Anna Makinda amponda Sitta kwenye kikao cha siasa Njombe

Mwamakula

JF-Expert Member
Nov 7, 2010
1,891
382
Tarehe 8/09/2011 siku ya alhamisi , kamati ya siasa wilaya ya njombe ilikutana ktk ofisi za ccm wilaya kujadili mambo mbalimbali likiwemo suala la hali mbaya ya kisiasa kwa ccm baada ya kuchakachua kura za maoni 2010 na agenda ya makao makuu ya wilya mpya iliyo anzishwa hivi karibuni.

Wajumbe waliweka bayana kuwa kuna mpasuko mkubwa katika jimbo la njombe magharibi uliotokana na kuchakachua kura za maoni ambapo mtu aliyepita kwa kura nyingi ni yono kevela lakini kura zilichakachuliwa kwa ushawishi wa philimoni luhanjo na kumuweka Gerson Lwengwe(Naibu waziri maji) ambaye amemjengea nyumba Luhanjo pamoja na kashifa za kufukuzwa Tanroad kwa ufisadi.

Mhe Lwenge alisikika akilalamika nje ya kikao kuwa , wapiga kura wake wanampigia simu na kumutukana na anawafahamu na kumwambia katibu kuwa ubunge wake upo rehani.
Alimwambia kuwa yeye kwa sasa ni kama jiwe.
Baada ya mjadala mkali wameazimia kwamba wabunge wote wilayani humo wachange pesa na kuanza shughuli za siasa kupambana na chadema.
Wajumbe walisema kwamba ccm haikubaliki na watu wengi wanahamia cdm na wanafungua matawi mapya.

Agenda ya wapi iwe makao makuu ya wilaya mpya yalileta mgogoro mkubwa kiasi cha kutoleana maneno makali.

Mh lwenge amehamisisha madiwani 11 wa eneo la igwachanya(anakotoka lwenge) na kuweka matambiko ya kimila na kuweka msimamo kuwa makao lazima yawe hapo na kama watakataa wanahamia chadema.

Philimon Luhanjo naye ameandika barua kutoka ikulu ikitowa maelekezo ya wilaya mpya huku akielekeza makao makuu yake yatakuwa wanging'ombe anakotoka yeye ili kumpa heshima na wakazi wa huko wanasema wasipo fanya hivyo wanakwenda chadema. Luhanjo anapiga debe eneo hilo kwamba yeye ndiye aliyesababisha wilaya hiyo iundwe kwa kumushawishi kikwete.

Maelekezo ya Kikwete yalikuwa ni kutoa wilaya mpya lakini wapi yawe makao makuu aliwachia wahusika wajadili na endapo watashindwa wamwambie awaamulie.

Sasa mvutano huo ulipamba moto na ndipo anna makinda alipo inuka na kutoa uamuzi kuwa suala hilo limeshindikana na kuandaa taarifa ya kumwachia kikwete awamulie watu wa njombe suala ambalo limewakera wazee wa kimila ambao tayari wamesha tambika.

Wakati anamalizia Anna Makinda alianza kuzungumuzia utendaji wa serikali ,mawaziri na wabunge wa ccm ambapo alianza na kumuponda Mh Samweli Sitta kuwa hajui shughuli za bunge na kwaba Anna Makinda amekaa sana bungeni na ndiye aliyemufundisha Sitta Uspika. Aliwambia wajumbe kuwa Sitta ni tatizo kwenye ccm na serikali kwa kuwa ni mwaasisi wa ccj na kwamba Sitta ndiye aliye kuwa anafanya kampeni za kusema Anna Makinda ni mbumbu wa sheria na hajui shughuli za bunge. Aliwambia wajumbe kuwa shughuli za bunge zinaendeshwa kwa kanunni na sio sheria. Na aliwataka wajumbe wamupuuze Sitta kwa kauli zake kwani zina vuruga ccm.
 
nchi yetu kweli imeoza. Hamna hata utaratibu / vigezo vya kuchagua makao makuu ya wilaya, sasa hawa mafisad wanajivutia kwao as if wilaya ni mali yao.
 
