Anna Makinda amponda Sitta kwenye kikao cha siasa Njombe

hapa kazi ipo, kamati ya siasa ya CCM ni nini hadi iamue makao makuu ya wilaya mi nadhani watu wote wa Njombe ndiyo waamue kama kuna utata basi kura zipigwe

Luhanjo, Lwenge waamini wazi kuwa cheo ni dhamana na siyo rungu au kuonyesha kuwa wao ni mwarobaini wa watu wa Njombe.

Spika makinda atofautishe bunge la kabla ya SS, bunge la SS, bunge lake ajue kuwa SS ndiye aliye fanya bunge liwe na mvuto kwa watu na alikuwa na ngozi ngumu ktk siasa za maji taka.
 
Nyimbo anafungua matawi ya chadema huko Njombe vijijini kama vile hana akili nzuli; hilo ndilo linawapa wasiwasi hao watu wa ccm!!
usipime kabisa kasi ya chadema njombe inatisha,maeneo kama ya lupembe,igwachanya boimanda,kifanya,mdandu,ilembula kote huko nyimbo kachakaza na raia huwaambii kitu juu ya chadema. Hata uchaguz mdogo wa diwani wa kata ya mji mwema ccm hawapati kitu.
 
Ikiwa kama kweli Mama Anna kasema hivyo kuhusu Mh. Sitta, atakuwa amefanya kitu cha hatari sana ktk siasa zza CCM. Nina uhakika, Mh. Sitta akidhibitisha hili lazima atalijibu, tena jibu lake litakuwa kombora!
 
Huwez amin.jana 9/09/011 ilikuwa ni cku ya kurudisha fomu za wagombea uchaguz wa diwan kata ya mji mwema njombe mjin.cha kushangaza wakat wa urudishaj wa fomu mida ya saa 5am ccm walikuwa na msururu wa magar kam 20 ulioanzia ofis ya chama wilaya(turbo),hakuna hata raia mmoja aliyeshabikia kila mtu alikuwa busy na shughuli zake..mida ya saa 7 CDM nao walianza msafara wao wa kurudisha fom ukianzia ofis za chama haukuwa na magari meng sana kwn hta 10 hayakufika,but walipofika maeneo ya stend ya njombe,raia walijiunga na msafara huo,mwenye baiskel,aliyetembea kwa miguu,tax na magar binafs yakajoin ukawa bonge la msafara utafikir ni Dr. Katua njombe. Nakuambia ccm ina kaz ya ziada 2015 kushinda uchguz.
 
Tarehe 8/09/2011 siku ya alhamisi , kamati ya siasa wilaya ya njombe ilikutana ktk ofisi za ccm wilaya kujadili mambo mbalimbali likiwemo suala la hali mbaya ya kisiasa kwa ccm baada ya kuchakachua kura za maoni 2010 na agenda ya makao makuu ya wilya mpya iliyo anzishwa hivi karibuni.

Wajumbe waliweka bayana kuwa kuna mpasuko mkubwa katika jimbo la njombe magharibi uliotokana na kuchakachua kura za maoni ambapo mtu aliyepita kwa kura nyingi ni yono kevela lakini kura zilichakachuliwa kwa ushawishi wa philimoni luhanjo na kumuweka gerson lwengwe(naibu waziri maji) ambaye amemjengea nyumba luhanjo pamoja na kashifa za kufukuzwa tanroad kwa ufisadi.

Mhe lwenge alisikika akilalamika nje ya kikao kuwa , wapiga kura wake wanampigia simu na kumutukana na anawafahamu na kumwambia katibu kuwa ubunge wake upo rehani.
Alimwambia kuwa yeye kwa sasa ni kama jiwe.
Baada ya mjadala mkali wameazimia kwamba wabunge wote wilayani humo wachange pesa na kuanza shughuli za siasa kupambana na chadema.
Wajumbe walilaamum kwamba ccm haikubaliki na watu wenge wanahamia cdm na wanafungua matawi mapya.

Agenga ya wapi iwe makao makuu ya wilaya mpya yalileta mgogoro mkubwa kiasi cha kutoleana maneno makali.

Mh lwenge amehamisisha madiwani 11 wa eneo la igwachanya(anakotoka lwenge) na kuweka matambiko ya kimila na kuweka msimamo kuwa makao lazima yawe hapo na kama watakataa wanahamia chadema.

Philimon luhanjo naye ameandika barua kutoka ikulu ikitowa maelekezo ya wilaya mpya huku akielekeza makao makuu yake yatakuwa wanging'ombe anakotoka yeye ili kumupa heshima na wakazi wa huko wanasema wasipo fanya hivyo wanakwenda chadema. Luhanjo anapiga debe eneo hilo kwamba yeye ndiye aliyesababisha wilaya hiyo iundwe kwa kumushawishi kikwete.

Maelekezo ya kikwete yalikuwa ni kutoa wilaya mpya lakini wapi yawe makao makuu aliwachia wahusika wajadili na endapo watashindwa wamwambie awaamulie.

Sasa mvutano huo ulipamba moto na ndipo anna makinda alipo inuka na kutoa uamuzi kuwa suala hilo limeshindikana na kuandaa taarifa ya kumwachia kikwete awamulie watu wa njombe suala ambalo limewakera wazee wa kimila ambao tayari wamesha tambika.

