DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Mbunge wa zamani wa Muleba Kusini na waziri wa Ardhi katika serikali ya awamu nne Prof. Anna Tibaijuka kupitia ukurasa wake wa Twitter (X) Anaandika;
"Wakati tunasubiri Tume ya Uchunguzi kutupa taarifa na majibu ya kina kuhusu mauaji ya 29 Oktoba, uwajibikaji stahiki na mbinu za kuliponya taifa tusimpe shetani nafasi kutugawa zaidi kwa kisingizio cha propaganda uchwara za udini kwa kuwatumia vijana wasiojitambua kuwashambulia viongozi wa dini zetu mbalimbali.
"Ni fedheha. Kama ilivyo kwa sisi wazee, ni wajibu wa viongozi wa dini wawe wa TEC au BAKWATA au KKKT na CCT kutulea katika maadili mema ya haki na upendo na kutukumbusha amri za Mwenyezi Mungu; Usiue, Usiibe, Usiseme uongo, nkd, ili kudumisha amani.
"Tusiwakasirikie na kuwadhihaki wanapofanya kazi zao vizuri. Ni faida kubwa kuwasikiliza. Ndiyo HESHIMA na HEKIMA."