Anna bwana
sasa yeye ni spika wa bunge tena anasema anajua vizuri kanuni
yeye na Kikwete kuna tofauti kubwa? si hawa wote ni viongozi wa kitaifa
tena yeye anaongoza wabunge wenye mahusiano ya moja kwa moja na wananchi
imekuwaje ameshindwa kutatua suhala la wilaya mpaka Kikwete?

ina maana hata pale bungeni yana mshinda na kuomba msaada kwa Kikwete?
huku ni kuudhalilisha uspika bana,
spika anashindwa ushawishi wa wapi yawe makao makuu ya wilaya?
 
Wanaoamua wapi Makao makuu ya Wilaya/ Mkoa yawe ni wakazi wa Wilaya/Mkoa husika, jambo hili halina uwakilishi, ninawashangaa (kama ni kweli) hao viongozi wa CCM wanaotaka kuandika Kwa Rais kuwa jambo hilo limeshindikana. Kwani wakazi wote wa Njombe ni wana CCM? Hakuna wana CHADEMA? Hakuna wasio na vyama?
 
Anna Makinda hana ubavu wa kushindana na Mh.Sitta kwani hata Uspika kapewa tu ili kulinda mafisadi,na akitaka kujimaliza aanze kushindana na Sitta.Alianza kwa kuwaonea Wabunge wapinzani aliposhitakiwa kwenye tume ya maadili akapunguza uonevu bila kutolea ufafanuzi mashitaka dhidi yake.
 
Mh! Kumbe ccmagamba wanaendesha mambo yao kutokana na pressure from chadema, ''msipofanya hiv tutahamia chadema'', nimefarijika sana; karibuni nyooote!
 
Wakati Mama Anna Makinda anaingia bungeni kwa mara ya kwanza John Mnyika hakuwa amezaliwa (plse correct me if I am wrong). Lakini Mnyika anamtoa kamasi huyu mama when it comes to Kanuni za Bunge. Tatizo la watu kama mama Makinda ni kufanya kazi kwa KUKREMU kwa sababu tu uliambiwa hivyo. Kanuni za bunge ni muongozo wa kisheria, na sheria hazisomwi in ISOLATION na hili liko wazi kabisa. Sasa sijui Mama Makinda ana utaalam gani kusoma sheria kuliko Mh Sitta ambaye amesomea sheria. Naamini leo hii kungefanyika utafiti huru juu ya nani wananchi wanaamini ana uwezo wa kuongoza bunge kati ya Mh Sitta na Mama Makinda sidhani kama angefua dafu. Bahati mbaya sana tunaona kila kitu LIVE TBC.

NB: Hukumu juu ya madai ya Lema, Zitto, Lissu yako wapi mama Makinda kama kweli wewe unajua kuongoza bunge?
 
Mzeee 6 yule aliysema wapinzani wanafiki?du!hivi alishakabidhi nyumba ya spika wa mjengo?baada ya kutoswa uspika na wana wa magamba.
 
Wote hawana jipya kwani kuendesha harakati ndani ya magamba ni sawa na kumpigia m buzi gitaa.WAENDE IGUNGA KUSAIDIA KAMPENI kwani hasimu wake RA.
 
Hivi Makinda ndio nani nchi hii? Kwanza kwanini anapita bila ya kupingwa kila wakati? CDM hebu mfungieni kazi huyu mama.
 
Tarehe 8/09/2011 siku ya alhamisi , kamati ya siasa wilaya ya njombe ilikutana ktk ofisi za ccm wilaya kujadili mambo mbalimbali likiwemo suala la hali mbaya ya kisiasa kwa ccm baada ya kuchakachua kura za maoni 2010 na agenda ya makao makuu ya wilya mpya iliyo anzishwa hivi karibuni.

Wajumbe waliweka bayana kuwa kuna mpasuko mkubwa katika jimbo la njombe magharibi uliotokana na kuchakachua kura za maoni ambapo mtu aliyepita kwa kura nyingi ni yono kevela lakini kura zilichakachuliwa kwa ushawishi wa philimoni luhanjo na kumuweka gerson lwengwe(naibu waziri maji) ambaye amemjengea nyumba luhanjo pamoja na kashifa za kufukuzwa tanroad kwa ufisadi.

