Anne Kilango achukua fomu ya kuwania spika wa bunge

Kumchagua kuwa mbunge haimaanishi kwamba 'anafaa', kuna watu bogus wengi tu wameshinda, mathalan kuna wanachi kule kwene constituency ya Chenge wamechagua kwa kishindo, hiyo nayo utaizungumziaje?

Wakuu Abdulhalim/Kiranga::

Ukweli mnaouandika hapa nadhani hautawapendeza walio wengi! Anne Kilango hafai hata kuwa Mbunge ukiachilia mbali U-Spika. Ni "mpiga debe" tu na by CCM standards huyo ndiye anayefaa kuongoza! Kuna story nyingi juu yake kule SAME "za kushindwa kutekeleza ahadi zake" ambazo zinafichwafichwa lakini all in all hafai kuwa hata Diwani... NUKTA
 
Kilango Kilango....hafaiiiiii kabisa kua spika!
abakie kama mbunge period!aghhhhh

Wakuu sasa naona tuwe tunatoa reason/s kutokana na misimamo yake ni jinsi gani anavyo weza kunufaisha au kutokunufaisha taifa. Tunahitaji watu wenye misimamo au slogan ambayo tutampima kwa hiyo la sivyo tuanishe qualities za kuwa spika bora.
 
- Mama Anne Kilango Malecela, amekuwa mbunge wa muda mrefu sana sasa toka wa kuteuliwa na Rais Mkapa, na hii ni mara ya pili anachaguliwa na wananchi kuwakilisha jimbo lake la Same East,

- Akiwa bungeni, amekuwa mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama, Makamu wa Mwenyekiti Miundo Mbinu, Mwenyekiti kamati ya Maadili ya bunge, kama ni mabifu yangejiotokeza kwenye hizo kamati hasa akiwa Mwenyekiti wa Maadili ya bunge,

- Sheria iko wazi kwamba mbunge yoyote anaweza kugombea na kuchaguliwa kuwa Spika, wananchi wa Same East siamini kwamba wanaweza kumuondoa Waziri maarufu kama Daniel Yona na kumpa Jimbo Mama Kilango, ambaye ni mapepe na hajatulia mambo mengine ni kwa Great Thinkers kutumia common sense japo kidogo tu kabla hutjaandika hapa uwanja mtukufu.


William.

Mama mdogo LAZIMA
 
Huyu mama hana uwezo wa kuchambua mambo huwa anakariri tu, na kung'ang'ania
 
Mkuu safari ni safari,wabunge siyo machifu kwamba lazima awe wa kabila la eneo analowakilisha. ndiyo maana Joseph Mbilinyi (mkinga) ni mbunge wa mbeya mjini kwa wasafwa!
 
1. Nani kamkataza nani kuchukua fomu? Siye miye niliyesema mama ana haki ya kugombea cheo kama Matonya alivyo na haki ya kugombea urais, lakini the fact kwamba Matonya ana haki ya kugombea urais haimfanyi kuwa anafaa kuwa rais? Umeniona kuandamana kufunga njia mama asichukue fomu? Nimeweka pingamizi sehemu yoyote asichukue fomu?

2.Kusemekana ndiyo basis ya forum, tuna discuss validity ya uwezo wake, kuna watu mpaka wa familia yake wamechangia thread, hawajakanusha, wanamtetea mama ana uwezo, sasa kama mimi naona hana uwezo kwa nini nisiseme?

3. Demokrasia ina mipaka yake, lakini mipaka hii hainifungi nisizungumze nani anafaa kuwa spika na nani hafai.Mind you, sijataka kuingia mjengoni nikapige kura ya kumkataa au kumkubali mtu kuwa spika, sina privilege wala muda huo.Point yako ya kwamba sina haki ya kumchagua Spika ingekuwa valid kama ningekuwa nataka kumchagua Spika, mimi sitaki kumchagua Spika, sifungi safari Dodoma, natoa maoni yangu tu. Tuna wabunge wengi sana wanaoingia hapa kila siku, wanaweza kuona maoni yangu yakawasaidia kuamua, si ndiyo maana ya "representative democracy" hiyo? Kwamba badala ya sote milioni 40 kwenda Dodoma, tunawatuma wabunge mia chache waende kutuwakilisha, tunawapa mawazo yetu wayafikishe kama wakiona sawa, na mimi natoa mawazo yangu, sasa kibaya kipi hapo?

Au Tanzania siku hizi wananchi hawaruhusiwi kutoa maoni yao kuhusu uongozi wa juu wa nchi? Mimi nilifikiri hii ni haki ya kikatiba na ushirikishwaji wa umma maana yake wananchi wasiwaachie wabunge maamuzi yote, bali kuwe na ushirikiano, sasa wewe unasema tuwaachie wabunge wafanye kila kitu hiyo ni "representative democracy" kweli ?

Kiranga:

Unayo haki ya kujadilia mtu. Kitu ambacho sitakubaliana nacho ni mtu kutoa posti ya mstari mmoja na kusema huyu mama hafai. Kama hafai toa sababu basi.

Mpaka sasa wachangiaji wengi katika thread hii wanasema mama hafai. Na washindwa kutoa hoja za kuthibitisha kuwa mama hafai.

Huwezi kumnyima mtu haki zake za kikatiba kwa feelings zako tu kuwa mtu huyo hafai.
 
Kumuondoa Yona kwenye ubunge si kigezo cha ubora wa utendaji wake, kumbuka Yona alikuwa liability kwenye chama kama walivyokuwa kina Mramba na Lowasa bahati mbaya hakuwa na support ndani ya ndani ya chama, miaka hii CCM haichagui spika kwa kuangalia uwezo wa mtu vigezo vyao wanajali nani atetea maslahi ya chama hata kama yanaliumiza taifa, mh. Sitta alijaribu kidogo kufuata maadili ya kazi za spika kwa kuruhusu mijadala ambayo ilifichua maovu mengi ya mafisadi na utendaji mbovu wa serikali ya JK matokeo yake JK na CCM walimuona Sitta ni msaliti. Inawezekana unajaribu kumtetea Anne Kilango lakini ukweli wa mambo hafai na wala CCM hawatampitisha, lingine kumbuka CCM walimtosa mzee Malecela kwani walikuwa hawamuhitaji tena; Malecela alileta mpasuko mkubwa ndani wakati wa kampeni zake za kutaka kugombea uraisi; leo hii mke wa Malecela awe spika si utakuwa mwendelezo wa mipasuko ndani ya chama? Je jiulize CCM wako tayari kuendelea na migawanyiko ndani ya chama? Kilango na Sitta kuchukua fomu ni kufarahisha nafsi zao. Uteuzi wa spika ndani ya CCM si uchaguzi huru wabunge wa CCM watapiga kura kwa kufuata maelekezo watayopewa na si ridhaa zao.
 
Mkuu safari ni safari,wabunge siyo machifu kwamba lazima awe wa kabila la eneo analowakilisha. ndiyo maana Joseph Mbilinyi (mkinga) ni mbunge wa mbeya mjini kwa wasafwa!

Sikujua hilo...hata Chambiri kapewa na Wabarbeig...ni mwamko mzuri
 
Huyu grace Mugabe (Anne Malechela) anafagilia ufisadi uliofadhili ndoa yake hata Sofia Simba anajua! Kifupi hafai kabisa
hana tofauti na JOSEFINE MUSHUMBUZI, ILA YEYE ANNE KILANGO ANA AFADHALI KIDOGO KWANI HAJAIKIMBIA NDOA YAKE WALA KUINGILIA NDOA YA MWINGINE.
 
William,

You have family connection to this madam, therefore, truth be told, you could never be objective on this matter.
Naomba uniruhusu nirudie tena ulichokisema ili kuhakikisha tuko ukurasa mmoja na mlengwa:

"William,

Una mahusiano ya kifamilia na Mwanamama huyu, kwa hiyo, kusema ukweli, huwezi kamwe kuwa na mawazo huru katika swala hili."
 
- Mama Anne Kilango Malecela, amekuwa mbunge wa muda mrefu sana sasa toka wa kuteuliwa na Rais Mkapa, na hii ni mara ya pili anachaguliwa na wananchi kuwakilisha jimbo lake la Same East,

- Akiwa bungeni, amekuwa mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama, Makamu wa Mwenyekiti Miundo Mbinu, Mwenyekiti kamati ya Maadili ya bunge, kama ni mabifu yangejiotokeza kwenye hizo kamati hasa akiwa Mwenyekiti wa Maadili ya bunge,

- Sheria iko wazi kwamba mbunge yoyote anaweza kugombea na kuchaguliwa kuwa Spika, wananchi wa Same East siamini kwamba wanaweza kumuondoa Waziri maarufu kama Daniel Yona na kumpa Jimbo Mama Kilango, ambaye ni mapepe na hajatulia mambo mengine ni kwa Great Thinkers kutumia common sense japo kidogo tu kabla hutjaandika hapa uwanja mtukufu.


William.

Kile kiwanda cha Tangawizi nasikia ilikuwa geresha! Pesa zilizochangwa zimeenda wapi?
 
Changieni....lakini mkae mkijua kwamba CCM wanaye mtu 'wao' tayari. Duru za siasa ndani ya chama cha mapinduzi zinaainisha kuwa Mh. JK ametoa mwongozo na jina la nani awe spika. Walio karibu na JK wanasema 'mzee' hakufurahia spika Sitta alivyosimamia mijadala mbalimbali katika bunge lililopita ikiwemo issue ya Richmond iliyopelekea kupoteza uwaziri mkuu kwa swahiba wake wa karibu sana Mh. Lowassa ambaye kwa kauli yake Jk anasema 'hawakukutana barabarani'. Hivyo JK hayuko tayari kuruhusu kiti cha uspika kikaliwe na mtu ambaye si "ndiyo mzee" kwa matakwa yake na ya kamati kuu ya CCM.
 
Kama JK kawa Rais, Yeyote anaweza kuwa chochote NCHI hii. Namshangaa tu Yusuph Makamba hajachukua fomu ya USPIKA! Kinana, JSM, Warioba, SAS, Shamsi Vuai Nahodha, Rosta Aziz,.....wanasubiri nini? Hii ndio CCM tulionayo sasa.
 
UNajua uspeaker unaitajai mtu aliyetulia uyu mama ana jazba saaaaaaaaaaaaaaaaaaaana hataweza
 
Back
Top Bottom