Antofagasta: Somo muhimu wa JPM na CCM.

Travelogue_tz

JF-Expert Member
Sep 28, 2010
848
1,212
Tethyan Copper Company Pty Limited (“TCC”) ni kampuni tanzu iliyoundwa kwa Muungano kati ya Antofagasta plc ya nchini Chile na Barrick Gold Cooperation ya nchini Canada.
Kampuni hizi kwa pamoja zinasemekana kuwekeza kiasi cha dola za kimarekani bilioni 3 katika mradi mkubwa ujulikanao kama Reko Diq ikimaanisha mradi mkubwa zaidi wa uwekezaji wa madini nchini Pakistan.
Mradi huu unapatikana katika jimbo maarufu la Balochistan, na ulitegemewa kugharimu zaidi ya dola za kimarekani bilioni 3 kama fedha za uwekezaji wa awali wa mradi husika . Reko Diq ni miongoni mwa eneo lenye utajiri mkubwa wa copper na dhahabu duniani ambalo bado halitaendelezwa, na utajiri wake unakadiriwa kuwa na uhai wa zaidi ya miaka 50.
Mnamo mwaka 2011 katika harakati za kuendelea na zoezi la utafiti katika eneo hilo , Tethyan Copper Company Pty Limited (“TCC”) ilitakiwa kuomba leseni ya muendelezo wa uchimbaji na utafutaji wa madini kama sehemu ya masharti ya mkataba unavyotaka, kinyume chake Utawala wa jimbo la Balochistan ulikataa kutoa kibali husika huku kampuni hiyo ikiwa imekwisha wekeza kiasi cha dola za kimarekani milioni 500 kwa ajili ya utafiti na upembuzi yakinifu wa mradi husika.
Katikati ya mwaka 2013 Serikali ya Balochistan ilifungua kesi katika Mahakama Kuu Zaidi ya Pakistan kuhoji uhalali wa kisheria wa mkataba kati ya Tethyan Copper Company Pty Limited (“TCC”) na mamlaka ya Jimbo, na Mahakama iliipa ushindi Mamlaka ya Jimbo hilo na hivyo kuwa pigo kwa Kampuni ya Antofagasta na Barrick Gold Cooperation.
Kutokana na maamuzi hayo, pamoja na zuio la kusitisha leseni lililofanywa na mamlaka, Mlalamikaji aliingia katika majadiliano na Serikali ya Jimbo la Balochistan. Tethyan Copper Company Pty Limited (“TCC”) alifungua shauri husika kutokana na Serikali ya Pakistan kutenda kinyume na sheria kwa kukataa kutoa leseni ya madini ili kuwezesha uendelezaji wa Mradi wa Reko Diq mwaka 2012.

Katika taarifa yake Barrick Gold Corporation (NYSE:ABX)(TSX:ABX) (“Barrick” or the “Company”) ilieleza kwamba Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya kibiashara ( Arbitration tribunal of the World Bank’s International Center for Settlement of Investment Disputes (“ICSID”) siku ya Tarehe 20 Machi,2017 ilitoa maamuzi kuhusu usuluhishi wa kampuni tanzu ya Tethyan Copper Company Pty Limited (“TCC”) iliyoundwa kwa Muungano kati ya Antofagasta plc na Barrick, dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Pakistan.
Mnamo March 21, 2017 ICSID ilitoa maamuzi/ hukumu kwa kuipa ushindi kampuni ya Antofagasta plc na Barrick Gold Corporation katika shauri maarufu linalojulikana kwa jina la Reko Diq Arbitration Proceedings TORONTO .
Katika siku hiyo ya Maamuzi, ICSID tribunal ilikataa hoja za utetezi upande wa Serikali ya Pakistan , na kuthibitisha kwamba Pakistan ilikiuka vipengele mbalimbali vya sheria za Uwekezaji kati yake na Australia ambapo kampuni ya TCC imesajiliwa.
Kutokana na hukumu hiyo, Wawekezaji hao walifungua shauri kuhusu fidia lilianza kusikilizwa Machi,22 ambapo Mahakama itapanga kuamua juu ya kiwango cha fidia kitakachopaswa kulipwa na Serikali ya Pakistan kwenda kwa kampuni ya TCC, huku hukumu ikipangwa kutolewa Mwaka 2018.
Wataalamu wa Uchumi na masuala ya madini wanakadiria kwamba Serikali ya Pakistan inaweza kuwajibika kulipa kiasi cha takribani Trilion 23 kutokana na ukiukwaji wa wazi wa Mikataba ya Uwekezaji.

ICSID Issues Decision In Favor Of Antofagasta, Barrick In Reko Diq Case.

Pakistan’s $500bn gold mine kept under wraps | The National
 
Nenda kamsaidie Lisu, mtafanya naye kazi vizuri.
 
Ukiongea tofauti na huu uhalisia unaitwa mnafiki, mchumiatumbo msaliti uliyekosa uzalendo na kwamba unatetea wazungu ili upate 10%
Lakini kwenye Bible tulifundishwa kuwa werevu kama nyoka DAUDI kijana mdogo tu aliyekuwa na kombea alimshinda jitu kubwa GOLIATI shujaa wa vita... Daudi alitumia akili na werevu hakutumia maguvu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom