Tarehe 8/09/2011 siku ya alhamisi , kamati ya siasa wilaya ya njombe ilikutana ktk ofisi za ccm wilaya kujadili mambo mbalimbali likiwemo suala la hali mbaya ya kisiasa kwa ccm baada ya kuchakachua kura za maoni 2010 na agenda ya makao makuu ya wilya mpya iliyo anzishwa hivi karibuni.
Wajumbe waliweka bayana kuwa kuna mpasuko mkubwa katika jimbo la njombe magharibi uliotokana na kuchakachua kura za maoni ambapo mtu aliyepita kwa kura nyingi ni yono kevela lakini kura zilichakachuliwa kwa ushawishi wa philimoni luhanjo na kumuweka Gerson Lwengwe(Naibu waziri maji) ambaye amemjengea nyumba Luhanjo pamoja na kashifa za kufukuzwa Tanroad kwa ufisadi.
Mhe Lwenge alisikika akilalamika nje ya kikao kuwa , wapiga kura wake wanampigia simu na kumutukana na anawafahamu na kumwambia katibu kuwa ubunge wake upo rehani.
Alimwambia kuwa yeye kwa sasa ni kama jiwe.
Baada ya mjadala mkali wameazimia kwamba wabunge wote wilayani humo wachange pesa na kuanza shughuli za siasa kupambana na chadema.
Wajumbe walisema kwamba ccm haikubaliki na watu wengi wanahamia cdm na wanafungua matawi mapya.
Agenda ya wapi iwe makao makuu ya wilaya mpya yalileta mgogoro mkubwa kiasi cha kutoleana maneno makali.
Mh lwenge amehamisisha madiwani 11 wa eneo la igwachanya(anakotoka lwenge) na kuweka matambiko ya kimila na kuweka msimamo kuwa makao lazima yawe hapo na kama watakataa wanahamia chadema.
Philimon Luhanjo naye ameandika barua kutoka ikulu ikitowa maelekezo ya wilaya mpya huku akielekeza makao makuu yake yatakuwa wanging'ombe anakotoka yeye ili kumpa heshima na wakazi wa huko wanasema wasipo fanya hivyo wanakwenda chadema. Luhanjo anapiga debe eneo hilo kwamba yeye ndiye aliyesababisha wilaya hiyo iundwe kwa kumushawishi kikwete.
Maelekezo ya Kikwete yalikuwa ni kutoa wilaya mpya lakini wapi yawe makao makuu aliwachia wahusika wajadili na endapo watashindwa wamwambie awaamulie.
Sasa mvutano huo ulipamba moto na ndipo anna makinda alipo inuka na kutoa uamuzi kuwa suala hilo limeshindikana na kuandaa taarifa ya kumwachia kikwete awamulie watu wa njombe suala ambalo limewakera wazee wa kimila ambao tayari wamesha tambika.
Wakati anamalizia Anna Makinda alianza kuzungumuzia utendaji wa serikali ,mawaziri na wabunge wa ccm ambapo alianza na kumuponda Mh Samweli Sitta kuwa hajui shughuli za bunge na kwaba Anna Makinda amekaa sana bungeni na ndiye aliyemufundisha Sitta Uspika. Aliwambia wajumbe kuwa Sitta ni tatizo kwenye ccm na serikali kwa kuwa ni mwaasisi wa ccj na kwamba Sitta ndiye aliye kuwa anafanya kampeni za kusema Anna Makinda ni mbumbu wa sheria na hajui shughuli za bunge. Aliwambia wajumbe kuwa shughuli za bunge zinaendeshwa kwa kanunni na sio sheria. Na aliwataka wajumbe wamupuuze Sitta kwa kauli zake kwani zina vuruga ccm.