Mhe lwenge alisikika akilalamika nje ya kikao kuwa , wapiga kura wake wanampigia simu na kumutukana na anawafahamu na kumwambia katibu kuwa ubunge wake upo rehani.
Alimwambia kuwa yeye kwa sasa ni kama jiwe.
Baada ya mjadala mkali wameazimia kwamba wabunge wote wilayani humo wachange pesa na kuanza shughuli za siasa kupambana na chadema.
Wajumbe walilaamum kwamba ccm haikubaliki na watu wenge wanahamia cdm na wanafungua matawi mapya.

Agenga ya wapi iwe makao makuu ya wilaya mpya yalileta mgogoro mkubwa kiasi cha kutoleana maneno makali.

Mh lwenge amehamisisha madiwani 11 wa eneo la igwachanya(anakotoka lwenge) na kuweka matambiko ya kimila na kuweka msimamo kuwa makao lazima yawe hapo na kama watakataa wanahamia chadema.

Philimon luhanjo naye ameandika barua kutoka ikulu ikitowa maelekezo ya wilaya mpya huku akielekeza makao makuu yake yatakuwa wanging'ombe anakotoka yeye ili kumupa heshima na wakazi wa huko wanasema wasipo fanya hivyo wanakwenda chadema. Luhanjo anapiga debe eneo hilo kwamba yeye ndiye aliyesababisha wilaya hiyo iundwe kwa kumushawishi kikwete.

Maelekezo ya kikwete yalikuwa ni kutoa wilaya mpya lakini wapi yawe makao makuu aliwachia wahusika wajadili na endapo watashindwa wamwambie awaamulie.

Sasa mvutano huo ulipamba moto na ndipo anna makinda alipo inuka na kutoa uamuzi kuwa suala hilo limeshindikana na kuandaa taarifa ya kumwachia kikwete awamulie watu wa njombe suala ambalo limewakera wazee wa kimila ambao tayari wamesha tambika.

Wakati anamalizia anna makinda alianza kuzungumuzia utendaji wa serikali ,mawaziri na wabunge wa ccm ambapo alianza na kumuponda mh samweli sitta kuwa hajui shughuli za bunge na kwaba anna makinda amekaa sana bungeni na ndiye aliyemufundisha sitta usipika. Aliwambia wajumbe kuwa sitta ni tatizo kwenye ccm na serikali kwa kuwa ni mwaasisi wa ccj na kwamba sitta ndiye aliye kuwa anafanya kampeni za kusema anna makinda ni mbumbu wa sheria na hajui shughuli za bunge. Aliwambia wajumbe kuwa shughuli za bunge zinaendeshwa kwa kanunni na sio sheria. Na aliwataka wajumbe wamupuuze sitta kwa kauli zake kwani zina vuruga ccm.
Si kweli kwamba Yono Kevela ndie aliyeongoza kura za maoni bali aliyeongoza na kuchakachuliwa ni Thomas Nyimbo
Kuhusu makao makuu ya Wilaya pamoja na kwamba simuungi mkono Lwenge kama Mbunge lakini ukweli unabaki pale pale Igwachanya ndio mahali sahihi pa kuweka makao makuu kwani ni katikati ya Wilaya na kuna miundombinu ya kutosha kama hospitali, shule, usafiri, barabara n.k
 
Msipofanya hivi nitahamia Chadema
Msipofanya vile nitahamia Chadema
Mkitekeleza hili nitabakia CCM
Mkitekeleza lile nitabakia CCM
Nikibakia CCM msipotekeleza mliyoahidi nitahamia chadema
 
Nyimbo anafungua matawi ya chadema huko Njombe vijijini kama vile hana akili nzuli; hilo ndilo linawapa wasiwasi hao watu wa ccm!!
 
Anna achana na habari za SIX utajiabisha bure,
Haya makao makuu wananchi ndio waamue wenyewe yawe wapi, msiwaamulie
luhanjo na Lwenge, wote inaonekana ni tatizo kwa maendeleo ya Njombe.
 
Habari zingine nzuri sana kwa wanamapinduzi,sasa na sisi tuseme hivi rais asipo tataue matatizo ya umeme,mfumuko wa bei,kuanguka kwa pesa yetu,epa,meremeta,iptl na mengine tunamtoa madarakani na kuipa chadema 2015.peopleez power.cdm wanasumbua magamba am happy to hear that.thanks.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom