Anne Makinda, historia ya watanzania kumsaliti Oscar Kambona lazima iwasute | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anne Makinda, historia ya watanzania kumsaliti Oscar Kambona lazima iwasute

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SubiriJibu, May 11, 2012.

 1. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,124
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  Spika wa Bunge, Anne Makinda, amesema Tanzania inahitaji muda zaidi wa kujipanga ili kujikita kikamilifu katika mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

  Amesema Tanzania ni nchi kubwa yenye mipaka mipana na watu zaidi ya milioni 45, hivyo kuingia huko bado ni mapema mno kunahitajika muda zaidi.


  “Siyo kwamba tunasita. Isipokuwa bado hatujawa tayari na tunahitaji muda zaidi. Kuna haja ya kuwaelimisha watu wetu kwa makini ili tunapoingia kusiwe na wasiwasi wowote”


  “Tanzania inataka kwanza ihakikishe wananchi wake kwanza wanapata vitambulisho vya taifa kabla ya kujikita na sera nyingine za mtangamano”.


  SOURCE: NIPASHE

  DATE: TODAY

  PAGE: 12

  MY TAKE:

  MAANA YA KWANZA

  Mambo mengi ya Julius Nyerere hayakudumu baada ya kuondoka kwake siasani na duniani. Hayakudumu kwa sababu aliyaingiza kama yake binafsi na si kitaasisi.

  Kumbuka tamko kwamba yuko tayari kuchelewesha uhuru wa Tanganyika kusubiri Kenya na Uganda ili uhuru uje siku moja kwa nchi moja kubwa iitwayo East Africa Federation.

  Tamko lile alilitoa mwaka 1959 akiwa Ethiopia mbele ya wanafunzi wa Tanganyika waliokuwa wanasoma kule. Wanafunzi hao walimzomea palepale na ndiyo maana ile ni moja ya hotuba kadhaa ambazo hazijachapishwa na kitabu chochote chenye hotuba za Nyerere.

  Huku nyumbani, ilibidi Katibu wa TANU, Oscar Kambona atoe tamko kwamba hiyo ilikuwa kauli binafsi ya Nyerere na haikuwa kauli ya TANU kwani haikuwa imebarikiwa na kikao chochote cha TANU.

  Wachambuzi wengi huwa hawautaji kama huu ni ugomvi wa kwanza kati ya Kambona na Nyerere kuhusu masuala ya msingi.

  Kilichofuata baada ya hapo ni mengi. Vikaja muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao hata haukuwa na ridhaa ya watu bali mikakati ilifanyika kwa siri kama Nyerere alivyokiri mwenyewe.

  Hatimaye mwaka 1967 likaja Azimio la Arusha. Kambona akaona mambo hawezi kuendelea kuwa ndani ya serikali kwa mtindo ule. Akaamua kuachana na siasa.

  Nimemtaja Kambona si kwamba alikuwa sahihi. Bali ni kweli kwamba tupende, tuchukie, ukweli ni kwamba aliona afadhali aweke wazi anayochukizwa na Nyerere kuliko kukaa kimya tu wakati dhamiri inamuambia kuwa hakubaliani nayo.

  Kambona angekuwa mnafiki basi wa kuea “Yes-man” basi hakuna ambaye angemfikia hapa nchini ukiangalia urafiki wake na Nyerere ulivyokuwa wa kiwango cha juu kuliko mtu yeyote.

  Kwa nini nimemtaja Kambona? NImemtaja Kambona kwa sababu ali-sacrifice urafiki na maraha yote aliyoweza kuyavumilia kwa unafiki. Leo dunia inamkumbuka kama mtu aliyekataa waziwazi mawazo ya Nyerere.

  Ajabu leo, wanasiasa waliokuwa hawampingi Nyerere walipokuwa naye madarakani ndiyo wenye kutoa kauli ambazo angezisikia angewafukuza kama alivyotimka Kambona na wengine.

  Kusema kwamba “Tanzania hatujawa tayari kuingia East Africa” ni kauli ambayo wanasiasa hawa wana uwezo wa kuisema wakati Nyerere yuko kaburini.
  Anne Makinda yumo TANU, CCM na Serikalini tangu 1975. Ashingethubutu kutamka kauli hii akijua nia ya wazi ya Nyerere ilikuwa ni kuunganisha East Africa yote.

  Je, nikisema kuwa huu ni unafiki nitapigwa ban? Ukweli tuuite ukweli tu.

  MAANA YA PILI

  Maanay apili ni kwamba kumbe Nyerere, Obote na Kenyatta wangeungana basi leo hawa akina Makinda na wengine wangekuwa na kitu kiitwacho “Kero za Muungano wa East Africa” Wenye mawazo kama Makinda wangesema, “Tanganyika tuliungana kabla hatujajipanga” au “Tanganyika tuliungana kabla hatujawa tayari”

  Hadi hapo sisemi kuhusu chanzo cha kero za Muungano wetu na Zanzibar.

  Ni hawahawa ambao kabla ya “Azimio la Zanzibar” kimyakimya moyoni mwao walikuwa wanajisikia kuwa kuna “kero za Azimio la Arusha”. Walisubiri Nyerere aachie uenyekiti na hawakupitisha hata miaka miwili wakaondoa kero zile kwa kuleta “Azimio la Zanzibar”.

  Hivyo, ni heri kuwa kama Kambona hakupata nafasi hapa duniani kushuhudia aliyoyapinga sasa dunia imemsaidia kuyaondoa tena Nyerere akishuhudia na asifanye kitu kwani asingeweza kutimua dunia nzima ya utandawazi.

  Kungekuwa na uwezo bais mtu kama Kambona alitakiwa kuishi kwa muda mrefu hadi sasa ili wanafiki wanaojitokeza sasa hivi aweze kuwasuta kwa kuwauliza “acheni unafiki na undumilakuwili wenu, mlikuwa wapi wakati nayapinga mwenyewe hadi mkanifukuza”

  Hivyo, sera ya kusubiri kujiunga na East Africa federation. Binafsi siishabikii kwa maana kwamba mimi ningependa hata leo tujiunge. Hili lisilete mjadala kwa sababu ni mtizamo wangu.

  Lakini pamoja na kwamba sipendi tuchelewe, bado ninajua kwamba kutopenda huku kunaweza tu kuelezwa vizuri na CHADEMA au chama chochote cha upinzani. Mwana CCM akitaka kutudanganya kwamba anataka tusubiri basi, kwanza ajue ana deni la kutueleza ni kwa nini miaka yote ya uhai wa Nyerere mtizamo wao kama chama ulikuwa ni kuwahi kiasi cha kuuchelewesha uhuru wa Tanganyika halafu leo mtuambie kuwa tucheleweshe muungano na East Africa!

  Mjadala mwema!
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,604
  Trophy Points: 280
  Nakuipa tano kwa udadavuzi mahiri!naona huyu bi kiroboto hata uwezo wake kuchambua mambo una mashaka makubwa!!heshima yako and salute nimeipenda hii
   
 3. Z

  Zinjathropus JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2012
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kaka, ni miaka mingi sana toka enzi za akina Kambona, Anne Makinda kujiunga na TANU, Jinsi tunavyotawaliwa na kujitawala, mwenendo wa siasa zetu kuna vyama vingi sasa (sababu za maamuzi zinabishana), hali za uchumi wa mataifa ya sasa na yale wakati ule yapo tofauti, uzingatiaji wa demokrasia umekua kia-ina.

  Inabidi kujikinga pia na malalamiko au kuangalia sababu kuu za kuungana leo, surely sio zilezile za Nyerere za wakati ule. Na kwa fikra za Nyerere muungano unaoliliwa leo naamini angekuwa wa kwanza kuupinga kwa sababu zilezile alizokuwa anapigania muungano wa miaka hile (exploitation).

  Sasa wewe mleta mada kabla ujamuhusisha baba wa taifa kwa fikra zako usimsizingie bado angeutaka muungano huu ambao hayo mataifa tayari yameshawakuta sasa wanalilia ardhi yetu kwa manufaa yao. Si ni wakenya ndio waliokuwa mstari wa mbele kuuvunja muungano wa Kwanza wa kiuchumi wa EA iweje leo waulilie. Sidhani kamwe kwa fikra za mwalimu leo angekuwa anautaka huu muungano kwa kuwa auna madhumuni yaleyale aliyokuwa anayataka yeye.

  Kwa maana hiyo baadhi ya maamuzi yanatolewa sio kwa unafiki bali kwa fikra za sasa, may be its time na wewe huwe creative kidogo na kuacha kukariri tu.
   
 4. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #4
  May 12, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,124
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  Ndilo tatizo lenu kukurupuka bila kusoma wakati vitabu, articles, journals, publications ziko tele.


  Wenye mawazo kama haya mngekuwa mnasoma basi hofu ya wakati ule ilikuwa ni kubwa kuliko sasa hivi.

  Wewe unamuogopa mkenya wa sasa hivi ambaye ni mkikuyu, mjaluo mnandi. Eti hawa ndiyo wanaokupa hofu sasa hivi.


  Kwa taarifa yako ni kwamba wakati Nyerere anadai tuungane, wala hawa wajaluo, waluo, wakikuyu hawakuwa hofu ndani ya East Africa.


  Hofu kubwa ilikuwa ni settlers wa Kenya ndiyo walioogopewa kuliko chochote. Settlers waldhaniwa kwamba tukiungana basi Tanganyika na Uganda itatawaliwa kiuchumi na hao ma-settlers.

  Na hofu yenyewe ilikuwa ni kweli kwani wakati huo umasikini ukiwa wa kiwango cha kutisha na si kama sasa.

  Hivyo, usimsingizie Nyerere kuwa angeukataa muungano unaohitajika sasa hivi kwa hofu ya sasa ambayo mimi ninaiita ya kitoto. Utawaogopaje wakenya watu ambao mmewatangulia kupata uhuru.

  Mtawaogopaje wanyarwanda watu ambao tangu kabla ya uhuru wao wamekuwa watu wa kuchinjana. Nyinyi mnakaa mnafanya nini hadi wenzenu wawe superpower mnakaa.

  Umenifanya nisema nisichokuwa nimepania kwani mada yangu haikuwa huu muungano mnaouogopa sasa hivi. Hoja yangu ilikuwa muupende msiupende ni unafiki mnaoonyesha sasa hivi wakati Tanganyika mliongoza juhudi za kuungana kwa kuwaambia wakenya na waganda kuwa ukabila wao utapungua.

  Hoja yangu imeendelea kwa kwa kuitathmini hali ya sasa iwapo tungekuwa tumeungana.

  Kumbe hata Zanzibar nayo tungesema tusubiri hadi miaka ya 1990 tuungane basi mngesema hayahaya kwamba Tanganyika haijawa tayari kuungana na Zanzibar.

  Na ingewezekana maana Kikwete kaishatutamkia kuwa kuna maombi ya Comoro kuungana na Tanzania na sijui kwa nini kuko kimya.

  Inawezekana ni kutokana na huu usemi mpya uliozaliwa "Bado hatujawa tayari".

  Pambana na wanaume wenzako, usiwakimbie kwamba hauko tayari.
   
Loading...