Uchaguzi 2020 Antoni Komu amesoma alama za nyakati alikuwa mzigo tu jimboni

2019

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
2,982
4,457
TAHADHARI!! KORONA IKO MTAANI SASA PAMBANA JUU CHINI USIISHI KIMAZOEA.

Kwenye mada

Kwanza kabisa jimbo la Moshi Vijijini halijawahi kuwa miliki ya chama chochote cha siasa yaani hakuna chama kinachoweza kudai pale ni ngome yake.

Toka mfumo wa vyama vingi uanze 1995 wabunge waliowahi kuchaguliwa pale ni kama hivi.

Uchaguzi wa 1995 Ngoto Laino kupitia NCCR Mageuzi
Kipindi hiki sikuwa na uelewa kwenye siasa sababu nilikuwa mdogo lakini mwaka 2000 huyu mzee hakurudi tena. Inadaiwa hakutekeleza ahadi zake akapigwa chini.

Uchaguzi 2000 akapewa nafasi Thomas Ngawaia kupitia TLP (jirani yangu kabisa) akatoa ahadi nyingi sana lakini ambayo ilikaa akilini mwa watu ni kuleta gari ya wagonjwa. Huyu baada ya kuchaguliwa akala kona hakuwahi kuonekana kijijini tena. 2005 akarudi akiwa CCM kwenye kura za maoni akapigwa chini na Cyril Chami.

Uchaguzi 2005 Kapewa Cyril Chami kupitia CCM huyu mzee alipambana sana kwanza alijenga shule ikaitwa kwa jina lake anatekeleza baadhi ya miradi muhimu akajenga barabara ya kutoka Shanty town hadi KNCU

2010 Cyril Chami akaomba tena na akapewa mara ya pili akavunja rekodi ya kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa mara mbili. Sina hakika kama utekelezwaji wa miradi ni kwa sababu alikua CCM ama la.

2015 kipindi cha viguvugu la mabadiliko Cyril akakataliwa na wananchi na hatimaye akapita Antoni Komu kwa nguvu ya wananchi tena kwa shida kubwa sana maana walilinda kura mpaka alipotangazwa.

Toka 2015 alipochaguliwa Komu hakuna alichofanya hata kimoja,kama maendeleo yanaletwa na chama na sio sera wananchi wamesema bora CCM tu maana maendeleo wanayaona.

Kuna barabara kubwa sana inatoka Masoka hadi Kibosho hospitali hii barabara ni muhimu sana lakini ameshidwa hata kuiombea iwekwe lami na ina huduma zote za kijamii kama mashule na vyuo vingi tu hakuna hata kituo cha polisi.
Komu alijua kabisa hana chake pale jimboni hata akigombea kupitia CCM hatopata tena

Wananchi wa Moshi huwa hawaangalii sura wala chama wanachoangalia ni utekelezwaji wa ahadi tu ukishindwa unakula kona.

2020 atakuwa ni nani?? Sera zipi zitampa nafasi ya kugombea na kupita? Tusubiri tuone

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kauli Hii Aliwahi Kuisema Augustine Lyatonga Mrema (Mzee Wa Kiraracha)
Namnukuu:-
"Ukishindwa Kuuza Jumla, Uza Rejareja "
😁😊😀😄😅😃
 
Huyu komu kajiharibia kabisa na atapotea kwenye medani za kisiasa! Bora angemaliza kabisa ngwe yake na akafanya kuhama kwake Siri yake lakini kwa nguvu za Mungu kamfanya aropoke! Atakosa yote yaani mwana na maji ya Moto kwani wiki hii haitokwisha bila kutupwa kule! Na hapo ndio ataijua cdm mpya bila wanafiki inafanyaje kazi! Karibu uraiani mhasibu mbobevu usiyeweza kujiajiri!
 
Tuendelee kushuhudia tu
Huyu komu kajiharibia kabisa na atapotea kwenye medani za kisiasa! Bora angemaliza kabisa ngwe yake na akafanya kuhama kwake Siri yake lakini kwa nguvu za Mungu kamfanya aropoke! Atakosa yote yaani mwana na maji ya Moto kwani wiki hii haitokwisha bila kutupwa kule! Na hapo ndio ataijua cdm mpya bila wanafiki inafanyaje kazi! Karibu uraiani mhasibu mbobevu usiyeweza kujiajiri!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom