Ng'wanangwa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 10,827
- 4,174
nimemaliza kusoma kitabu kimoja kinaitwa Animal Farm cha George Orwell.
kitabu hiki kinaeleza kisa cha wanyama walioamua kuasi na kumtimua bwana shamba wao. wakafanikiwa. wakabaki kujitawala wao bahati mbaya kiongozi wa mapinduzi Bwana Major akafariki. wakabaki waliobaki ila katika hao waliobaki ikaaminiwa kuwa nguruwe ndiyo walikuwa wenye akili kuliko wanyama wote. wakawa ndiyo haswa wakubwa wa kazi. maguruwe wawili Napoleon na Snowball wakawa ndiyo viranja wakuu wakipanga mikakati ya kila namna ya kuishi katika shamba lile. hata bwana shamba wao alipojaribu kurejea alishindwa vibaya.
kutokana na wanyama wengine kuamini kuwa maguruwe ndo wenye akili basi maguruwe nao wakatumia fursa vizuri. ikawa chakula kizuri wanakula wao, malazi na mavazi bora wao na kila kitu kizuri chao. lakini pamoja na hayo bado wanyama wengine walizidi kuamini kuwa bwana napoleon na snowball ndiyo wenye akili wengine maboya tu. kuna siku mnyama mmoja akinywa maji aliyasifu kuwa ni maji yenye ladha nzuri na yote hiyo ni kwa sababu ya mkubwa wa kazi napoleon.
hata hivyo napoleon na snowball walipishana lugha na bwana napoleon akaamuru mijibwa wamfukuzie mbali bwana snowball akapotelea alikopotelea. kwa misemo ya kisasa bwana snowball alitumbuliwa jipu. ikawa katika kutumbuliwa huko kwa bwana snowball bwana napoleon akapat mwanya wa kusingizia kuwa katika lolote baya linalotokea bwana snowball anahusika na njama. kukiwa na njaa anasingiziwa snowball, kukiwa na ukame sababu ni snowball.
hali ilikuwa mbaya pale bwana napoleon , baada ya masuala ya kuongoza kumuwia ugumu akaanza kuwasingizia baadhi ya wanyama kuwa wanamhujumu kwa ushirikiano na muasi aliye mafichoni - snowball. ikaitishwa 'asembo' siku ya siku na wale wote waliohisiwa washirika wa muasi snowball wakachinjwa hadharani. utawala wa kidikteta ukawa dhahir shahir.
muda utasema...