Aona ndoa chungu kwa kero za wakwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aona ndoa chungu kwa kero za wakwe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jun 17, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  [TABLE]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD]MWANAMKE mmoja[30] [jina linahifadhiwa] mkazi wa Ukonga jijini Dar es Salaam, amechukua uamuzi wa kumfata mchungaji aliyemfungisha ndoa kwa kuchoshwa na vitendo anavyofanyiwa na ndugu wa upande wa mume wake aliyefunga nae ndoa miaka minne iliyopita k[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Chanzo cha habari hii kilidai kuwa, mwanamke huyo aliyebahatika kupata mtoo mmoja wa kike katika ndoa yake hiyo, alikuwa akilazimishwa kutengana na mwanaume huyo na ndugu wa mumewe nayeye pia kuchoshwa ili awe huru maishani kutokana na kuchoshwa na vitendo ambavyo ameona vinampa bugudhi katika maisha yake ya kila siku

  Chanzo cha habari kilidai kuwa, mwanamke huyo amepeleka ombi ya kuvunja ndoa yake baada ya wakwe zake kumpa tuhuma kila kukicha kuwa ni mshirikina kwa kuwa mume wake anamuonyesha upendio wa dhati na kumsikiliza kwa kila analolihitaji kwake

  Imedaiwa kuwa, mume wa mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina moja la Frank alikuwa na utamaduni wa kusikiliza ushauri anaopewa na mke wake kuliko mtu mwingine yeyote aliyekuwa chini ya jua

  Kutokana na upendo huo anaouonyesha kwa mkewe huyo ndugu wa mwanaume huyo walikuwa hawafurahishwi kabisa

  Imedaiwa kuwa, kutokana na upendo huo kwa mke wake ndugu wa mume walianza minong’ono ya hapa na pale kuwa mwanamke huyo ni mshirikina na walifikia uamuzi wa kumuamuru amuacha mwanamke huyo na aoe mwanamke wa kabila lao kwa kuwa walikuwa na maadili mazuri

  Hata hivyo imedaiwa Frank wazo hilo alilopewa na wazazi wakiwemo ndugu hakuweza kulipokea kwa mikono miwli hivyo kupingana nao na kitendo hicho kilizidi kuwauzi ndugu hao na kuanza vituko vya wazi kwa mwanamke huyo

  Imedaiwa kuwa, mwanamke huyo mfanyakazi wa serikali huku mume wake akiwa mfanyabiashara katika upande wa madini waliweza kujipatia mashamba mawili, nyumba moja na gari ambalo limedaiwa kuwatoa roho ndugu hao kwa kudhani mmiliki halali ni Frank kumbe ni kinyume kwa kuwa mwanamke huyo alinunua gari hilo kwa njia ya mkopo anaokatwa kwa kila mwezi katika mshahara wake

  Bila kutambua hilo wazazi walimtaka Frank gari hilo liwe kwenye mfumo wa kubeba abiri yaani ‘Tax’ ili liweze kuwasaidia kipato cha kila siku kitendo ambacho Frank aliwajibu haitawezekana kuchukua maamuzi hayo kwani si mali yake kama wanavyofahamu bali ni mali ya mikewe na aliwataka wazungumze na mkewe kama wangekubaliana waelewane wao wenyewe

  Kutokana majibu hayo wazazi hao walitishia kumtenga mtoto wao huyo kwa kumuweka mkewe mbele wao nyuma na tokea kutoa majibu hayo wazazi ,wakiwemo na ndugu walionyesha chuki ya juu kwa mwanamke huyo na kuanza kumfanyia vitendo vya ushirikana ili aweze kutengana na mwanaume huyo

  Chanzo kilidai kuwa, walikuwa wakimtuhumu mwanamke huyo kuwa ni mshirikina na kumuambia dhahiri kuwa atengane na Frank kwa kuwa alimfanyia vitendo vya ushirikina ili aweze kumsikiliza yeye pekee na si mtu mwingine na kudiriki

  Imedaiwa mwishoni mwa wiki iliyopita, dada wawili wa Frank walifika nyumbani kwa kaka yao huyo na waliangusha chungu ambacho kilizingirwa na kitambaa cheusi waliambatana na kuvunja mayai aina ya viza kwa kitendo kilichoshuhudiwa na majirani na haikufahamika mara moja kama walikuwa na lengo gani

  Imedaiwa mwanamke huyo walipokuwa wakirudi jioni na mumewe huyo walishangazwa na hali hiyo na wanandoa hao waliingiwa na hofu na kuogopa kuinga ndani kutokana na hofu ya vitu hivyo[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,576
  Likes Received: 12,860
  Trophy Points: 280
  hypocrits
   
 3. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #3
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  ndoa ikashakuwa na wapambe ndi mwanzo wa mwisho wake...ndoa ni mume,mke na MUngu wao,full stop.ukiwaingiza marafiki,ndugu,mkwe nk umekwisha.
   
 4. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,643
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Wakabidhi maisha yao kwa Yesu tu, ndiye muweza wa yote, kutengana ni kumtangazia shetani ushindi. Kila jema huja na jaribu lake.
   
 5. D

  Dr.Mbura Senior Member

  #5
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Yesu ndiyo jibu hata huyo jamaa akilazimishwa kumuacha mkewe watakayemtafutia watampangia masharti pia
   
 6. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2011
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,584
  Likes Received: 848
  Trophy Points: 280
  ni hulka mbaya sana ya hawa ndugu wa mume na kwa kuwa huyo mwanaume anahusika na madini basi ndugu wanajua mali zote ametafuta mwanaume na hapo ndipo tabu ilipo kwani kama huyo mume asingekuwa na kazi sidhani kama wangemsumbua mkwe wao hivyo au kama angalikuwa anakaa nao nyumba moja huenda hata ndoa isingekuwepo. poleni wapendwa na kila mmoja amwone mwenzi wake ni wathamani ktk maisha yake pia hayo mambo ya ushirikina ni kumwomba Mungu azidi kuwalinda siku zote
   
Loading...