Galacha Maestro
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 1,353
- 2,231
BARUA KWA ANITA
-1-
Mpenzi Anitha, Salam sana.
Ama baada ya Salam nakuombea Kwa Mungu akupumzishe mahala Pema Peponi.
Dhumuni la Barua hii Ni Kukujulisha Kuwa yale yalikuwa makosa yangu,
Hili Ni haki Yangu, Acha yanikute, Acha niteseke,
Acha iwe fundisho kwa wengine, Acha niwe Mfano ili kuinusuru jamii,
Acha iwe ilivyo, Acha Niuchomoe mwiba.
Anitha my Love, Rafiki yangu nakuita naomba itika.
Nakuita itika nikwambie yalo mtimani mwangu,
Itika uzungumze na Moyo wangu,
Itika ninusuru Wenzangu,
Itika nikueleze la mbali moyoni mwangu.
Anita mpenzi wa penzi lililochipua katikati ya mabonde, mito na vilima,
Likamea kwa shida mfano wa mbegu za mibuni ama Tende Jangwani pasipo maji kumwagiliwa.
Likawa Penzi maridhawa lililowashinda Wafitini,
Penzi zito lililogandamana mithili ya sumaku kwenye vyuma vya mioyo yetu..
ANITHA nakumbuka jinsi ulivyosisitiza liwe penzi la kirafiki tu na Jinsi kinafki nilivyoitika SAWA
Napoukumbuka msimamo wako huu Roho inaniuma, Nafsi inanisuta na Majuto makali huniandama hasa Ninapojiangalia kwenye kioo na kujiona ni-dhaifu sana
Mwili umechoka Sura imenikakamaa hata Tumboni ile mikunjo ya Six Packs sasa haipo tena.
Nikiitizama ile picha uliyonipiga siku ile pale gym kwa Derick nayaona machozi yaso kilio cha sauti yakifunika kope za macho yangu,
Nauona Mzigo dunia ukinielemea kichwani mwangu na hakuna wa kuushusha,
Najiona si lolote si chochote na ninabaki nalia.
ANITA my Love Mrembo Usie na makuu,
Msichana Mzuri asilia uso mfanowe.
Mwenye ngozi laini usiyepaka lotion.,
Mwenye harufu murua usijipuliza manukato kuumiza pua za wapitao karibu yako.
Mwenye mwendo ushangazao na kuwa kazi kuhukumu ni wa maringo au majigambo.
Anita Mpenzi rangi yako ya Udhurungi Sio Cheusi Mangala Kama Zuzy, Nywele zako Singasinga sio Kipilipili kama Lucy,
Umbo lako No 8 sio La Simba kama Manka,
Mguu wako wa bia Sio hii Milonjo Ya Aisha na Sauti Nyembamba ya Upole kama muimba nyimbo za kuabudu.
Anita Msichana wa kianalogia katika ulimwengu wa kidigiti,
Usiye na hofu juu ya uzuri asilia aliokubariki M/MUNGU.
Mtanashati Msamawati uliye Mmaridadi wa short kati niliyependa nikafa nikaoza.
Anita Wewe uliyejipaka Mafuta ya mgando aina ya La Belle ukavutia, Uliyejifukiza udi ukanukia,
Mrembo Uliyejaa adabu utii na upendo kwa watu wa rika zote,
Usiye na makuu na yeyote yule,
Uliyejaa Vigezo vya kuwa Mke bora au Mama na Mlezi wa familia yeyote.
Mimi nilikuwa nani hata nisikutamani?
Anita Sina Mengi zaidi ya Kukuomba Msamaha,
Naomba unisamehe.
Nakiri nilikukosa, Najutia Sikujua mapema Lakini naomba kusamehewa..
ANITA mimi ni Binadamu makosa ni jadi yetu naomba nisamehe mwenzako maana teyari nipo hoi bin taaban kitandani watu wanangoja waleo wakesho..
Pakikucha wanadhani mchana pakichwea wanadhani usiku lakini Mungu ndie pekee ajuae siku na saa kamili.
