakifanyiki ktk simu zingine???
 


Marekebisho kidogo. Iphone x display sio QHD. Resolution yake ni ndogo ya QHD (2880 x 1440) vs iphone x 2436 x 1125
 
Hapa kesi imeisha.
 
vimbwanga vya face id vikiendelea


told you guys muda ni mwalimu mzuri,

mchichapori
Mkuu apple walisema kwamba sio kwamba simu ikiwa na face id dunia nzima watashindwa kuifungua,ila walisema kuwa fingerprint ni 1:50000 na face id ni 1:1,000,000 kwa hiyo sijaona makosa yako wapi hapo.
Kama hii video ni kweli basi huyo mtoto ni one in million kati ya wanaofungua hiyo simu.
Kwa hiyo apple sio wa mchezo mchezo.
Hapa hata kesi huwezi kuwapa kwa sababu walishasema wao. anything?
 

Attachments

  • 1277899829_termionator-2-bomb[1].gif
    5 MB · Views: 34
Hayo mambo yote yalikuwa addressed pale Steve jobs theater. Siyo mapya
 
Hayo mambo yote yalikuwa addressed pale Steve jobs theater. Siyo mapya

1. wali adress kwamba mask itafungua simu yako? walikataa kata kata na kuonesha demo yao ya uongo na kweli

2. walisema simu ya mzazi itafunguliwa na mtoto au vise versa?

3. walisema simu itafunguliwa na kaka au ndugu?

ninachokumbuka walisema tu twins,

hilo la mama na mtoto ndio baya zaidi sababu watoto watapata dezo ya kuangalia porns na mambo wasiyopaswa waone, na watoto wa siku hizi walivyo wasiri mpaka ukigundua its too late.

mkuu island ulikuwa unaniforce nikupe jibu baina ya face id na iris ipi nzuri, hope jibu umelipata.
 

Umeona wapi imefunguliwa kwa mask , au ile video uliyoleta huku una wasi wasi nayo yan we mwenyewe huiamini ndo inakufanya u conclude haya , umeleta rumours ngapi za kuiponda iphone X ambazo zote baadae zikagundulika hazina mashiko , kwa hiyo kila unachoona you tube basi ni cha ukweli ? Hiyo video ya mama na mwanae inaonesha upande mmoja mama akiwa anaweka lock lakini kwamba lock inatolewa na mtoto haioneshi, bali dogo anaangalia then anageuza simu inaonesha kesha unlock , hata ile ya mask haioneshi kama kweli ile mask ilitoa lpck badala yake unaoneshwa simu ishakuwa unlcked. unaaminije video za hivi mkuu , these videos are too cheap to trust. kuna video za kuamini ambazo zinaonesha simu ikiwa inatoa lock mbele ya uso na vyote vinaonekana in real time, video za hivo at least unaweza ziamini.

Hapa naweka snap yako mwenyewe ukiwa huna uhakika kama ni hoax ama la,

Hapa ntakuwea video zinazoonesha uso na screen ya simu at the same time , hizi at least unaweza kuamini. Hapa ni video ya Mkbhd akiwa anaongelea face id , angalia angle ya camera na jinsi anavyofanya.


 
hahaha kwa hio dogo alivyoangalia nini kimefungua pale miujiza au? na simu ilipoelekezwa kwenye mask ikafunguka nini kimefungua? video zote mbili wameanza kutest wao wenyewe kisha wakaelekeza kwa mtu/mask ambayo si owner wa simu, ulitaka vipi wewe?

wangeonyesha simu ikifunguka bila sura ungekuwa wa kwanza kusema kuwa mbona hawaonyeshi sura ya mfunguaji.

hebu nioneshe na iris basi ikichezewa kama hivyo.
 

Mkuu siwezi ku deal na rumors, kila mtu anaweza kuweka video youtube na akasema chochote, ingekuwa trusted source au cases za hivo zimekuwa nyingi tungezipa mashiko bila hata kusubiri apple wenyewe kutoa public release.

Una habari kwamba hata fingerpring na iris scanner zilikuwa na cases kama hizi ? Hujakutana nazo? tena hiyo iris scanner ilikuwa fooled kwa picha tu on first day.
 
show me mkuu, iris scanner imekuwa fooled na picha, usilete zile za android ambazo zinatumia front camera zile ni fake nataka true iris scanner kama ya windows hello ambayo inascan retina yenyewe na sio kucapture 2D picture ya jicho. nioneshe mahala popote lumia 950 au lumia 950xl, au HP elite x3, au suraface pro na kifaa chochote chenye iris scanner yenyewe inayoscan retina kimekuwa fooled either first day au na picha etc.

mkuu hizo sio rumors, rumors au tetesi ni kitu ambacho hukioni kwa macho, leo hii ukimuona mtu anagongwa na gari barabarani ni rumors? video umeekewa mama na mtoto live kabisa na site zote kubwa duniani wamereport, tena sio video ya kwanza kuna video kibao nimeziona watu sio twins ila wanaingiliana na face id, hapa huwezi kataa mkuu na kusema ni rumors, na nakwambia bado haijaenda mainstream face id utaona vituko zaidi ya hivi.
 
fungua hiyo video

Mkuu video hii hapa window hello madogo wamei fool kirahisi sana,

 
fungua hiyo video

Mkuu video hii hapa window hello madogo wamei fool kirahisi sana,

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…