Wakati anamalizia anna makinda alianza kuzungumuzia utendaji wa serikali ,mawaziri na wabunge wa ccm ambapo alianza na kumuponda mh samweli sitta kuwa hajui shughuli za bunge na kwaba anna makinda amekaa sana bungeni na ndiye aliyemufundisha sitta usipika. Aliwambia wajumbe kuwa sitta ni tatizo kwenye ccm na serikali kwa kuwa ni mwaasisi wa ccj na kwamba sitta ndiye aliye kuwa anafanya kampeni za kusema anna makinda ni mbumbu wa sheria na hajui shughuli za bunge. Aliwambia wajumbe kuwa shughuli za bunge zinaendeshwa kwa kanunni na sio sheria. Na aliwataka wajumbe wamupuuze sitta kwa kauli zake kwani zina vuruga ccm.

Magwanda mna mambo sana. Yaani mnajitungia habari ili iendeleze stori za jamvini. Kweli kazi ipo
 
Si kweli kwamba Yono Kevela ndie aliyeongoza kura za maoni bali aliyeongoza na kuchakachuliwa ni Thomas Nyimbo
Kuhusu makao makuu ya Wilaya pamoja na kwamba simuungi mkono Lwenge kama Mbunge lakini ukweli unabaki pale pale Igwachanya ndio mahali sahihi pa kuweka makao makuu kwani ni katikati ya Wilaya na kuna miundombinu ya kutosha kama hospitali, shule, usafiri, barabara n.k
Uko sahihi sana bwana Gerrad. Watu kama Luhanjo wakubali ukweli huo na waache kutumia nafasi zao serikalini kulazimisha mambo. Sio sahihi kuweka makao makuu Wanging'ombe ambako ni kukame sana.
 
Hakuna ushahidi wowote umeonyesha makinada sio fisadi, mwongo, hajui sheria wala hana background yeyote ile ya sheria na hakuna signs zozote makinda ni kiongozi Tanzania.

Makinda ndio anachangia sana umaskini na kuua demokrasia ya Tanzania. Poleni sana wananchi wa Njombe na tunawaomba mumfukuze.

 
Uko sahihi sana bwana Gerrad. Watu kama Luhanjo wakubali ukweli huo na waache kutumia nafasi zao serikalini kulazimisha mambo. Sio sahihi kuweka makao makuu Wanging'ombe ambako ni kukame sana.
Licha ya ukame Mkuu, hebu fikiri mtu anayetoka Igagala, Usalule, Makoga, Igosi, Wangama au Kipengere atafikaje Wanging'ombe bila kuzunguka Njombe Mjini? Iko wapi dhana ya kusogeza madaraka kwa wananchi? Si ni afadhali kuanzia Mdandu wabaki kwenye wilaya ya Njombe?
 
Hii safi, Tanzania inahitaji chama mbadala ili kiweze kuwa tishio kwa chama kilichopo madarakani kiweze kuwaletea wananchi maendeleo kwani kitakuwa kinajua bila wananchi kunufaika watapigwa mweleka, na wananchi inabidi waelimishwe kwamba chama kisicho waletea maendeleo wasikichague. Kuleta maendeleo ni kwa kuweka sera nzuri za kodi,elimu,afya, nk pia kuwe na viongozi wanaowajibika. Mwanzo mzuri tutafika
 
ukweli ni kwamba Ana Makinda amechakachua Bunge na sasa anatetea Mafisadi kwa Kukandamiza Hoja za Wapinzani Sitta alikuwa anajali Haki sawa kwa wote
 
Bunge ni Chombo cha kutunga sheria na sio kanuni.Hivyo lazima kiongozi mkuu wa Chombo hicho ajue Sheria na sio Ushirikina .
 
KWA NINI VYAMA VINGINE HAVI HUSIKI KATIKA MAAMUZI YA WAPI YAWE MAKAO MAKUU YA WILAYA? Kwa sababu makao makuu ya Wilaya sio ccm Mak
 
Mhe. Nyimbo ongeza kasi ya kufungua matawi ya cdm ili waendelee kuraruana kwenye vikao. Hivi kumbe makao makuu ya wilaya yanaamuliwa kwa mapenzi ya mtu tu na siyo kuna vigezo rasmi!!! Haka kanchi hakataisha vioja.
 
Maamuzi ya Wananch wa Njombe waachiwe wao wenyewe na sio waingiliwe na Makundi ya Maeneo Mengine. Mbona Znz waliachiwa?
 
Anna achana na habari za SIX utajiabisha bure,
Haya makao makuu wananchi ndio waamue wenyewe yawe wapi, msiwaamulie
luhanjo na Lwenge, wote inaonekana ni tatizo kwa maendeleo ya Njombe.

sheria ya serikali za mitaa ya mwaka 1982 RE 2000 Sec.5(1-5) inatoa mamlaka kwa waziri mwenye dhamana na serikali za mitaa kuanzisha halmashauri ya wilaya. na contents of establishment zinatajwa sec.6(a-c). procedures for establishment sec 7(1-5)
sasa huu uhuru wa mayani kujiamulia wapi yawe makao makuu ya wilaya unatoka wapi? na kama maombi ya awali ya uhitaji wa kuanzishwa kwa halmashauri mpya kwenda kwa waziri mhusika yalitoka kwa wananchi(baraza la madiwani) mihutasari ilikuwa inasema wilaya hiyo mpya iitwe jina gani? na makao makuu yawe wapi? na kama waziri alilizia kuanzishwa kwa wilaya hiyo je, alifanyia marekebisho yoyote kwa vigezo vya awali?

kimsingi sioni sababu ya hili nalo kuwa ishu? na kwa upande wa pili naona hii ndiyo gharama ya Democracy kugeuka uhuru wa manyani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom