Antaktika ndio Jangwa kubwa zaidi kuliko Sahara

Apr 6, 2024
99
116
Jangwa linatambulika kwa sifa zake za kuwa na unyevu wa chini sana (upungufu wa mvua) badala ya kuwa na hali ya joto au baridi. kigezo kikubwa cha utambuzi wa jangwa ni kiasi cha mvua kinachopokea kwa mwaka.

Sababu Antaktika inapokea wastani wa chini ya 200 mm (8 inches) za mvua kwa mwaka katika maeneo yake mengi. Katika baadhi ya sehemu za ndani za bara hili, mvua inaweza kuwa chini sana, hadi kufikia karibu na sifuri.

Licha ya kuwa na barafu na theluji nyingi, unyevu wa hewa ni wa chini sana, na hivyo kufanya mvua kuwa nadra sana. Hali hii ya kukosa unyevu ni sifa kuu ya jangwa.

Antaktika ina eneo la takriban kilomita za mraba milioni 14, ambalo linaifanya kuwa jangwa kubwa zaidi duniani kwa ukubwa na eneo.

Upande wa Sahara inapokea wastani wa mvua ya chini ya 250 mm (10 inches) kwa mwaka, ambayo bado inakidhi vigezo vya kuwa jangwa. Hata hivyo, hii ni juu zaidi ikilinganishwa na Antaktika.Sahara ni jangwa lenye joto kali, lakini kiwango chake cha joto hakifanyi kuwa jangwa kubwa zaidi bali ni kiwango cha mvua kinachopokea.

Sahara ina eneo la takriban kilomita za mraba milioni 9.2, ambayo ni ndogo zaidi kuliko eneo la Antaktika, hivyo haiwezi kuwa jangwa kubwa zaidi duniani.

Jangwa linatambulika kwa sifa zake za kuwa na unyevu wa chini sana (upungufu wa mvua) badala ya kuwa na hali ya joto au baridi. Kwa hivyo, kigezo kikubwa cha utambuzi wa jangwa ni kiasi cha mvua kinachopokea kwa mwaka. Hii ndio sababu kuu kwa nini Jangwa Kubwa zaidi duniani ni Antaktika, na si Sahara.

dsaffdf.jpeg

 
Back
Top Bottom