Another crisis in the making | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Another crisis in the making

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by KIWAVI, Jan 20, 2010.

 1. KIWAVI

  KIWAVI JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 12, 2010
  Messages: 1,747
  Likes Received: 376
  Trophy Points: 180
  Wakuu, hii si news lakini ni news;

  Kuna udhaifu mkubwa sana hapa nadhani katika wizara ya miundombinu wa namna ya kuendesha hizi ferries na time management achilia mbali priorities za nguvukazi hapa ferry

  Kwa upande wa bandari, naona wameanza tabia ya kuruhusu meli zipite prime hours kama saa moja asubuhi nk. bila kujali kwamba huo ni muda wa kazi na watumishi wanaoishi kigambo wanateseka wakipisha meli ipite... jambo ambalo lingeweza kufanyika hata alfajiri au usiku wa manane... cost ya huu uzembe inaweza kuzidi mamilioni kwa dakika kwani inachelewesha vivuko, inachelewesha watendaji na kwa hesabu za harakharaka ni zaidi ya laki moja wanaovuka asubuhi

  Ukija kivukoni, jamaa ndio hamnazo, kwanza wanasubiri gari zijae ndio wawashe kivuko cha pili, halafu wameanza kupokea vijisenti vya kufanya baadhi ya gari kuwa premium kwa hiyo zisipange poleni

  Ukija kwenye daraja, naona huko sasa imekua another ATC... hakuna tena anayezungumza... cha kushangaza ni kwamba kuna vigogo wa wizara humohumo ambao wao hupita ki-VIP na kusahau kwamba zile foleni ni mazao ya kazi zao pungufu

  Watu wazuiwa kuendelea na ujenzi lakini hakuna kinachoendelea, tumeingia kwenye siasa na kusahau maendeleo

  Mwisho ni kwamba mbunge yeye naona ameamua kunenepa tu na kuacha wananchi wake

  surely this is another crisis in the making
   
 2. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  okay asante mkuu, je unaufumbuzi wa hayo?
   
 3. KIWAVI

  KIWAVI JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2010
  Joined: Jan 12, 2010
  Messages: 1,747
  Likes Received: 376
  Trophy Points: 180
  Mchagga, kumbe mko wengi!!! sikujua kwamba hata hilo unahitaji mkoba...
  kwa wizara nadhani waajiri competent staff na wawape training za logistics, customer service na umuhimu wa ile channel ya mawasiliano. kikubwa zaidi waache kuajiri vibarua ila wawe na permanent staffs... ulinzi wa pale bado ni walakini hivyo wa-review utaratibu wao

  kumbuka kwamba zile ferries zina engine nne, nne lakini utakuta wakati wa rush hour mtu anawasha mbili na power ya kivuko inapungua delays zinatokea au hata sometimes kuna nahodha mmoja yeye huwa anaenjoy namna watu wanavyopanga ile misururu

  kuhusu bandari, ni lazima wareview hizo schedule za kuruhusu meli

  kuhusu daraja, its four year now, wanapitia mikataba, wanarekebisha, wanapitia, wanarekebisha, wanapitia, wanarekebisha... enough is enough!!! wafanye kazi maana tunajua kwamba ule mradi wa ferry unawanufaisha watu pale..

  au mpaka watu waje waseme jinsi yale mapipa yaliyo nyuma ya wakusanya tiketi yana kazi gani humu? unajua nani anakusanya yale mabao? ni kama kashfa ya trafik wanaopewa zile pikipiki... WATANZANIA TUAMKE NA KUSUKUMA MAENDELEO
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Jan 24, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ni kweli kabisa... the economic value and potential za kigamboni zinategemea sana efficiency na success za ferries... ndio blood vessels za kigamboni, kwa bahati mbaya watanzania wengi hatuoni mambo kwa style hiyo, huwa tunasubiri wanasiasa waanze kelele ndio tugundue matatizo yetu

  Kigamboni is unique but very far behind is full potential
   
 5. g

  gudlack Member

  #5
  Jan 24, 2010
  Joined: Oct 11, 2009
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nivema ukatoa na ushauri kwani wenyenchi huwaga wanapita huku they can buy your ideas insteady ya kulalamika tu
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ushauri ni kwamba ile ferry iendeshwe kwa ubia kwani waliopo sasa wengi wao ni wabadhirifu na pia ni temporary staffs hasa ukizingatia kwamba kile ni chombo muhimu sana

  wabadilishe system ya kukata ticket na waweke independent monitoring system ya matumizi ya mafuta

  watumie mpango wa trip schedules na sio wa sasa ambapo nahodha au kiongozi anayekuwepo anachangia ferries kwenda kasi au taratibu kutokana na "hesabu" a siku na tamaa/ubinadamu
   
 7. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Wanabana mafuta yasitumike inavoyotakiwa?:confused:
   
Loading...