Anita Mwenzio sina hamu ya kuishi na kujiua siwezi,
Tena kumeza dawa hizi ndio kero kero kero iitesayo nafsi yangu, na Daktari kasema nitameza siku zote za maisha yangu.
Anita mpenzi huku mwenzako sina anayetamani kunigusa, kila mtu anionea huruma.
Wengi wanatamani nife wapumzike, Wanatamani nife hata kabla ujumbe wa BARUA hii haujawafikia Kina mimi Wengine waliojaa humu duniani,
Najiona mpweke nisiye na cha kuniliwaza,
Nimebaki kuwa mtu wa huzuni Asubuhi, Mchana mpaka jioni,
Sikumbuki hata lini ilikuwa mara ya mwisho kucheka.
Anita Najutia uamuzi wangu,
Najutia ushauri ule,
Najutia nguvu kubwa niliyoitumia kujilazimishia kiama hiki, Najutia zaidi napokumbuka jinsi ulivyolia na kujitahidi kujinasua lakini nikakuzidi nguvu, nayaona mengi Anita ila sisemi wazi na hata nikitaka kusema sina wa kumhadithia.
Anita Ndotoni nauona moto wa jahanamu ukiichoma Roho yangulakini Nikishtuka najiona hai, Nikifumba macho taswira yako inanijia tena ni ile umevalia gauni jekundu siku ambayo uliniambia nisiharakie maisha,
Siku ambayo ulinisisitiza kuchunguza kwanza jambo kabla ya kulitolea Hukumu au kulifanyia Maamuzi,
Roho inaniuma nafumbua macho naanza kulia...
Anita najua nilililia wembe ukauchukua ukauweka Mbali,
Nikaenda kuutafuta na kujikata,
Anita Natamani uinuke uniangalie nikilia nikuombe msamaha lakini haiwezekani
Natamani niweze kuja kukukiss busu la mwisho niseme fika salama laazizi mahabuba lakini siwezi.
Natamani ninyanyuke niinue mikono juu nikuombee lakini nashindwa.
Anita Mimi nilikuwa SIKIO LA KUFA nisingeweza Kusikia dawa, Nilikuwa mtu wa kushawishi tu pasipo kujiuliza kwa nini ulikataa,
Sikuwa nikiwaza upande wa pili maana moyo na nafsi vyote vilijaa hashki na hisia za kutaka Penzi lako.
Anita Ninaposema nateseka kwa majuto naomba uelewe ninapata uchungu sana hata naposoma Biblia na kuona huu mstari kwamba JIWE WALIOLIKATAA WAASHI LIKAWA JIWE KUU LA PEMBENI
Anita juzi walikuja watu wa maombezi nilitamani niwahadithie nikasita, Juma nae aliponipa Kisa cha SEND OFF ya John ilivyompatia GHONO na sasa anachomwa sindano kali nilitaka kumwambia nikasita.
Anita Naomba niwe shahidi hapa duniani na kesho Juu Mbinguni kwamba mimi ndiye chanzo cha yote haya,
Naona machozi yakinibubujika, vidole vikigoma kuandika huu UKWELI MCHUNGU.
Anita sijui kwanini vidole vinasita lakini naomba nijitahidi kuweka mambo hadharani
Nataka wasichana wapate funzo na kujua watajikinga vipi na akina sisi na wavulana vivyo hivyo kupitia Mimi.
Anita wewe teyari Mimi nitakufata siku sio nyingi.
.
Anita Siku ile ulikataa kuja nikalazimisha, uliposema hutaki mapenzi sikujua lengo nilihisi ni kama wengine tu ambao hubana bana mwanzoni na baadae huachia.
Nilijua wewe ni msichana kama wasichana wengine,
Sikujua ulikuwa msichana wa tofauti sana uliyeishi mjini miaka mingi lakini ukionekana kama bado mlokole flani hivi kwa jinsi ambavyo ulijiweka,
Anita ujue mimi nilidhani ulinipenda na kwamba ulitamani nikuoe ndio nile tunda kumbe hukuwa na lengo hilo?
Anita nilipambana sana kuhakikisha nalionja penzi lako toka kitambo na wewe ndio ulinizidisha hamu uliponieleza U-BIKIRA na hutaki ipoteza mpaka kiama.
Anita sikutaka uzikwe na bikira yako, sikutaka ufe kigoli, nilitaka uyaone maumivu ya kumwagika damu, Nilitaka uwe mwanamke na sio msichana kumbe ilikuwa kinyume chake.
Anita ni ATHUMANI rafiki yangu kipenzi alinishauri nikuwekee madawa,
Nami nikakuwekea kwenye juice ya Passion juice ambayo uliipenda sana.
Anita sikuwa na wazo hili lakini nililiafiki kwa kuwa nilitamani niione bikira yako kwani nilishatembea na wasichana wengi na hakuna bikira kati ya hao niliyembahatika.
Anita sikuwahi kukuhadithia lakini niliwahi kutoka na binti mdogo wa Form II ajabu alikuwa ameshapitiwa, Nikashangaa msichana wa miaka 27 aliyemaliza chuo kikuu mwenye kazi yake nzuri vipi uwe bikira?
Anita nilitaka kuiona bikira yako nijue ni fake au original
Nilitaka niitoe mwenyewe kumbe najikatia ticket kusafiri na basi nisilolipenda.
Anita hata uliponiambia huitaji kuolewa nilihisi ni masahibu ya mapenzi uliyokumbana nayo hapo kabla yamekukatisha tamaa nikajiandaa kuirejesha amani uliyoipoteza kumbe kazi bure sawa na kutafuta mabasi ya kwenda Zanzibar.
Anita pamoja na Madawa yale lakini bado ulionekana kupambana kujibana lakini muda ulivyozidi kwenda nguvu zilikuishia na hapo nikaona umeanza kulia na kulaumu kunijua, ukalaumu sana na kunilaani ukasema mimi ni mnyama lakini ndio kwanza nikawa najipa moyo na kukuambia nayafanya yale kwa kuwa nakupenda sana..
Anita hata nguvu zilipokuishia na kuona huna cha kufanya niliona uliniomba sana nitumie KINGA,
Nikikataa eti kwamba Hakuna bikra itolewayo kwa Condom,
Nakumbuka ulilia sana hata nilipomaliza na Kukuomba msamaha kwamba ni shetani tu alinivagaa bado hukuhitaji Kunisamehe.
ANITA nikifikiria uliposema
"Sitaki Mimi ni MUATHIRIKA"
huku ukilia sana roho inavimba nahisi nyongo inapasuka najisemea mwenyewe Mungu upo wapi uanze kuniadhibu?
ANITA nayakumbuka maneno yale nayaona machungu, nakumbuka majibu yangu kwamba NATAKA TUFE SOTE na leo umekwenda peke yako Naumia sana.
Nimepanga siku unazikwa niombe muda baada ya Risala nitoe waraka huu, niwaambie watu yote kuhusu mimi na wewe, nimwambie ATHUMANI asitoe ushauri kama ule tena, niwaambie nduguzo uliupanga UFE NA BIKIRA YAKO ili kumdhibitishia MUNGU hukuupata UKIMWI kwa kufanya zinaa bali uliupatia kwenye ajali ile ya Dodoma ulipokuwa form II Unaenda shule lakini hujafanikiwa kufa na Bikira yako sababu ya shetani mimi.
ANITA nitawaambia pia ulitamani sana baba na mama yako wasijue umeathirika na uthibitisho wa message yako ile ya MSONGO MKALI WA MAWAZO uliokuandama mpaka mauti yanakukuta nitawaonesha..
Anita wengi hulia na waliowaambukiza maradhi haya ila mimi ni tofauti, naomba niliye na MOYO WANGU,
Nilie na ushauri mbovu wa ATHUMANI,
Nilie na halmashauri mbovu ya kichwa changu licha ya kunisihi nisithubutu kuingiza mkono kwenye moto sikusikia Nikaingiza kwa makusudi.
Anita SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA Niombee CD4 zipande kidogo maana zimeshuka sana, zikipanda nikapata nguvu kidogo nitaokoka na kila siku nitakuombea DUA M/MUNGU akulaze mahala pema Peponi.
Wako Rafiki Kipenzi, Based on true story.. happened to my friend...